MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
DC wa Mwanga Mheshimiwa Abdallah Mwaipaya najua kuwa ulikuwa Radio One na ITV na ulikipenda mno Kipindi chako cha Mazungumzo ya Familia cha kila Jumapili ukiwa na Pacha wako Farhia Middle.
Kwa Mshangao kabisa leo nimekusikia nawe ukipiga Simu ( japo najua uliipiga ya Farhia Middle ) na Kuanza Kuchangia Mada za Masuala ya Mahusiano na mengineyo huku ukijisahau kuwa hivi sasa Wewe ni Mheshimiwa na Maadili hayakuruhusu hivyo.
Labda leo nikusaidie tu DC wa Mwanga Abdallah Mwaipaya kwamba kwa Hadhi yako kwa sasa unachoweza kufanya ni kuwa Msikilizaji wa hicho Kipindi ( ambacho kilikuwa chako na Farhia ) kabla ya Uteuzi wako na kama Mada ikikugusa unaweza kutuma Meseji ya Kusalimia na Kupongeza kwa Kipindi kizuri itatosha sana.
Lakini kwa hiki ulichokifanya leo tena DC mzima tunayetegemea upo busy Kushughulika na Changamoto tena za Watu wa huko Mwanga kupiga Simu Saa 3 Radio One, Kuchekacheka, kupiga Stori na Kuchangia sidhani kama kina Afya kwa Wadhifa huo ulionao sasa.
Ulishakuwa Radio One na ITV na sasa ni Mkuu wa Wilaya hivyo tafadhali achana na ya huku na Jikite na Majukumu yako hayo mapya, makubwa na mazito na kama labda bado unapenda kuendelea Kutangaza basi andika Barua ya Kuachia ngazi kwa Mama ( Rais ) Samia ili akutoe na urejee Radio One katika hicho Kipindi chako uendelee Kubebishana na Rafiki yako Kipenzi wa Redioni Farhia Middle.
Nawajua Watangazaji wengi tu tena waliokuwa Wazuri kukuzidi katika Media zingine ila tokea Wateuliwe hawana muda tena wa kupoteza Kufuatilia Vipindi vyao bali sasa wamejikita zaidi katika Kuwatumikia Wananchi na kuwaletea Maendeleo yao.
Huyo Mtangazaji Farhia Middle ambaye ndiye anapenda na Kukulazimisha sana uwe unachangia katika hicho Kipindi kuwa nae makini kwani atakuponza kama vile Samson alivyoponzwa na Delilah na utakuja Siku moja Kunikumbuka Mimi Mightier wa hapa JamiiForums.
Ni matumaini yangu kuwa utanielewa DC wa Mwanga Abdallah Mwaipaya kwa huu Ushauri wangu, ila kama kuna mahala nimekukwaza kwa huu Uwazi wangu Kwako naomba Radhi sana.