Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdulrahman Omari Kinana amedai Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kililipwa Tsh. Bilioni 2.7 ikiwa ni malipo ya ruzuku ya miaka mitatu kutoka Serikalini, mchakato ambao ulifanyika wakati wa mazungumzo ya maridhiano baina ya CCM na CHADEMA.
Amesema “Ruzuku inapitia katika Bajeti ya Serikali na ikishapita haipatikani tena lakini Rais (Samia Suluhu) akaagiza Serikali kutafuta utaratibu wa kuwalipa na wakasema mkitupa hizo hela itakuwa mwanzo mzuri wa kutambuana, wakalipwa lakini hawakuwahi kusema japo madai yao yalikuwa yamepitwa na wakati.”