A God can be a mere theory, nothing more

Kwani wewe nae hauamini mungu?
Mungu wangu aweza kuwa tofauti kwani siamini kuna ahera au moto wa milele. Jehanamu na ahera vipo hapahapa duniani. Viumbe vyote hai kwenye umauti ni sawa. game finito. Ukiishi maisha ya wema ahera yako ni ndani ya mioyo ya watu hai. Ukiwa muovu vivyo hivyo jehanamu yako ni ndani ya mioyo ya watu hai. Jamii hai inabidi ikuhukumu kwa wema au uovu wako ungali hai...siku njema
 

Hahahaaaa! Mkuu hizi stori za shetani zinamkanganyiko mkubwa sana. Idea or story ya Shetani kwa wakiristo inachanganya sana. mara waseme roho, mara malaika, vile vile wanachanganya kati ya shetani na jini na hapo ndipo wanaponiacha hoi coz kunamajini wakiristo pia kama kulivyo na majini waislamu (Ruhani)

Idea ya malaika kati ya uislamu na ukiristo inatofautiana sana. coz ktk uislamu malaika ni sinless na hawaja wahi wala hawatowahi kumuasi Mungu. Chaajabu hapo kila mmoja anajiona yupo sahihi kuliko mwenzie. Hizi dini hizi, wee acha tu!!
 

Haujajibu swali mkuu..unaamini mungu au hauamini?
 

Tatizo lako la msingi ni kutotambua na kulazimisha Dini ya Kiislam na Umani ya Kikristo kuwa zinamwabudu Mungu mmoja, hiyo ndiyo sababu ya kuchanganyikiwa kwako. Ungejua Kila mmoja anaabudu Mungu wake japo kila mmoja anampa Sifa na ukuu sawa wala udingehangaika kulinganisha matango na viazi.
Mungu anayeabudiwa na Wakristo sie Mungu anayeabudiwa na Waislam.
Ukitambua hilo utakuwa na uwezo wa kuchambua mambo ya Mungu na kuyaelewa.
Mungu wa Wakristo anaweza kuwa na mwana pasipo mke... Kwa kuwa ni muweza wa yote
Mungu wa Waislam hayumkiniki awe na mwana ili hali hana mke...

Sijui kama utaelewa ...
 

Sikuelewi naona namna unavyojichanganya. Unachanganya matatixo wa watu binafsi na kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu.

Unajuchanganya sanaaa.
Kiasi huwezi kutofautisha tatizo la uelewa kwa MTU mmoja mmoja na kile asichokielewa. Wewe unaaminj kutokuelewa kitu kunatokana na kitu husika pasipo kutafakari tatixo linaweza kuwa ni mhusika mwenyewe.

Ni ngumu Sana kufundisha MTU wa aina yako.
Unamtafakari Mungu kwa kuangalia petty issues za wanaoaminj uwepo wako ?

Ukiambiwa unakariri mambo yasiyo na mantiki na kutengeneza mantiki zako zisizo na maana huelewi, tungekuwa upande wako tungehitimisha sawa na wewe kwamba huelewi kwa kuwa Mungu yupo na wewe hujitambui
 
Last edited by a moderator:

Wakristo walichokifanya ni kutumia kisa cha Mfalme mmoja(ni binadamu) hivi ambaye ndiye alitamka hayo maneno ambayo wao wakristo wanasema aliyatamka Malaika. Kwahiyo kiukweli hakuna Malaika aliyetamka tamka maneno ya kumuasi Mungu,na hata tukianza kuchambua kisa kizima hapa utaona wazi kuwa hakiendani kabisa na Malaika na ndiyo maana Idea yao ya Shetani haina uhalisia.
 

Tatizo la msingi ni kukosa kujuamini kwa Waislam na Uislam wao.
Allah sio Yhwh period.
Chambua malaika/shetani kwa mtazami huo lakini ukuweka kwamba wote ni sawa na tofauti ni namna tunavyomchukulia utaendelea kuabudu kisichokuwepo
Mungu ninaye mwabudu mimi sio kichaa nikiamini ni yule yule kwa wakristo na waislam nitakuwa nakufuru kwa kuwa nitamaanisha Kuwa ni Kichaa...
 

Mie hapa nazungumzia kisa cha Malaika mnayesema alimuasi Mungu na ndiye shetani. Mie sizungumzi habari za Mungu wa Waislamu na wakristo,hakuna anayesema Mungu anayeabudiwa sasa na wakristo ndiye Mungu wa waislamu,Mungu wenu ana sifa zake ambazo Mungu wa waislamu hana sifa hizo kama Kufa. Mungu wenu anayo sifa hiyo ya kufa lakini mungu wa waislamu hana sifa hiyo kwahiyo haiwezekana wakawa sawa. Yehova hana sifa ya kufa.
 

Taratibu basi mbona una-panic,nimekuuliza unapinga uwepo wa Mungu au hukubalian na namna binadamu wanavyomuabudu Mungu?jibu ili twende sawa
 

Critical thinker sijui uelewa wako ni mkubwa zaidi au vipi.. sijui. Ila hakuna aliesema wala kumanisha Mungu wa wakirito na waislamu ni huyo huyo.

Niliona kaelement ka maandishi ya kike kwa post yako iliyopita huko nyuma. ulikataa but now umerudia kukoti post huku content yako ikiwa na mawazo ya kike kike. Utamlazimishaje mtu kitu asichosema? Kwanza ulidai nimesema ukiristo na uislamu umetofautiana kidogo tu.

Mkuu jaribu kuwa mkweli, usichangie kwa jazba, usione watu hawanaakili. usijifanye mlokolole huku ukiongea uongo hadharani. ukiona post, isome, ielewe, ikiwa hujaelewa uliza. jambo ulilojifanya kunieka sawa hapo linanipa mashaka ikiwa ulisoma mada na kuilewa, zaidi jambo hilo nimeligusia point no 1.

Ngoja nikuache.
 

Mi tarabu siwezi bhana. Ahsante kwa michango yako mardadi. Bwana awe nawe.
 
Taratibu basi mbona una-panic,nimekuuliza unapinga uwepo wa Mungu au hukubalian na namna binadamu wanavyomuabudu Mungu?jibu ili twende sawa

Vyote.
 
Mambo ya Mungu kamwe Hayawezi Kuelezwa na yakaeleweka kwa akili za kawaida sana kama zako au Zangu. Inabidi uwe mtu wa rohoni saana na kuongozwa na Mungu Mwenyewe ktk Jina la Yesu Kristo ndo unaweza kueleza na kueleweka. Kwanza Neno Mungu ni Relative Term so kuwa na miungu wengi siwezi shangaaa, kama wewe unavyo takakutumia kujenga Hoja, ndo maana waislamu Mungu wanao Mwabudu ni yule ambaye aliabudiwa na Mtume SAW. Sisi Wakristo ni yule ambaye Aliabudiwa na Yesu Kristo.
 
ivi "Mungu" alikua na maana gani kuagiza amri(amri ya tatu ktk amri kumi walizopewa wakristo) inayosema "usiabudu miungu mingine bali mimi tu"

je,
anajua kuna mungu wengine, kwa hiyo anaogopa ataachwa na wanadamu aliowaumba?

au, kama kuna Mungu mmoja tu(ambaye ni yeye), je alikua anarefer Mungu gani wengine?

tusaidiane jamani, inawezekana sina uwezo wa kuelewa biblia...
 

Nakushauri Rudi chumbani ujitafakari upya kuhusu imani yako,you are atheist naturally alaf bado unasema unapinga uwepo wa mungu,Kama huamin uwepo wa mungu kwanini uwe concerned na namba binadamu wanavyoabudu kisuchokuwepo?povu lote la,nini kwa kisichopo?
 
Kweli hujielewi wewe kabinti,kama huamini uwepo wa Mungu mambo ya binadam wanavyoabudu kisiichokuwepo yanaakuhusu nini?umekurupuka dogo,nadhani ndo umejua matumizi ya internet majuzi
 
Kweli hujielewi wewe kabinti, kama huamini uwepo wa Mungu mambo ya binadam wanavyoabudu kisiichokuwepo yanaakuhusu nini?umekurupuka dogo,nadhani ndo umejua matumizi ya internet majuzi

Kutokujibu post yako si kwamba sikuiona, basi tu nimeona huna hoja ujachokifanya ni kuniattack! Hope underline umeweka wazi dhamira yako…

Any way ikiwa una hoja kupinga nilichoandika ningependa kuskia.

Nb: Mungu yupo ila si anaeabudiwa na waislamu na wakiristo.
 

Ha ha ha dah kweli mmejipanga wadau, ila ni bora uamini yupo hata usipomkuta haina shida, kuliko kuamini hayupo halafu ukamkute..
 

Ningeshauri tuache kufikiri uwepo au kutokuwepo mungu na kuzidi kupotosha watu. Kila mtu aishi na msimamo alio nao kwani hata wasio na dini yoyote wanaamini mungu yupo.Nakubali yapo makanisa mengi na madhehebu mengi kama ilivyo misikiti mingi na yote inaamini uwepo wa mungu au mtu aliye na mamlaka kuu kwa vimbe vyote miti na mimea. Huo uchunguzi na utafiti wenu muelewe yupo aliewawezesha vinginevyo wote wangeweza. Wote waliofanya tafiti na kuziweka kwenye maandiahi miaka mingi nyuma walishindwaje kugundua njia ya kuwafanya wao wasife.Mbona hamjafanikiwa njia ya kumfanya binadamu asife? na akifa muwe na uwezo wa kumfufua akaishi tena kama alivyofanya Yesu? Hapo ndipo mjue yupo anaetakiwa kuabudiwa na ndie alietuleta duniani na atatuchukua kila mmoja kwa wakqti wake.
 

Mkuu nimependa majibu yako, unajua skeptics wengi wanadhani ukiristo ni dini ya watu wasiowaza, kuamini kila wanachoambiwa kanisani kumbe sio hivyo.

Biblia inasisitiza sana reasoning and faith na sio blind faith kwamba kuamini kila anachosema mchungaji.
Yesu alikua anafundisha kwa mifano kisha anauliza maswali sasa utajibu vipi swali kama hufikirii, ndio maana walipokua wanakosea alikua anawaambia kumbe hamna akili kabisa kisha anawafafanulia.

Hata Mungu anasema come and lets reason together and bring your argument. Sasa utareason nini na mungu kama hutumii akili kufikiri.

Actually christianity encourages people to use their minds. In facts the bible says that God created humans and endorsed them with brains so that they can use it

Christianity teaches people to have a rational faith based on reasoning and knowledge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…