A.Lusekelo( Mzee wa Upako, Pombe Si DHAMBI, ni kosa.

A.Lusekelo( Mzee wa Upako, Pombe Si DHAMBI, ni kosa.

Ndugu Rabbon, jifunze kujielimisha kwanza kabla ya kuanza kung'ang'ania jambo ambalo huna uhakika nalo kwa 100%. Haya mambo ndiyo yanafanya watu watudharau Walokole, na tuonekane watu wa hovyo.
Hujui zipo Divai zisizo na kileo?

Non alcoholic?

Nawe ni mlokole mnywa pombe?
 
Ewe msabato divai ni pombe

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
Pombe ni nini?

Na Divai ni nini?

Kilevi ni nini?

Kunywa ni nini ?

Kulewa ni nini?

Kipi kipimo Cha ukomo Ili kufikia ulevi?

Lusekelo alianza mdogo mdogo akifichama, saizi hawezi tena jizuia.

KATAA POMBE NA ULEVI 🙏
 
Msilewe Kwa mvinyo ambamo Kuna ufisadi, Bali mjazwe Roho (Waefeso 5:18).

Soma na uelewe, BIBLIA inasomwa Kwa ujumla kutafuta maana, Si kujikita kwenye FUNGU Moja na kuweka judgement.
Amesema msilewe kwa mvinyo na sio msinywe mvinyo.Kunywa mvinyo unywe ila kulewa ni dhambi hivyo unywe kwa kiasi
 
(1 Wakorintho 6:9-11)

Bali walevi, hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mkimbieni haraka Nabii huyu wa uongo.
Hao wanaokumbatia wake zenu na kuwatomasatomasa eti wanawahamishia nguvu za Mungu ndio manabii wa kweli !!
 
Mithali 3:9-10 – "Mheshimu BWANA kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote; ndipo ghala zako zitakapojaa tele, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."

2. Mhubiri 9:7 – "Enenda, ukale chakula chako kwa furaha, na ukanywe divai yako kwa moyo mwema; kwa sababu Mungu amekwisha kuyakubali matendo yako."

3. Zaburi 104:14-15 – "Huotesha majani kwa wanyama, na mimea kwa mahitaji ya wanadamu, ili kuleta chakula kutoka ardhini, na divai iwapendezao mioyo ya wanadamu, na mafuta kuyang'ariza nyuso zao, na mkate umpao mtu nguvu."

4. 1 Timotheo 5:23 – "Usiwe unakunywa maji tu, bali tumia kidogo divai kwa ajili ya tumbo lako na maradhi yako ya mara kwa mara."
 
Back
Top Bottom