A God can be a mere theory, nothing more

Nimsaidie kidogo, hata kama ataleta hizo jibu.

Kuwa mkristo OR muislam haiwezi kuwa sababu ya kujua makosa yote yaliyomo kwenye msaafu, kwanza kwenye misaafu hakuna errors za kiimani labda errors za kiuandishi na nk.

Ndiyo maana kila MTU (siyo binadamu) huwa anatafuta hizo errors kwenye IMANI isiyomuhusu ili iwe bakora kwa mbwigas.

Nakupa hii hapa, kati ya vitabu vyoote ulivosoma kipi kinarudiwa na mara zote many years throughout badp kinaoneka hakichoshi na kuonekana kama hujawahi kukisoma?

Kumbuma sayansi ime_copy from Bible, also history issues.
bila shaka wewe ni mkrsito hebu nijibu maswali haya.
1. nitajie errors 5 za kisayansi zilizopo kwenye biblia.
2. nitajie errors 5 za kihistoria zilizopo kwenye biblia.
nataka nijue uelewa wako kwanza kabla sijafika mbali.
 
Mkuu wala kurudiwa sio hoja kuna vitabu vingi vya comic na hadithi vinarudiwa hivyo haihalalishi uahalisia wake biblia na quran vina fall kwenye category ya vitabu vy hadith kuna watu wachache manataka kuwafanya charcaters kama god angel na demons ni viumbe halisi hapo ndio shida ilipo.

pamoja na hayo kuna erros nyingi sana kwenye biblia na quran just google it ukishindwa nitakuletea mwenyewe.
 

Apo xaxa yesu mweupe maraika weupe....asa inamana enzi izo yesu alipo shuka duniani ina maana wa africa hawakuwepo.....
 
MBONA HUKUJADILI UCHAWI KAMA UPO AU LA. Unajitahidi kusema Mungu hayupo na kudhirisha wewe ni wa shetani hukujadili kama shetani yupo au la. NAWAOMBA WOTE AMBAO MUNGU WETU AMEKASHIFIWA NA KUVUNJIWA HESHMA TUMUOMBE AMSHUHULIKIE HUYU MJUMBE WA KUZIMU MPAKA AJUE NGUVU ZA MUNGU.
 
Mungu hachunguziki. Mungu ni Roho, basi yakupasa uingie rohoni "kuokoka" kwa kumuamini Yesu Kristo kuwa ni BWANA.
 
Yeyote aliye kinyume na Mungu aliye hai muumba wa mbingu na nchi, vinavyoonekana na visivyonekana huyo ni wa shetani.
 
4. Kwamba mitume na manabii wote wametoka FAR EAST. kwamba around north Africa and western Asia. no more. (Ikiwa unaushahidi hata wa maandiko tu kupitia vitabu vitakatifu unaoonesha uwepo wa mitume apart from far east ningependa unitoe haya matongo)

Jee Mungu hakutaka kuabudiwa na watu kutoka Southern Africans? China? Korea? Northern Europe? North and Southern America? Australia?


Kwa jinsi ninavyofahama ramani, China, Korea, Japan nk ndio zinaitwa Far East. Sasa sijui ulikua unamaanisha Middle East?
 
Hipo hv kijana nimeeleza hapo awali false ethics zako zinatoka wapi ila nagundua ukipata elimu mujarabu utabadirisha muelekeo huo mbaya.

Ufunuo 12:7 -soma

Alafu nimependa utambulisho wa hao jamaa uliowataja hapo kwenye yellow colored yaweza kuwa sawa maana me siwajui hao hata kwa niaba ya mwenye kuAMINI yeyote. Kumbuka kuna God na god pia Angel na angel.

Jambo la mwisho la kutaka ni_Google nimekwambia awali so take care again, si kila kitu ni ku_Google kijana. zinatoka
 
Apo xaxa yesu mweupe maraika weupe....asa inamana enzi izo yesu alipo shuka duniani ina maana wa africa hawakuwepo.....


Umeona ee, WAKATI YESU ni agano jipya kwanini wasitupendelee waseme Yesu ni mwafrika. hawa watu hawa!!! mmh!!
 

Kabla ya kuja na hizi empty threats ungemuomba huyo mungu kuyaondoa maovu yote aliyoyaumba, ungemuomba aaache wivu, aache visasi kwa vizazi visivyo na hatia, aache upendeleo, amuangamize shetani ambaye ni uumbaji wake na aache kuwa a controlling freak, he/she/it certainly can't control me
 
bila shaka wewe ni mkrsito hebu nijibu maswali haya.

1. nitajie errors 5 za kisayansi zilizopo kwenye biblia.
2. nitajie errors 5 za kihistoria zilizopo kwenye biblia.

nataka nijue uelewa wako kwanza kabla sijafika mbali.

1.Unadhihirisha ulivyo mvivu kutafakari. Nani kakudanganya kuwa Biblia ni kitabu cha kurejea habari za kisayansi ?
2. Bado biblia sio kitabu cha historia kiasi unataka nianze kuangalia makosa ya kihistoria.
Kajipange lete maswali yeye mashiko
 
Very interesting!

Ninaelewa kuhusu issue ya cheo na jina, let say watu 10 wanapotamka Mungu huwa wanahisi wametamka kitu kimoja lakini mara nyingine wanaweza wakawa wanamaanisha kitu tofauti kulingana na madhehebu ama mifumo ya dini waliyomo.

Challenge ya kusema Mungu hayupo, regardless of what God we are talking about ni kwamba tayari kwenye akili zetu tummefundishwa ama kuamini kuwa mungu ni mamlaka kuu, ndiye muumbaji, ana nguvu na uweza wote. Kwa baadhi ya watu kule kujadili tu uwepo wa mungu ni kukufuru, hapa tunajadili kutokuwepo kwake ama katika nadharia au katika proof, hii pekee ni hatua kubwa sana.

Kwenye kusoma imani za wengine, i am very open to new ideas, knowledge and information. Nimesoma sana dini na madhehebu karibu yote yaliyopo duniani, si katika uwepo wa mungu tu bali hata kwa nini wanaamini vile wanavyoamini. Nitakutumia kitabu kinaitwa Faith Perspective in World religions.
Hata kwa wenye dini ambao wanaamini uwepo wa Mungu bado kuna mambo mengine ambayo ni myths wanapoyaonma kwenye dini nyingine.

Kwa mfano katika bandiko hili mtoa mada anasema ana mashaka na uwepo wa mungu kwa sababu kadhaa, napenda kugusia hii moja

1. kama mungu ana uwezo mbona anaacha watu wateseke; hii ni hoja nyepesi kwa sababu kwa dini nilizosoma zote zina majibu juu ya hili. Japo majibu ya dini zote yapo tofauti lakini hiyo pekee haiwezi kutosha kuhafifisha uwepo wa mungu.

Kadiri siku zinavyokwenda napata hisia kwamba kila dini ama dhehebu lina namna yake ya kuji-defend kama dhehebu bora ama la kweli kwa kutumia maandiko yake lenyewe.

Jambo lingine ni kwamba kuna mengi ambayo mwanadamu hawezi kuyaeleza kwa sababu yapo 'beyond explanation'' ambayo hutumika na watu wenye dini zinazoamini uwepo wa mungu kama ushahidi wa uwepo wake.
Asante kwa mjadala bora kabisa Mashaxizo!



QUOTE=Mashaxizo;12697073]Yah! Got you well jerry, i see how you are reasoning!

Umesema god ni cheo na sio jina, you can be right by your reasoning, but ukumbuke hata cheo ni sifa but sifa inaweza kuwa noun too. hope hapo ni issue ya lugha so let us skip on that.

Hapo underline. always tunaproof existence, we cant proof non existence in a sense that you cant find a thing which doesnt exist, he who allege the existence of something the burden to proof lies to him.

Also it seems umestic na imani ulionayo bila kujiuliza maswali ambayo unasema ni mpaka uwe neutral kitu ambachohisi si kizuri. But ukumbuke kuwa neutral sometimes ni bora coz hapo utakua free kuchanganua na kugain new knowledge.

Sometimes ni bora hata kusoma na imani za wengine ili kufanya critical analysis ukihusisha na imani yako. Ni mbaya sana mkuu jerry kufunga kichwa chako kutoruhusu other knowledge kuingia kichwani kwako IKIWA UKO INTERESTED KUUTAFUTA UKWELI.[/QUOTE]
 
Basi inaonekana huamini kuwepo kwa Mungu wala shetani. Basi wewe unaamini umetoka wapi?

Process iliyotumika kupatikana mimi ndio hiyo hiyo iliyotumika kupatikana wewe. Wazazi wasinge gegedana na kutupia sperms kwenye ua, nisingepatikana hata iweje. Mkuu hilo liko wazi whether you know and accept it or not.

Mimi najiamini mwenyewe, najua nikifanya kazi na kujituma everything will be alright.
 
Tuanze na namba moja, ningependa nipate ufafanuzi zaidi.

Ok. no. 1 nimejiridhisha kwamba imani za kuamini Mungu ziko nyingi na zinatofautiana ktk sifa za Mungu huyo pia zinatoa mafunzo tofauti, but licha ya uwingi huo, kila imani inajiona ikosahihi kuliko imani nyengine. Sasa jee inawezekanaje imani hizo zote ziwe sahihi?

Njoo kwenye madhehebu, ukiristo unamadhebu yasiyopungua 50 world wide but kila dhehebu linajiona liko sahihi kuliko jengine, ikiwa unasoma historia utagungua kuna vita zilipiganwa ambavyo ni dhehebu moja dhidi ya jengine Hata ujerumani walishapigana hii vita.

Ktk uislamu kuna madhehebu zaidi ya 7, na kila dhehebu linajiona liko sahihi hadi kupigana vita. kumbuka Irani Shia v. Sunni. Suni wanawaona mashia makafiri na kinyume chake ni hivyo hivyo ukizingatia hao wote wanaini na kufuata Quran.

Sasa basi hapo nikadraw conclusive and unconlusive ruling kwamba;

Conclusive: Haiwezekani imani zote dhidi ya Mungu ziwe sahihi. Jee unapinga hapa?
Unconclusive: But KUNAUWEZEKANO hao wote ni waongo.

Yupi ni mkweli na yupi ni muongo inategemea na hoja nyengine 8 zilizobaki ili kudraw conclusive rule.
 

Uko sahihi. mimi nimekosea.
 
jerrytz nakusoma vizuri.

Unasoma idea ya God inaweza kutafriwa ktk mitindo tofauti kwa kuzingatia imani tofauti hapo tuko pamoja, coz hata mimi naami 'GOD' ni abstract idea. Kwa mantik hiyo hata mimi naweza kusema Mungu yupo kwa kigezo cha 'Super natural power' hope hilo liko wazi na ndio sababu ktk kichwa cha habari sijaeleza moja kwa moja kwamba God hayupo "A God can be a mere theory"

Mungu wa wakirosto na waislamu (hata traditional gods) ndie ninaemkataa kutokama na sababu tisa nilizoorodhesha kwa thread.

There can be a God in sense of Super natural power ambaye naweza kusema kwamba hana mahusiano yoyote na imani tajwa hapo juu.

What do you think jerry?

(Naomba unipatie hiko kitabu.)
 
Last edited by a moderator:

Ujue kuna imani na kuna dini,wapo wenye kuamini kuwepo kwa mungu ila hawaamini dini,sasa ukiwaweka wote hao kwn kundi moja halafu ndiyo uulize kwanini wanatofautiana utakuwa haujatenda haki...hebu weka sawa kwanza jambo hilo.
 
Kwa wengi Mungu ni wa kufikirika zaidi ili tu wakidhi haja ya kuona wapo chini ya mamlaka fulani.

Dini nyingi ni matokeo ya wachache kupanga mfumo wa dini kwa maslahi yao. Uwepo wa Mungu kwa upande wangu unaweza usiwe kwa namna ambavyo dini zinafasiri kwa kuzingatia tendency ya wanadamu kuweka mambo na kuyapanga kwa maslai yao.

Sababu zako tisa zinaweza kuwa za kufikirisha ila hazijibu wala dhana ya kutokuwepo kwa Mungu.

Unaweza kuwa na wazazi na wakakuacha bila msaada je hiyo ni proof kuwa hauna wazazi?

Kikubwa ninachoona hapa ni kuwa tunataka Mungu ajifunue kwetu kwa namna tunayotaka, vitabu vya kiroho vimetueleza mengi kuhusu Mungu lakini walimu wa kiroho wamemweka Mungu mbali zaidi na waumini kwa kuwa wao wamekaa kati ya Mungu na wanadamu.

Wengi wameona sauti za viongozi wa dini kuwa sauti ya Mungu, tazama dini zote zenye ''extremists'' , watu wameshawishiwa kufuata misimamo ya watu kwa kigezo cha ''thus said the Lord'', or ''that's what Allah commands''

All in all, tunachokosa wanadamu ni tafsiri sahihi ya Mungu na madhumuni ya kutuumba katika mtazamo wa maisha tunayoishi.

Wengi wanatamani Mungu awafanye wawe vile wanavyotaka kuwa. Ni sawa tu na girlfriend wako kupima upendo wako kwa kumnunulia gari,usimpomnunulia gari basi conclusion ni kuwa humpendi!!!

My conviction is; the existence of God is far beyond mere theory,myth or speculation.



Tuendeleeeeee


 
Last edited by a moderator:
Ujue kuna imani na kuna dini,wapo wenye kuamini kuwepo kwa mungu ila hawaamini dini,sasa ukiwaweka wote hao kwn kundi moja halafu ndiyo uulize kwanini wanatofautiana utakuwa haujatenda haki...hebu weka sawa kwanza jambo hilo.

Yah ni kweli ulivyosema.

I mean dini na madhehebu yake.
 
Kwa wengi Mungu ni wa kufikirika zaidi ili tu wakidhi haja ya kuona wapo chini ya mamlaka fulani.

Hahahaaaaa! Kweli tupu!
Dini nyingi ni matokeo ya wachache kupanga mfumo wa dini kwa maslahi yao. Uwepo wa Mungu kwa upande wangu unaweza usiwe kwa namna ambavyo dini zinafasiri kwa kuzingatia tendency ya wanadamu kuweka mambo na kuyapanga kwa maslai yao.
Nilianza kuwa na mawazo hayo kabla ya kuhitimisha kukataa uislamu na ukiristo. hapo unakubali wewe na hata mimi but ukimueleza shekhe au padri maneno hayo anaweza kukuesabu umekengeuka maandiko.
Sababu zako tisa zinaweza kuwa za kufikirisha ila hazijibu wala dhana ya kutokuwepo kwa Mungu.
Yah, na hiyo itatokana na ile dhana ya Mungu kwamba ni abstract theory inayotafsiriwa kulingana na imani fulani rather than reality how God is and whats really want us to do for the sake of him.

Always idea come first.
Unaweza kuwa na wazazi na wakakuacha bila msaada je hiyo ni proof kuwa hauna wazazi?
Hiyo haiwezi kumanisha huna wazazi but ukumbuke wazazi ni binadamu ambao ni wadhaifu wakati Mungu ni the perfect one ambae hawezi kuwa na huo udhaifu. hope you see the logic.
Kikubwa ninachoona hapa ni kuwa tunataka Mungu ajifunue kwetu kwa namna tunayotaka, vitabu vya kiroho vimetueleza mengi kuhusu Mungu lakini walimu wa kiroho wamemweka Mungu mbali zaidi na waumini kwa kuwa wao wamekaa kati ya Mungu na wanadamu.
Si umeona hapo mkuu? Nimeonaijadala mengi ya kidini hapa kati ya wakiristo na waislamu, unakuta muislamu anauponda ukiristo kwa matendo ya mapadre kwa mfano padre akilazimisha watu kutoa sadaka, Sometimes padre wakitia mimba kondoo wao nk. na pia wakiristo wakiponda uislamu kwa vitendo vya mashekhe kufanya uzinifu, kubaka, matendo ya alshabab, boko haram nk.

Always sipendi kujadili or hata kutoa maanani dini fulani kwa vitendo vya waumini wake. siku zote naangalia jee vitendo hivyo ndio mafundisho hasa au ni utashi tu.

Hapo nakua nabase zaidi kwenye maandiko thus why hata mada haina hoja inayolenga matendo mabovu ya waumini, njia mzuri ya kujadili kitu ni kuangalia theory kukiwa na ulazima basi ni kuangalia events.

Mkuu hapo nimeelezea sana, nikiwa na maana ya kwamba nazikataa hizo dini kupitia maelezo na mafunzo yake kupitia vitahu vitakatifu ambavyo vimecontain, ukweli, uongo and many unreasonable teachings. kwangu mimi, Mungu hawezi kuongea uongo na pia hawezi kutoa mafunzo ambayo ni unreasonable. Na akifanya hivyo huyo si Mungu au vitabu vielezee kabisa kwamba hata Mungu hawezi kufikiri sawa sawa na sio kumpa kila sifa mzuri wakati anatudanganya na kutupotosha.
Wengi wameona sauti za viongozi wa dini kuwa sauti ya Mungu, tazama dini zote zenye ''extremists'' , watu wameshawishiwa kufuata misimamo ya watu kwa kigezo cha ''thus said the Lord'', or ''that's what Allah commands''

Na hapo ndipo niliposema kwamba anaweza kuwepo but sie huyu anaeongelewa na Muslims and Christians.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…