McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Alichoandika Hilda Newton:
Nakumbuka January 15, 2026 Buyobe alinitumia namba yake DM akasema nimchek WhatsApp kuna issue tuongee, nilimchek tukaongea.
Alinielezea jinsi alivotekwa na kikosi cha Mafwele, walimvotesa n.k pia alishukuru kwa jinsi tulivompazia sauti.
Katika maongezi hayo aliniambia kwamba pamoja na kwamba ameachiwa kwa dhamana bado watekaji wa Mafwele wanaendelea kumfuatilia hivyo maisha yake yapo hatarini , nilimwambia achukue tahadhari maana hao watu hawana masihara, akasema anafikiria kuondoka nchini, nikamwambia ni wazo zuri, akaniambia kama kuna Taasisi yoyote ambayo naijua inasaidia watu ambao wanachangamoto kama yake nimuunganishe nayo, nikamwambia hakuna Taasisi yoyote ambayo naijua so tukaishia hapo.
Baada ya siku kadhaa alinipigia simu akaniambia, kwamba yupo mahali nilipo anaomba tuonane, tusalmiane na kufahamiana maana hatujawai kuonana zaidi ya humu mitandaoni, nikamwambia kwasasa siwezi kuonana nae kwasababu za kiusalama, nikamwambia kukiwa shwari nitamtafuta mimi mwenyewe, tukaishia hapo.
Baada ya hapo alimpigia simu
@Twaha_Mwaipaya
akamuomba waonane, Twaha alinipigia simu kuniuliza kama namfahamu, nilimjibu Mwaipaya kwamba simfahamu zaidi ya kumuona online hivyo Mwaipaya na yeye akamkwepa badae akampigia simu
@Sativa255
kumuomba waonane.
Baada ya issue ya Mshabaha kutekwa ndo nikajua kwamba kumbe wakati anawasiliana na mimi kuniambia habari za yeye kuondoka nchini kuna mtu mwingine ambae alimshirikisha huyo mtu ndo alimuunganisha na lifeofmshaba ili amsaidie kutoka nchini kwasababu alisema vijana wa Mafwele walikuwa bado wanamuwinda.
Alifika Nairobi akapokelewa na
lifeofmshaba
na kupelekwa mahali pa kuishi, muda wote alikuwa akidai kwamba anaumwa shingo, kichwa na miguu lakini pia alimwambia Mshabaha vitisho vya Mafwele kusema kwamba atamfira + kuonana na watekaji live ni vitu vilimuumiza sana kisaikolojia hivyo alitafutiwa Mwanasaikolojia lakin alipoambiwa aende Hospital kufanya checkup ili wajue Polisi wamemuumiza kwa kiwango gani ili apatiwe matibabu alikataa.
Muda wote wakati Buyobe yupo Nairobi. Mshabaha alikuwa anakwenda kwake kumjulia hali kutokana na madai ya changamoto yake ya afya alokuwa nayo.
Siku ya tatu, Buyobe alimpigia simu Mshabaha akamjulisha kwamba, nyumban kwake kuna mgeni ambae na yeye kalazimika kukimbia Tanzania kwasababu Mafwele anataka kumuua akaenda mbali zaidi akamdanganya kuwa mgeni huyo ni Mwanachama wa CHADEMA wakati si Mwanachama wa Chadema.
Mshabaha alifika mahali alipokuwa anaishi Buyobe akamkutana huyo mgeni ambae Buyobe alimtambulisha kuwa anaitwa Aidan Msuya ni rafiki ake wa miaka mingi.
Buyobe alimdanganya Mshabaha kwamba Msuya alikuwa Diwani wa Chadema wa Ubungo huku akijua fika kwamba Msuya hajawai kuwa Diwani.
Mshabaha alimuliza ndani ya CHADEMA anamfahamu nani Buyobe akasema
@ExMayorUbungo
na Hilda Newton japo kwasasa Msuya hana mahusiano mazuri na Bony.
Ili Mshabaha amuamini zaidi Msuya, Buyobe akamdanganya Mshabaha kwamba Msuya ni boyfriend wa Hilda Newton wakati huo anajua fika kwamba mimi na Msuya hatufahamiani kabisa.
Mshabaha alimwambia kama anamahusiano na Hilda mpigie simu, Msuya akasema hapana itamletea shida, maana amekuja hajajipanga Mafwele amefunga account zake zote za Bank na kama girlfriend wake, akijua yupo Nairobi na akashindwa kumuhudumia itakuwa aibu sana kwake, haya ni maswali walikuwa wanajibu Buyobe na Msuya kwa pamoja na kwasababu walijua wanasema uwongo, wakamuomba Mshabaha asiniambie chochote so Mshabaha akakausha.
Huo ndo ukawa mwanzo wa Mshabaha kumfahamu Msuya ikawa kila akienda kumuona Buyobe anamkuta Msuya kuna wakati walikuwa wanaenda kula pamoja, Mshabaha hakuwa na wasiwasi na Msuya kwasababu ya Utambulisho ambao alipewa na Buyobe, aliamini ni mtu Genuine.
Buyobe akatoa wazo wapate gari maana na hali yake ya kiafya na usalama ni muhimu wakawa na gari, mara wazo likawa linafanyiwa kazi na Msuya.
=====================
Mshabaha anasema mpaka muda huo, kuna mambo mengi yalikuwa yanaanza kwa Buyobe then yanatekelezwa na Msuya.
Kabla ya tukio la Mshabaha kutekwa siku nne nyuma Buyobe na Msuya walimtembelea mzee mmoja wa Kenya, kisha wakamtumia picha Mshabaha kwenye picha yuko Buyobe na Msuya na huyo mzee na mkewe wake.
Wakasema ni mwanaharakati ambae ana knowledge kubwa, kwasababu Mshabaha nae ni Mwanaharakati waliona ni muhimu Mshabaha akaenda kuonana nae kuna mambo atajifunza.
Mshabaha akakubali hivyo wakakubaliana kwamba watapanga siku waende.
Lakini pia Buyobe na Msuya walimueleza Mshabaha kwamba wangependa kufanya training kwa Wanaharakati wote wa Tanzania walipo Nairobi, Mshabaha aliwakatalia na kusema hawezi kuwatafuta watu na kuwakusanya kwasababu ni risk.
Msuya alipoona Mshabaha amekataa mambo ya training akamuomba amkutanishe na Hilda, Maria, Sativa, na Mwaipaya, Mshabaha alikataa mind you huyu mtu ambae anamuomba Mshabaha amkutanishe na mimi, kwenye utambulisho wake alisema kwamba mimi ni girlfriend wake,😂😂😂
Walipoona mpango wao wa kutaka kukutanishwa na watu ambao wanawawinda, umeshindikana ikabidi wamkomalie Mshabaha ili waende nae kwa yule Mzee Mwanaharakati wa Kenya ambae walikubaliana kwamba wataenda nae.
Ikumbukwe Msuya na Azizi walikuwa wanaishi nyumba moja, Buyobe alikuwa anakwenda kwa Msuya ambapo Azizi alikuwepo na ilikuwa ikifika usiku wakati mwingine Aziz alikuwa anakwenda kulala kwa Buyobe na wakati wote huo Buyobe alikuwa anatumia line ambayo imesajiliwa kwa passport ya Aziz.
Hata usiku wa kuamkia siku ya tukio la utekwaji, Azizi alilala kwa Buyobe so wakati wanaenda kwenye utekaji Azizi alitokea kwa Buyobe, Buyobe alipoulizwa ilikuaje akawa anaishi na watekaji, alijitetea kwa kusema kwamba eti alikuwa analala kwa kujifungia chumbani eti hiyo ndo ilikua pona yake.
Sasa tuje siku ya tukio la Utekaji, wakati wanatoka hiyo asubuhi Buyombe alihairisha safari, akawambia Msuya waende tu wenyewe na Mshabaha,wakati huo Mshabaha alijua wanaenda tu kumuona huyo Mzee Mwanaharakati then watarudi
So walikutana sehemu inaitwa China center maeneo ya Kilimani, wakaingia kwenye gari binafsi ambayo Msuya aliikodi, wakaingia Petrol station wakajaza mafuta, kisha wakaanza safari.
Ndani ya gari alikuwepo Mshabaha, Aziz, Msuya na Wakenya wawili, wakiwa njian Msuya aliomba kushuka ili achimbe dawa baada ya Msuya kushuka tu Dereva akakanyaga mafuta so ndani ya gari kukawa na taharuki hapo ndo Mshabaha akaanza kupambana na Aziz na Mkenya wa Africa Kusini, wakaanza kumkaba huku wanamnyeshwa vitu na kujaribu kumchoma sindano muda huo gari ilikuwa speed,
Mshabaha alifanikiwa kufungua mlango wa mbele, akaukanyaga ili usijifunge wakati huo alikuwa anavutana na Azizi huku gari ikiwa kwenye mwendo.
Wakasimama kufunga mlango, Mkenya akashuka lakin kabla hajafunga mlango watu wakiwemo bodaboda wakawa wameshajaa, walipoona nyomi yule Mkenya akarudi haraka kwenye gari, Dereva akawa anaondoa gari kabla hawajaondosha gari vizuri Mshabaha akaruka.
Ndipo Wananchi waliokusanyika eneo hilo wakaanza kumpatia huduma ya kwanza Mshabaha na kuwapigia Polisi na kuwapa details za iyo gari ndipo Polisi walianza kukimbizana na hiyo gari, akina Aziz walipoona mitutu wakasimama na kukamatwa, kisha wakapelekwa kituoni ambako walijaribu kuhonga milioni 10 ya Kenya lakin Polisi Kenya walikataa.
Mwisho walifikishwa Mahakaman kesi Inaendelea.
Baada ya hili tukio ndo simu zikaanza kutembea, badae Mshabaha alivotoka Hospital akanieleza kuhusu huu mkasa wote ndipo akanitumia picha ya Kiongozi wa watekaji (Msuya) akaniuliza kama namfahamu, nikamwambia Hapana simjui labda ngoja tumpost mitandaoni lazima tutapata tu mtu/watu ambao wanamjua.
Ndo hapo Mshabaha akaanza kushagaa kwamba inakuaje mimi simfahamu huyo mtu wakati Buyobe alimuaminisha kwamba mie ni girlfriend wa huyo Msuya, Binafsi nilishangaa sana kwanini Buyobe aliamua kunisingizia jambo la uwongo?
Ndo hawa kwenye hii picha hapa
==========================
Nimuuliza Mshabaha kwanini hakuniuliza, aliniambia kwamba walimuomba asiniambie.
Nilimpigia simu Buyobe, nikamuuliza kwanin alimdanganya Mshabaha kwamba mimi ni Girlfriend wa Msuya wakati anajua mimi na Msuya hata hatufahamiani, alijiumauma sana mwisho akajitetea kwamba Msuya alimdanganya.
Baada ya hapo ndo nilipost picha ya Msuya kuomba watu wanipe taarifa zake, na watu wengine pia wakapost.
Taarifa zikaanza kutiririka ndo hapo tukajua kuwa Msuya baada ya kupiga tukio jioni ya siku hiyo hiyo, alionekana maeneo ya Namanga akivuka kuelekea Dar wakati huo Buyobe yeye alikimbilia maeneo ya Busia (Hii ni kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe) na hapo alifanya bila kuwasiliana na mtu yeyote hata wale waliompokea hakuwajulisha, licha ya kwamba awali wakati anafika alisema haijui kabisa Kenya ni mara yake ya kwanza kufika Kenya.
Kupitia taarifa izo tulizopokea ndo tulijua kwamba Msuya na Buyobe ni marafiki tangu Buyobe akiwa anafanyakazi Tanroads na zamani walikuwa wakiishi majirani, maeneo ya Ubungo Msewe.
Msuya baada ya kufika Dar alimpigia simu
@ExMayorUbungo
, akamuomba waonane maana anachafuliwa mitandaoni, Bony alikubalia so Msuya akaenda nyumban kwa Bony, alikiri kwamba ni kweli alienda Nairobi, ni kweli alionana na Mshabaha, Buyobe, Aziz na wale Wakenya wawili ila akasema hausiki na utekaji na wala hakuwepo kwenye tukio kabisa.
Wakati Bony anazungumza na Msuya Buyobe alimpigia simu Msuya, akamwambia na yeye amekimbilia Busia maana ameona baada ya hilo tukio wale watoto watamng’ang’ania, wakapiga story kidogo then Buyobe akakata simu.
Badae Bony alizungumza na Mshabaha ili asikilize na upande wake, Mshabaha akamueleze tukio lote akampa na ushaidi wa namna ambavyo Msuya amehusika.
Bony alimpigia simu Msuya, akamuuliza wewe umesema haukuwepo eneo la tukio, mbona maeneo yote mlikopita unaonekana kwenye CCTV ukiwa pamoja nao, Msuya akamwambia ngoja kwanza nitakupigia ndo akapotea mazima.
Baada ya kufeli kwa mpango wa kumteka Mshabaha na Wanaharaki wengine, Buyobe alirudi bongo licha ya kwamba alisema maisha yake yapo hatarini, Mafwele anamuwinda.
Naomba niwarudishe nyuma kidogo baada ya Buyobe kuachiwa kwa dhamana alimpigia simu
@IAMartin_
akamuelezea kwamba anaomba msaada wa Wakili kwasababu anatakiwa kwenda kuripoti Polisi.
Aliunganishwa na Wakili then siku ya pili akasindikizwa kureport, wakati wanafika Chang’ombe Polisi njee ya kituo wakakutana na RCO, RPC, OCCID na Askari wengine ambao ni wapelelezi pamoja na Wanachama wa Chadema ambao na wao walikuwa wameenda kuripoti.
Mashuhuda wanasema RCO alimuita Buyobe “Wewe njoo hapa” Buyobe akasogea walipo.
RCO akamwambia chuchumaa chini, Buyobe akachuchumaa, RCO akamwambia, tumekupa dhamana kwanini umeenda mitandaoni kutushambulia kwa mambo ya uwongo au Tukufutie dhamana?
Buyobe akaanza kujitetea kwamba account yake ya X (Twitter) inaendeshwa na watu wengi na aliyewashambulia kupitia account hiyo ni Martin Maranja Masese, RCO akachukua pen na karatasi akaandika jina la MM ili akamatwe na kuhojiwa, Halafu kipindi hiko ilikuwa ni baada ya Oktoba 29 watu walikuwa wanapewa kesi za uhaini sana.
Wakili aliyemsindikiza pamoja na baadhi ya Wanachama wa Chadema waliokuwa pale njee wakamwambia Buyobe “Oya vipi mbona unataka kufanya mambo yawe makubwa, kwanini unataja watu ambao hawausiki” walimind sana.
Badae Wakili alimshauri aombe msamaha, ndo Buyobe akaomba msamaha na Wakili nae akawa anakazia kwa kuwambia Polisi wamsamehe.
Sasa wakati anaomba msamaha RCO na RPC wakaanza kumuuliza kwamba “Tuwaambie hawa watu wa Chadema ili wakujue wewe ni nan, unajifanya wewe ni mpambanaji/Mwanaharakati wewe ni Mwanaharakati kuanzia lini?
Pale pale mbele ya wanachama wa Chadema na Wakili, Buyobe akaanza kuomba msamaha huku akimsihi RCO asitoboe siri “Nakuomba mkuu usiseme”
RCO akawauliza watu wa Chadema kwamba nyie mnamtetea huyu jamaa mnajua vizuri?
Watu wanasema kila mmoja alibaki anashangaa maana walikosa majibu wakati huo Buyobe yeye alikuwa amenywea, kimya!
===============================
Mashuhuda wanasema RCO na RPC walimuwashia moto sana, badae wakamwambia awafuate ili akatoe maelezo ya ziada so wakaingia nae ndani ya kituo cha Polisi.
Walipoingia ndani kuna baadhi ya Wanachama wa CHADEMA, walijiongeza wakawafuata wale Askari waliokuwa pale njee, wakawauliza kwani Buyobe ana issue gani kubwa mpaka kamuomba RCO asiiseme mbele yetu?
Wale Askari wakawajibu kwamba walipoenda kumkamata Buyobe nyumbani kwake Kigamboni alijitambulisha kuwa yeye ni ofisa wa TISS, wakamchukua na kuondoka nae kulekea kituo cha Polisi Chang’ombe.
Walipofika Polisi wakamuomba atoe password ya simu yake, akatoa wakaingia kwenye WhatsApp yake wakakuta anawasaliana na Mkuu wa Dawati la Siasa wa TISS, Thobias Mwesiga na alikuwa anampa info za watu mbalimbali,(Japo Mwesiga kwasasa kaondolewa kwenye hiyo nafasi) mtu mwingine ambae alikuwa akiwasiliana nae ni Abdul mtoto wa Idd Amin Mama.
Lakin pia alikuwa anawasiliana na baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri na kote huko alikuwa anajitambulisha kama afisa wa TISS so Polisi baada ya kuona mawasiliano yake na hao watu, hata wao wenyewe waliogopa.
So hao Wanachama wakajua issue ni nini so waliondoka zao ila walimwacha Buyobe pale kituoni na Wakili ambae alikuwa kamsindikiza.
Mwisho kabisa hii sio vita ya maneno ni uhalisia wa mambo na kwa tulipofika sasa ili kulikomboa Taifa letu lazima kwanza tulindane kwa kuepushana na hatari zinazoepukika.
Nawatakia siku njema.