Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Hali ndani ya Chadema si shwari. Kama imefikia hatua kiongozi mwandamizi ndani ya CHADEMA bila aibu anampeleka Abduli kwa Lissu kumshawishi achukue rushwa. Tena anamwambia kuwa watu kibao ndani ya chama wamechukua na wewe chukua, hii ni hatari sana.
CCM wametumia technic ya kimafia sana, imewapa njaa makamanda, kisha inapenyeza "asali" kwa wachache. Basi makamanda mtifuano mtindo mmoja.
Wachache ambao ni waadilifu kama Lissu wanaanza kuonekana maadui maana wao wanamaanisha katika kuwakomboa watanzania dhidi ya uongozi mbovu wa CCM, kumbe wenzake wapo kimchongo zaidi ndani ya Chadema.
Halafu kuna watu wanasema eti Lissu anyamaze, akayaongelee "chumbani". Mnataka ubakaji wa haki uongelewe sirini?.
Msikilize Lissu hapa akieleza namna kiongozi mwandamizi ndani ya Chadema alivyotaka Lissu naye ale rushwa!.
Tena kumbe huko Chadema kuna Listi ya waliokula hela ya Abduli. Hatari sana hii!
View attachment 3065586
Marehemu maalim Seif aliwaambia wapemba , Ukipewa pesa na CCM usiziwache , zichukuwe, jawabu utawapa kwenye sanduku la kura , kule usiwape kitu