Abbas Tarimba, wewe uko tayari mtoto wako afe badala ya mtoto wa boss wako?

Abbas Tarimba, wewe uko tayari mtoto wako afe badala ya mtoto wa boss wako?

"Mtu anatolea mfano mtoto kipenzi wa rais et akitobolewa macho itakuwaje? Huu ni utovu mkubwa wa nidhamu anajua uchungu wa kulea kweli? Nashauri chama changu kimuite kamati ya maadili achukuliwe hatua hatuwezi kuwa na mtu ana kadi ya chama halafu anatusumbua"_kauli ya mbunge wa jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba.

Kwa maneno hayo Abbas unamaanisha Uhai wa Abdul uliyemuita "Mtoto Kipenzi" ni wa thamani kuliko Uhai wa watoto wa Watanzania wengine? Je wewe binafsi uko tayari kupoteza Mtoto wako badala ya Huyo Mtoto Kipenzi? Unataka watu waone Uhai wa Abdul ni Bora kuliko Uhai wa Mzee Kibao, Mdude, Soka, Chori na wengine waliopotezwa nchini? Yaani mama zào waridhike na vifo vya watoto wao Kwa vile "Mtoto wa Taifa" yeye hajadhulika?

Mbunge unafikia hatua ya kuthaminisha Uhai wa Watanzania Kwa madaraja?
Kinondoni mmetukosea Sana.
Nadhan ni sarcasm kwa yule mama.
 
Gwajima alitolea mtoto wa Rais kama mfano.....lakini pia alitoa mfano wa mwanae pia anaitwa Jordan...
Hili zee sijui limetokea wapi...

Haya mazee yenye uraia wa kuunga unga ni tatizo.
 
Back
Top Bottom