Kwa nini kuna kitu chochote kilichopo na kinachoonekana? Sayansi imethibitisha kuwa vitu vyote tunavyoona vimewekwa hapo kwa nguvu msingi kuu nne;
- Strong force - Nguvu kubwa - Hii wakati mwingine huitwa nguvu ya kiini (Nuclear Force) na husababisha uwepo wa viini vya tonoradi (Atomic Nucleus)
- Electroweak forces - Nguvu dhaifu sana
- Electromagnetic forces - Nguvu ya umemesumaku
- Nguvu ya uvutano - Gravitation force
Sayansi bado inatafuta nguvu kuu inayounganisha nguvu hizo katika mifumo tofauti tofauti na kusababisha uwepo wa chochote kilichopo; kinachoonekana kwa macho na kisichoweza kuonekana kwa macho. Nguvu hiyo inatafutwa katika kipande kinachoitwa "Higgs Boson" inayosababisha "Higgs Field" ambayo ndo inaelezea uwepo wa tungamo (Mass). Vitu vyote vyenye tungamo (Mass) ndo tunavyoviita ulimwengu - Sayari, Nyota, Galaksia na Makundi ya Galaksia. Tonoradi ni sehemu ndogo sana ya sayari na tonoradi huweza kuvunjwa vunjwa na hatimaye unagundua kuwa tonoradi huundwa na nguvu tatu nilizozitaja hapo mwanzo (isipokuwa tu Nguvu ya uvutano). Bado sayansi inatafuta ni katika kiwango gani vipande vya chini kabisa vya tonoradi yaani kwaks zinapopata tungamo, kwani hapo ndo nguvu hubadirika na kuwa vitu. Uhusiano huu ukiweza kuelezeka; msingi wa uwepo wa vitu vyote vilivyopo utakuwa umepatikana. Uhai tunaoujua ni sehemu ya sayari (planets) kwa maana kuwa uhai huzuka katika sayari yoyote yenye mazingira wezeshi. Je huhai huzuka tu? Wengine wanasema uhai umeanzia kwa mungu na husema kuwa uwepo wa vitu vyote unawezeshwa na nguvu ya uumbaji - Mungu. Kwa kuwa utaalam wa utambuzi na ung'amuzi wa mazingira na vilivyomo na mahusiano yake; yaani sayansi haijaweza kuunganisha au kutoa majibu ya maswali yote - wengi bado wanaamini katika maarifa ya "kiroho" na maelezo yanayotolewa "kiroho".
Swali la mleta mada ikiwa Mungu yupo au hayupo, ni swala la kifalsafa. Kwa sasa hakuna jibu moja; kutegemea aina ya maarifa aliyonayo mtu kiroho. Hata hivyo, njia za kisayansi hazijaweza kuthibitisha uwepo au kutokuwepo kwa Mungu na wengi wanajiuliza ikiwa sayansi inao uwezo wa kutoa majibu. Njia za kisayansi ni njia bora zaidi za kujifunza maarifa yasiyojulikana bado. Kwa kuwa sayansi haijaweza kutupa majibu, tunachukulia majibu yaliyopo kuwa ni majibu sahihi mpaka hapo maarifa mapya yatakapopatikana.
Majibu yaliyopo leo yanasema Mungu huweza kujulikana tu kwa yeye mwenyewe kujidhihirisha vinginevyo mwanadamu hawezi kutambua (au kung'amua) uwepo wa Mungu. Maelezo ya kiroho hutuambia kuwa Mungu asipojidhihirisha kwako kamwe huwezi kumtambua (Au kung'amua uwepo wake). Katika biblia, kitabu cha Mwinjili Mathayo Yesu aliwauliza wanafunzi wake "watu husema mimi ni nani?" wanafunzi wake walitoa majibu mengi, hatimaye akawauliza nanyi mwaniita nani? Simulizi hili la Mathayo linatuambia kuwa Petro alimjibu yesu jibu sahihi - Yesu akamwambia jibu hilo lazima ameambiwa na nguvu kubwa zaidi kwani mwili na damu haviwezi kutambua hivyo. Kwa hiyo wakristo wanaomwamini Mungu kupitia kwa Yesu Kristo huamini kuwa hatuwezi kumtambua Mungu hadi yeye Mwenyewe ajidhihirishe kwetu - hapo huwa hatujiulizi tena.
Kwa hiyo, kwa kuwa muanzisha mada Mungu hajajidhihirisha kwako, ni vigumu sana kuwa utamjua au kung'amua uwepo wake. Siku akijidhihirisha kwako ama kwa hakika utamjua na hutahitaji kuuliza maswali. Kwa sasa unachoweza kufanya ni kuishi kama mwelekeo wa mawazo au fikra zinavyokutuma - ili mradi huvunji sheria za nchi.