Maisha yanakwenda kwa kasi mno mengi ambayo tunaona hayawezekani au hayapo wenzetu huko wanakesha kutuonyesha jinsi kila kitu kinawezekana kama ukiwa na nia thabiti na mipango..Huko duniani kuna vitu vinaitwa Futurist na Futurology, Futurist ni watu wanaojihusisha na mambo ya Futurology. Futurology inafahamika kama Future studies (masomo yanayohusu mambo ya baadae), Ni masomo yanoyohusu ku-predict mambo mbalimbali yajayo kwa kufanya tafiti kuangalia mambo yaliyopo sasa hivi na kutabiri mambo yajayo.
Naomba utueleze misingi ya tafiti zao zimejengeka katika nini ? Maana ukijua msingi ndio utajua jambo hilo linawezekana au story za wana Sayansi.
Hujatuambia kwamba ni mambo yote yajayo au ya kisayansi tu ?
Je shuguli hii kwa mara ya kwanza ilianza lini,na je kuna lolote ambalo waliwahi kutabiri likatokea ? Kama lipo ni jambo gani na ilikuwaje ?
Futurist wanapredict mambo yajayo kwa kuangalia siasa za dunia,teknolojia ya mwanadamu, intelligence ya mwandamu, Ustaarabu wa mwanadamu, uchumi,nk nk na kutabiri kua miaka kadhaa ijayo kutakua na hiki au kile.
Unakubali ya kuwa utabiri nje ya ufunuo ni ubahatishaji ? Sasa kwanini wanajishughulisha na kamali/kamari/bahati nasibu?Vipi yasipotokea hayo wanayoyatabiri ? Huoni kama wanapoteza muda na nguvu zao ? Huwa wanasema nini baada ya kufanya tabiri zao ?
Ndio maana nataka kujua misingi ya jambo lao.
Kwa mfano Futurist wanaelezea jinsi labda maisha ya ya mwanadamu dunia baada ya miaka 20, 30, 50 ijayo yatakua ni maisha yatakayokua yame Advance zaidi. Tutakua tunaishi katika Smart World hivyo binaadamu anaweza kusafiri less than 30 min kutoka bara moja kwenda lingine, Binaadamu anaweza kuanaanza kutumia teknolojia ya Artificial Intelligence At large,kilimo,Elimu,teknolojia vitaboreshwa, Dini zinaweza kua zimeungana nyingi kurudi kwenye shina kuu (Hasa ukristo)
Huwa nasema hivi kutokujua mipaka ya akili yako,ni utumwa wa kujitakia.
Kuna mambo hayawezekani kabisa lakini wanasayansi na hao futurist wanataka kuaminisha watu ya kuwa yanawezekana mwisho wa siku wanakuja kudanganya.
Achieve maisha yasiyo na kifo kwa ghalama yoyote ile.
Haya ni matumizi mabaya ya akili.Wanao jaribu kufanya hivyo hawajui kifo ni nini. Kwa maana hiyo hao katika hili tunawaita Wajinga.
Hapa wanajisumbua,kwanza kwa uchache tu kuhusi kifo :
1. Kifo hakihusiani na ajali,kuumwa au mfano wa haya na hizo zinabaki kuwa sababu tu,unaweza usiwe mgonjwa lakini ukafa,au kinyume chake.
2. Kifo ni haki,yaani kama ilivyo haki yako a kula.
3. Kifo ni muda wako tu ukifika huongezewi hata sekunde,utakufa.
4. Hakuna binadamu anaejua ni sejemu au mahali gani atafia,vioi waje kuweza kuzuia kifo. Bila shaka hawa wanafikiri kitoto na kivivu mno.