A God can be a mere theory, nothing more

A God can be a mere theory, nothing more

vitu vingi umeongea ukweli lakn wabongo kwa imani zao huwez kuwashawishi, hizi dini mbili ni mawazo yaliibuka hapo middle east watu waka copy na kupest na kutuletea huku. yaani mungu ambaye anaona dunia yoote awe na uvivu wa kupeleka imani mwenyewe brazil,afrika,china hadi watu waje wamsaidie tena wengine through vita?????

Hata baba yako na mama yako walianza maisha wawili,lakini leo mpo kikundi.na mnatawanyika.
Afu Dini haijaanzia middle east!
Jifunze nini maana ya Dini.Dini ilianza taratibu mpaka ikatimia!
 
Dhana ya uwepo wa Mungu haihusishi jinsi wanadamu wanavyoabudu,bali inajumuisha makundi yote yenye uhai.
Tunaweza kusema sisi kama binadamu kuwa hakuna Mungu lakini viumbe hai kama miti na wadudu wakathibitisha uwepo wa Mungu pasipo shaka yeyote.
Uwepo au kutokuwepo kwa Mungu uanza na huishia pale kundi moja linapobadilika kwenda kundi jingine la uhai.
Hivyo ili tuweze kuelezea dhana hii ni lazima tuangalie namna gani makundi ya vitu vyenye uhai vinavyoishi na kupotea kuliko namna gani dini zinavyotumika na kundi moja tu hususa sisi wanadamu.
Mimi kama binadamu ninaamini kuwa chochote kile kilicho na uhai na kisicho kilichoumbwa na Mungu kinatimiriza uwepo wake na ili kitokee ni lazima kitu hicho kitoke kwenye hali moja kwenda kwenye nyingine (mfumo mmoja wa uhai kwenda mfumo mwingine).
Pia naamini kuwa kifo ndilo fumbo kubwa linalowasumbua wanadamu na yamkini ndicho kitu wanakiogopa kuliko hata yule aliyewaumba.

Pamoja
 
Dah! mkuu umenikumbusha mbali kiasi cha kung'amua kwanini madrasa watoto wanachapwa sana. kiukweli kuchapwa kwa watoto madrasa ni kuwapandikiza uoga usio na sababu za msingi. ni tamaduni ya waarabu walipokuja kutufanya watumwa nothing more, madrasa ukichapwa sana na kulalamika unaambiwa hiyo ni heri yako coz makovu utakayoyapata ndio taa yako ukiwa kaburini. ni ujinga wa hali juu kabisa.

Ushahidi tafadhali wa maneno yako hata!
 
Mkuu Shetani ni nani? ni kiumbe? Embu nipe maana ya shetani ili nikujibu, may be im one of them according to your perspective.

Shetani ni yule anayeongoza watu katika kumpinga mungu,hata wewe unaongozwa na roho ya shetani.
 
Mkuu FATHER OF REALITY unatoa maelezo mengi sana yenye michanganyiko ya hoja tofauti. hii inapelekea ugumu wa kujadili ukizingatia kila point inaweza kuibua maswali.

Ningependa hata ukitoa maelezo mengi basi iwe ni kwa point moja ili tuweze kumaliza issue kwa haraka na ile hali ya kujirudia isitokee.
Labda tuanze na issue ya Mungu huyu wa vitabu. Kwanini vitabu vinaerror nyingi sana? Na kwanini waumini wa kitabu hicho wanatumia siasa ili ionekane kitabu chao kiko sahihi na kumaanisha Mungu hakuwa na maana kama inavyosomeka kwenye kitabu hicho? Basic ya swali langu ni kwamba kwenye ukiristo ni hivyo hivyo na uislamu ni hivyo hivyo? Itawezekana vipi hao wawili wote wawe sahihi?


Mkuu nimeheshimu, ushauri wa kuwa natoa maelezo mengi mno, ni kweli, lakini mkuu nitendee haki, muanzilishi wa mada alitoa maelezo mengi kisha akauliza maswali mengi zaidi yenye nature tofauti.

ni kweli, vitabu vina mikanganyiko ukivilinganisha, na hii ni kutokana na kuingiliwa na tamaduni mbalimbali, kaika kumtumikia Mungu, yeyoyote, aweza kuwa sahihi mahali popote, ilimradi dini hiyo haipingani na dhamiri njema.

maana yabgu ni kwamba baya ni baya tuu, na haliteteki, kipimo kitatoka katika uasili wa matendo, yaani jamiii hii hii uishiyo kuna mabo wote kwa namna tofauit wanasema ni mabaya na mengine wanasema mazuri. Cha msingi ni kwamba tuelewe kuna Mungu, mkuu wa mambo mema, na Shetani mkuu wa mambo mabaya.

Hiyo mikanganyiko katika dini haiondoi uwepo wa Mungu, kama mtawala mwenye nia njema.
 
Ahahahhahaaha taratiiibu unaanza kuamini kuwa Mungu yupo, thats very good beginning.

Hahahaaaa! Kijana Niliamini hiyo kitambo Mungu wenu wa vitabu. Supernatural power ikiwa ni Mungu basi namuamini huyo. Labda tu unisaidie ikiwa supernatural power ina dini na inaandika kitabu. then uniambie hiko kitabu chenyewe ni kipi.
 
Process iliyotumika kupatikana mimi ndio hiyo hiyo iliyotumika kupatikana wewe. Wazazi wasinge gegedana na kutupia sperms kwenye ua, nisingepatikana hata iweje. Mkuu hilo liko wazi whether you know and accept it or not.

Mimi najiamini mwenyewe, najua nikifanya kazi na kujituma everything will be alright.

Ushayakana mengi kwa kauli hii.
Si umesema una paneal grands.geuza jiwe mkate.

Kwanini mpaka ufanye kazi na ujitume.mbona hayo ni maamrisho ya Dini ya mungu?
Asiye Fanya kazi na asile.

We si umesoma?

Wapi pameabdikwa kila mtu alipatikana kwa kujamiina?
Thibitisha kama wazazi wako walijamiiana ukapatikana wewe.

Adam alipatikana kwa kugegedana nani na nani?

Hawa/Eva alipatikana kwa kugegedana nani na nani?

Yesu/issa alipatikana kwa kugegedana nani na nani?

Pia kama unaamini evolution theory ya uongo ya Charles d.

Masokwe yalipogeuka binadamu yaligegedana na nani?

Unachokiamini wewe ndio uongo.hujijui tu!
Umelewa somo la kishetani(philosophy)
 
unaogopa kujibu hilo swali kwani unajua fika kuwa hapo ndipo utumwa ulipoanzia,physical and mental slavery ambayo mmeachiwa mpaka leo.

Unaona sasa tatizo hilo?

Sasa ikiwa hapa afrika uwepo wa dini ni utumwa je,vp huko mahali pengine maana dini zipo kila mahali? Na ni aina gani hiyo ya utumwa unayomaanisha?
 
Mkuu nimeheshimu, ushauri wa kuwa natoa maelezo mengi mno, ni kweli, lakini mkuu nitendee haki, muanzilishi wa mada alitoa maelezo mengi kisha akauliza maswali mengi zaidi yenye nature tofauti.

ni kweli, vitabu vina mikanganyiko ukivilinganisha, na hii ni kutokana na kuingiliwa na tamaduni mbalimbali, kaika kumtumikia Mungu, yeyoyote, aweza kuwa sahihi mahali popote, ilimradi dini hiyo haipingani na dhamiri njema.

maana yabgu ni kwamba baya ni baya tuu, na haliteteki, kipimo kitatoka katika uasili wa matendo, yaani jamiii hii hii uishiyo kuna mabo wote kwa namna tofauit wanasema ni mabaya na mengine wanasema mazuri. Cha msingi ni kwamba tuelewe kuna Mungu, mkuu wa mambo mema, na Shetani mkuu wa mambo mabaya.

Hiyo mikanganyiko katika dini haiondoi uwepo wa Mungu, kama mtawala mwenye nia njema.

Mkuu ni mimi niliweka mada ila sikuweka kama unavyoiona sasa. ni mods ndio wameicompile, infact sio jambo baya. hata mimi nimependa. ila nimeweka bayana kupitia mada hiyo kwamba mtu achague kipengele anachoona hakiko sahihi kwa mtazamo wake ili tujadili.

Anyway. vitabu kujieleza kuwa vinatoka kwa Mungu, tena Mungu wa kweli na mkamilifu then tukaona mushkeli hapo lazima tuulize ukamilifu wa Mungu huyo ni upi.

Then mkuu umegusia suala la shetani hapo. Jee shetani ni kiumbe or ni theory?
 
Unabadiri hoja kwa kuingiza habari ya ibada ya sanamu. Nimekwambia Allah waliyekuwa wanamwabudu Makuraish aliwekewa wasaidizi zaidi ya 360 naabinti watatu. Hakukuwa na sanamu ya Allah Bali wasaidizi.
Wewe ndiwe eleza alikuwa anawalinfania nini ?

Hehe we jama ni pasua kichwa...haya huyo Allah ambaye alikuwa anaabudiwa na Makuraish alikuwa na sifa zipi?
 
Kwa wengi Mungu ni wa kufikirika zaidi ili tu wakidhi haja ya kuona wapo chini ya mamlaka fulani.

Dini nyingi ni matokeo ya wachache kupanga mfumo wa dini kwa maslahi yao. Uwepo wa Mungu kwa upande wangu unaweza usiwe kwa namna ambavyo dini zinafasiri kwa kuzingatia tendency ya wanadamu kuweka mambo na kuyapanga kwa maslai yao.

Sababu zako tisa zinaweza kuwa za kufikirisha ila hazijibu wala dhana ya kutokuwepo kwa Mungu.

Unaweza kuwa na wazazi na wakakuacha bila msaada je hiyo ni proof kuwa hauna wazazi?

Kikubwa ninachoona hapa ni kuwa tunataka Mungu ajifunue kwetu kwa namna tunayotaka, vitabu vya kiroho vimetueleza mengi kuhusu Mungu lakini walimu wa kiroho wamemweka Mungu mbali zaidi na waumini kwa kuwa wao wamekaa kati ya Mungu na wanadamu.

Wengi wameona sauti za viongozi wa dini kuwa sauti ya Mungu, tazama dini zote zenye ''extremists'' , watu wameshawishiwa kufuata misimamo ya watu kwa kigezo cha ''thus said the Lord'', or ''that's what Allah commands''

All in all, tunachokosa wanadamu ni tafsiri sahihi ya Mungu na madhumuni ya kutuumba katika mtazamo wa maisha tunayoishi.

Wengi wanatamani Mungu awafanye wawe vile wanavyotaka kuwa. Ni sawa tu na girlfriend wako kupima upendo wako kwa kumnunulia gari,usimpomnunulia gari basi conclusion ni kuwa humpendi!!!

My conviction is; the existence of God is far beyond mere theory,myth or speculation.



Tuendeleeeeee

Mafundisho yapi ya Dini yapo kimaslahi?

Kutumia mwiko kumpigia mtu haimaanishi kazi ya mwiko ni kupigia.kazi ya mwiko iko wazi.
Ila unakuwa umemisuse.
 
Habari za hapa.

Nimefanya research juu ya ukweli wa dini na uwepo wa Mungu hasa Mungu anaeongelewa na wakiristo na waislamu.

Ktk utafiti huo nimegundua mushkel mwingi SANA kuhusiana na dini hizo na suala la uwepo wa Mungu in general as it preached by Muslims and Christians.

My be I'm wrong thus why nimeweka hoja hapa ili mwenye uelewa anieleweshe na pia aweze kujibu maswali. Lengo langu ni kutambua ukweli na sio kuleta ubishi usio na tija. so nakaribisha maswali na pia nasistiza wale wasio na hoja wajifanye kama hawajauona uzi huu.

HAYA NI MAMBO NILIOYAONA KTK UTAFITI WANGU:

1. Dini ziko nyingi (ni zaidi ya 30 na hapo hujagusia madhehebu!!) but licha ya uwingi huo kila dini inajiona iko sahihi ZAIDI ya nyengine. It cant be all religions are true but there possibility all of them are wrong.

2. Kwa huku Africa dini hizi tumeletewa, walioleta dini walileta ili kututawala. hope hili liko wazi, ie Uislam uliletwa na waarabu ambao walikuja kufanya utumwa na kutuuza sehem tofauti kama bidhaa tu. kiukweli tulipata shida sana. Pia ukiristo uliletwa na wakoloni ambao walikuja kuchukua malighafi na nguvu kazi zetu na kutuacha ktk hali ya utegemezi hadi leo hii.

Jee dini ya kweli inaweza kuletwa na madhalimu?

3. Qur-an and Bible (here and after refers to vitabu vitakatifu) vimecontain ukweli, uongo, many unreasonable teachings and contradictions on its/them. eg: Kwamba dunia ni flat, imetulia na jua ndilo linalotembea kutoka mashariki kwenda magaribi. (hope mnautambua uongo huo but if hujatambua hilo niambie nikuekee ushahidi ili tuende sawa)
Pia dini zinaruhusu mtoto wa kike kuolewa na kuingiliwa hata kama hajavunja ungo!!!! (pia naweza kuthibitisha hilo) na mengi mengineyo. (just put a number and tell me which no. you don't agree)

4. Kwamba mitume na manabii wote wametoka FAR EAST. kwamba around north Africa and western Asia. no more. (Ikiwa unaushahidi hata wa maandiko tu kupitia vitabu vitakatifu unaoonesha uwepo wa mitume apart from far east ningependa unitoe haya matongo)

Jee Mungu hakutaka kuabudiwa na watu kutoka Southern Africans? China? Korea? Northern Europe? North and Southern America? Australia?

5. Vitabu vitakatifu vinatafsiriwa kisiasa zaidi ili kuzibia errors ambazo Mungu aliacha kwenye vitabu hivyo! Eg: Mungu ameweka wazi kwenye vitabu vitakatifu kwamba jua linazama kwenye matope but Muslims wanasaidia majibu kwamba ni Red sea! wanaact kana kwamba Mungu hajui kusema Red sea! unapoulizia kuhusu jua kutembea kutoka mashariki kwenda magharibi na suala la kwamba dunia ni flat hapo unaambiwa Mungu ameielezea dunia kama ambavyo sisi tunaiona!!!

But wakati huo huo tunaambiwa vitabu vitakatifu vinaendana na nyakati!!! kwamba hata mambo ya kisansi yameongelewa mle toka enzi na enzi ambayo practise zake zinatokea sasa! Hapo unaweza kuuliza mbona hizo scientific findings hazikuongelewa kama sisi tunavyoona? Issue inakuja kwamba kwenye bible ni hivyo hivyo na kwenye Quran ni hivyo hivyo wakati hizo dini zinapingana vilivyo hadi kufikia kuitana magaidi na makafiri!!!! (Hapa nnamifano mingi tu na ushahidi just put a number and request me to proof)

6. Dini ya mtu inatokana na namna ya wazazi and/or walezi walivyomlea. hapa ningependa kueka wazi kwamba si kila dini or imani ya mtu ni zao la wazazi but ni wachache sana wanaoamini dini or imani ambayo hawakufunzwa na wazazi wao. kwa makadirio ni asilimia 5 tu ya wanaoamini kinyume na mafundisho ya wazazi wao. na kati ya hao, wengi wamebadili imani kutokana na mapenzi (romantic love) na kipato/pesa. ni wachache sana walioamini dini nyengine kwa kutumia their logic reasoning na findings. Hata wewe unaesoma hapa unaamini hicho unachokiamini kwa sababu tu wazazi and/or walezi wako wametokea imani hiyo, nothing more. and you cant fight against reality.

Jee wazazi/walezi wote wako sahihi na imani wanazowapachika watoto wao?

7. Sifa anazopewa/anazojipa Mungu ni za uongo.

a) Mungu nimuweza wa yote. Kwanini haifanyi dunia kua sehwm salama? Kwanini mauaji? Kwanini unyama? Si anaweza yote? kwanini hazuii? For what? Ivi apa hamuoni ni sawa na mtu anaekwambia anapesa but ukimwambia nioneshe anakwambia nimeziacha nyumbani???

b) Mungu ni mpangaji wa kila kitu.
Nadharia hii jiliipinga wakati naamini na nilitetea kwamba Mungu anajua tu ila hapangi but niliambiwa napingana na maandiko. na kweli nilipewa ushahidi wa wa Maandiko Kwamba Mungu akimpangia mtu kupotoka hakuna wa kumuongoa na aliemuongoa hakuna wa kumpotosha!!!!

So ikiwa amepanga kila kitu kwanini aje aadhibu then?
Jee Mungu anaupendeleo? Sasa kwanini atupungie yeye matendo yetu? kwanini asituache tukaact by our own free will?

c) Mungu ni mkamilifu.
Kwanini anaumba vilema? Matahira? Wamemkosa nini hao? Au ukamilifu wake uko limited kwa baadhi ya vitu tu? Au vilema na matahira wameumbwa na nani?

d) Anapenda watu wote. Kwanini wengine wanahangaika sana? Kwanini wengine wanadhulumiwa sana? ukumbuke yeye ni mueza wa kila kitu.

Then kama anapenda kila mtu kwa nini ameahidi tabu na mashaka kwa vizazi vya Izrael kwa makosa ya mababu zao? Hawa wanaozaliwa sasa wamemkosea nini?

HOW UNREASONABLENESS GOD HE IS?

Sifa za uongo anazonyingi but let me skip and wait somebody who is interested on that point.

8. Ukweli juu ya Astrology. Astrology ni uhusiano wa mizunguko ya sayari na tabia za mtu kwa kuzingatia tarehe na saa aliyozaliwa. Najua hili ni somo geni kwa wengi wetu humu. but not an issue, ili nawe ujue ukweli wa astrology nitaweka link just put your information as it required on the given link so as to comment on this point.

https://alabe.com/freechart/

Hapo utagundua nini kimeinfluence tabia zako. Na kwa mantiki hiyo unapata jibu si kila unavyofanya or ulivyoepangiwa na Mungu also utajua si Mungu pekee anaeijua kesho ikizingatia alishasema hakuna anaeijua kesho. Ningependa kupokea hoja kwa point hii kwa mtu alietoa uvivu na kuingia humo. Narudia tena sipendi ubishi wa kiji.nga.

9. Miujiza na maono waliyokuwa nayo mitume ni uwezo alionao kila mwanadamu.

Inaaminika mitume waliweza kuota ndoto za kweli pia waliweza kutafsiri ndoto za wengine.
Waliweza kutabiri mambo yajayo pia waliweza kuelezea mambo mengi yaliyopita.
Pia waliweza kufanya miujiza tofauti tofauti.

Watu wengi hudhani yale ni Miujiza kutoka kwa Mungu kitu ambacho sio kweli, it just how they succeed to activate their pineal gland. Pineal gland ni part ya ubongo iliopo kati lakini chini ya ubongo wa kila mwanadamu. ingia ata google uone picha. Ukiweza kuactivate pineal gland unafungua nguvu zako za maono na miujiza. pineal gland kwa kishwahili wanaita jicho la tatu.

Ile miujiza sijui maono just ni psychic powers ambazo kila binadamu anazo sema zinatofautiana tu kidogo.

Wakiristo wengi huibiwa pesa zao makanisani kwa nguvu hizi. then ata biblia imegusia ili somo sema tu watu tuwavivu wa kusoma. always tunakarirshwa machache ili wajanja wale vyao bila tabu.

Namna ya kuactivate jicho la tatu ni kumeditate (tahajudi/kusali), hata Yesu inaaminika alikua akisali. wakiristo hawajiulizi huyu Mungu alikua akimsalia nani? Yeye si ni Mungu, si angefanya tu mambo yake bila ya kusali. ukija kwa uislamu tunaambiwa Muhammad alikua akienda milimani kusali kabla ya kupewa utume. tunaambiwa alipofatwa na mfalme najash ili kuthibitisha utume wake alisali kwanza, mifano ni mengi na inaanzia kwa ibrahim.

Point hapa ni kwamba wale waliodevelop vizuri pineal gland zao na kujitangazia utume ndio mitume iliyoorodheshwa kwenye vitabu. pia ikumbukwe ilifikia uwepo wa mitume miwili kwa wakati mmoja na ilitokea mtoto alikua mtume, baba yake alikua mtume, babu yake alikua mtume na yeye mwenyewe akazaa mtume. hiyo iko kwenye biblia na quran too. (anaepinga naweka ushahidi)

Nisiwachoshe sana. hivyo ndivyo nilivyogungua kwenye reseach yangu.
Yoyote mwenye kupinga naskiliza hoja yake.
'....religion is opium of society...' Karl Marx. so it is not a theoru but ganja. Jinsi wanadamu wanavyozidi kuelewa na kuweza kuyatawala mazingira yao ulimwenguni dini zitakwenda likizo na hatimae kustaafu.
 
Hahahaaaaa! Kweli tupu!

Nilianza kuwa na mawazo hayo kabla ya kuhitimisha kukataa uislamu na ukiristo. hapo unakubali wewe na hata mimi but ukimueleza shekhe au padri maneno hayo anaweza kukuesabu umekengeuka maandiko.

Yah, na hiyo itatokana na ile dhana ya Mungu kwamba ni abstract theory inayotafsiriwa kulingana na imani fulani rather than reality how God is and whats really want us to do for the sake of him.

Always idea come first.

Hiyo haiwezi kumanisha huna wazazi but ukumbuke wazazi ni binadamu ambao ni wadhaifu wakati Mungu ni the perfect one ambae hawezi kuwa na huo udhaifu. hope you see the logic.

Si umeona hapo mkuu? Nimeonaijadala mengi ya kidini hapa kati ya wakiristo na waislamu, unakuta muislamu anauponda ukiristo kwa matendo ya mapadre kwa mfano padre akilazimisha watu kutoa sadaka, Sometimes padre wakitia mimba kondoo wao nk. na pia wakiristo wakiponda uislamu kwa vitendo vya mashekhe kufanya uzinifu, kubaka, matendo ya alshabab, boko haram nk.

Always sipendi kujadili or hata kutoa maanani dini fulani kwa vitendo vya waumini wake. siku zote naangalia jee vitendo hivyo ndio mafundisho hasa au ni utashi tu.

Hapo nakua nabase zaidi kwenye maandiko thus why hata mada haina hoja inayolenga matendo mabovu ya waumini, njia mzuri ya kujadili kitu ni kuangalia theory kukiwa na ulazima basi ni kuangalia events.

Mkuu hapo nimeelezea sana, nikiwa na maana ya kwamba nazikataa hizo dini kupitia maelezo na mafunzo yake kupitia vitahu vitakatifu ambavyo vimecontain, ukweli, uongo and many unreasonable teachings. kwangu mimi, Mungu hawezi kuongea uongo na pia hawezi kutoa mafunzo ambayo ni unreasonable. Na akifanya hivyo huyo si Mungu au vitabu vielezee kabisa kwamba hata Mungu hawezi kufikiri sawa sawa na sio kumpa kila sifa mzuri wakati anatudanganya na kutupotosha.


Na hapo ndipo niliposema kwamba anaweza kuwepo but sie huyu anaeongelewa na Muslims and Christians.

Kumbe unakubali kuwa mungu yupo,sema humuoni.Na hiyo ndiyo imani.
 
Kipengele cha 7 c
vilema viwete ni matokeo ya dambi zetu

Mkuu dhambi za wazee wanabebeshwaje watoto? Si mnasema watoto ni malaika wa Mungu wasio na hatia. Ivi wewe ukigombana na jirani yako utakwenda kumkata mkono mtoto wake?
 
Duh. basi kweli Allah ni Mungu. Ok nijibu yale maswali yangu sasa.

Hatukuwa tukijadili kwamba Allah ni Mungu ama siyo Mungu,tulikuwa tukijadili suala la kwamba Qur'an ni maneno ya Mungu kupitia kwa Mtume muhammad.
 
Kumbe unakubali kuwa mungu yupo,sema humuoni.Na hiyo ndiyo imani.

Imani kukubali uwepo wa kitu bila ithibati.
Super natural power imeshakuwa proved na Science. Huyo Mungu wenu wa vitabu ndie asiethibitishwa mpaka leo hii.
 
Hatukuwa tukijadili kwamba Allah ni Mungu ama siyo Mungu,tulikuwa tukijadili suala la kwamba Qur'an ni maneno ya Mungu kupitia kwa Mtume muhammad.

Aya Mkuu. naomba unijibu yale maswali.
 
Back
Top Bottom