Aamua 'Kukojolea' Kitoweo (Mboga) baada ya Kunyimwa Ugali (Chakula) makusudi na wana Familia wake

Aamua 'Kukojolea' Kitoweo (Mboga) baada ya Kunyimwa Ugali (Chakula) makusudi na wana Familia wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Huwa napenda sana Watu ( Binadamu ) wenye Maamuzi magumu na ya papo kwa hapo kama huyu Baba na ningemjua ningempa Zawadi ya Mbuzi au Ng'ombe kama ambavyo hata Mshambuliaji Hatari wa Yanga SC Fiston GENTAMYCINE Mayele amekuwa akizawadiwa kwa Kutekeleza vyema Majukumu yake.

Yaani Mimi ndiyo Baba mwenye Nyumba ambaye pia Nahangaika Kutwa kuwatafutia Chakula Familia yangu halafu narudi kutoka katika Mihangaiko yangu nawakuta mnakula na Mimi mmeniachia tu Ugali huku Mboga ( Kitoweo ) mkininyima kwanini 'nisikikojolee' tu ili niwakomeshe na tukose Wote?
===

HABARI KAMILI
Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) kupitia mradi wake wa AWARE 2020, limembaini baba mmoja (Jina limehifadhiwa) Mkazi wa kijiji cha Damankia Ikungi mkoani Singida ambaye anadaiwa kulewa na kukojolea unga na kitoweo kwa lengo la kuwakomoa mkewe na watoto baada kutishiwa kunyimwa chakula.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa amekuwa akishindwa kuihudumia familia yake, na amekuwa akifanya kitendo hicho mara kwa mara licha ya kufikishwa ngazi ya kata lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema tukio hilo liliibuliwa hivi karibuni na Salim Hassan ambaye ni Katibu wa kamati za vijiji za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) wa kijiji hicho wakati wa kikao kilichohusisha jeshi la polisi, wenyeviti wa vijiji, mahakama na madiwani kwa lengo la kushughulikia kesi za watuhumiwa wa ukatili.

Chanzo: Swahili Times
 
Huwa napenda sana Watu ( Binadamu ) wenye Maamuzi magumu na ya papo kwa hapo kama huyu Baba na ningemjua ningempa Zawadi ya Mbuzi au Ng'ombe kama ambavyo hata Mshambuliaji Hatari wa Yanga...

Mimi ninachojua ukiwa baba nikuhakikisha familia inapata, chakula, mavazi, na makazi bora..... na thamani ya mke nikumpa heshima na watoto wako uwapeleke shule” iyo kukojolea mboga ni upuuzi baba gani sasa uyo?

Mimi Om kwangu nina mke dada wa kazi na mtoto mmoja, sasa dada ww kazi ni namba kweli kweli anakula sio poa kwaiyo sometimes unakuta mke katenga chakula changu lakini nikirudi sishibi na hawajawai kujua kama sishibi.

Kwasababu mwanangu ana afya mzuri na Naona bora dada anavyokula sana chakula chetu kuliko ale vyakula vya mwanangu maana mtoto ana vyakula vyake tofauti na sisi,

Kuna time nakasirika lakini nikimuangalia mwanangu alivyo na afya Naona poa tu..... kwaiyo baba sometimes sio tu mboga imeisha unaweza kula na usishibe sasa utaanza kuwaka hushiba?
 
GENTAMYCINE wewe ni msela wangu lakini kwenye hili sikuungi mkono. Ukiwa faza hutakiwi kukazia utopolo kama huo. Hapo kama ni mimi ningeondoka nikaagize makange ya kitimoto kilo nzima ninywe na konyagi moja nirudi kumtindua wife.

SASA HUYO JAMAA YAKO HAJANUNUA MBOGA AMERUDI KALEWA CHANG'AA ANATOA DUDU MBELE YA WATOTO ANAKOJOLEA MSOSI USIMSIFIE.
 
Huwa napenda sana Watu ( Binadamu ) wenye Maamuzi magumu na ya papo kwa hapo kama huyu Baba na ningemjua ningempa Zawadi ya Mbuzi au Ng'ombe kama ambavyo hata Mshambuliaji Hatari wa Yanga SC Fiston GENTAMYCINE Mayele amekuwa akizawadiwa kwa Kutekeleza vyema Majukumu yake....
Unatuchanganya sana, we si ulisema ni mwandishi wa habari?! Huko hamsomi ethics? Hivi kufanya kosa kunasuluhishwa kwa kufanya kosa lingine (kosa juu ya kosa)? Mimi nadhani ungekemea, lakini badala yake unashabikia! Noma sana.
 
Mimi ninachojua ukiwa baba nikuhakikisha familia inapata, chakula, mavazi, na makazi bora..... na thamani ya mke nikumpa heshima na watoto wako uwapeleke shule” iyo kukojolea mboga ni upuuzi baba gani sasa uyo?...
Usikae kimya,mnongoneze wife akutengee Cha kutosha km kipo
 
GENTAMYCINE wewe ni msela wangu lakini kwenye hili sikuungi mkono. Ukiwa faza hutakiwi kukazia utopolo kama huo. Hapo kama ni mimi ningeondoka nikaagize makange ya kitimoto kilo nzima ninywe na konyagi moja nirudi kumtindua wife.
SASA HUYO JAMAA YAKO HAJANUNUA MBOGA AMERUDI KALEWA CHANG'AA ANATOA DUDU MBELE YA WATOTO ANAKOJOLEA MSOSI USIMSIFIE.
Aibu kabisa
 
Mimi ninachojua ukiwa baba nikuhakikisha familia inapata, chakula, mavazi, na makazi bora..... na thamani ya mke nikumpa heshima na watoto wako uwapeleke shule” iyo kukojolea mboga ni upuuzi baba gani sasa uyo?...
Hongera kwa kupata mke anaejali. Lakini ni vyema kupaza sauti kama haushibi. Kisayansi tu unamwambia wife aongeze ratio ili dada ashibe zaidi maana the more atakavoshiba ndo atavopunguza kula kupitilizA.
 
Mimi ninachojua ukiwa baba nikuhakikisha familia inapata, chakula, mavazi, na makazi bora..... na thamani ya mke nikumpa heshima na watoto wako uwapeleke shule” iyo kukojolea mboga ni upuuzi baba gani sasa uyo?...
Labda huna hela ya kuongeza, kama hushibi badala ya kupika robo Kila siku jiongeze wapike walau nusu ushibe badala ya kuja kumsema house girl humu jf eti anakula sana.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ninachojua ukiwa baba nikuhakikisha familia inapata, chakula, mavazi, na makazi bora..... na thamani ya mke nikumpa heshima na watoto wako uwapeleke shule” iyo kukojolea mboga ni upuuzi baba gani sasa uyo?..
Muombe radhi huyo dada hata kimyakimy
 
Labda huna hela ya kuongeza, kama hushibi badala ya kupika robo Kila siku jiongeze wapike walau nusu ushibe badala ya kuja kumsema house girl humu jf eti anakula sana.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app

Akili huna wewe jamaa!!! Sizani kama hapa tunaongelea kuwa na hela au kutokuwa na hela.... mada ni ubabe wa baba kukojolea chakula kwa familia yake kwa kukosa mboga.

Kuwa baba sio kitu rahisi, kama wewe sio baba muwajibikaji kwa familia huwezi nielewa..... nataka nikwambie kwangu chakula sio tatizo hata kidogo mimi ni mkulima na sio mkulima mdogo kama wewe unavyoota!!!! Kwaiyo chakula kwangu sio tatizo”

Ukiwa baba muwajibikaji huwezi kufanya alichofanya uyo baba kwenye mada tajwa!!!

Mimi ni baba nawajibika kwaajili ya familia yangu huko kazini kwangu kuna muda naweza kushinda bila kula lakini huwezi kuja kwangu ukakuta kuna shida ya chakula, hayo y dada wangu usizingatie sana lengo ni kuelimisha ni jinsi gani baba anapaswa kuwa!!!

Kwaiyo kama mimi sikushiba nani nyumbani kwangu nikojolee chakula wanachokula watu wangu iyo ndo ubaba???
 
Back
Top Bottom