Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Abel na Kaini (kizazi cha Adamu na Hawa); Je, wake zao ni kizazi cha nani?

Hakuna swali gumu hapo, mtoto wa kike na wa kiume anayeendeleza ukoo ni mtoto wa kiume, katika biblia Watoto waliotaji ni wa kiume aimaanishi kuwa adama na hawa walikuwa na watoto wa kiume tu, Watoto wa kike alikuwa nao. Ili ukoo kuendelea unaitaji mtoto wa kiume ndiyo waliopewa nafasi kuelezewa vizuri wanawake walio waoa, fuatilia kuhusu uzao wa yesu kutoka Ibrahim mpaka yoseph watu wote waliotajawa ni wa kiume tu, Je Watoto wa kike hawakuzaliwa , yakobo, yusuph walikuwa na watoto wengi sana chunguza vizuri kuhusu Watoto walio elezewa katika maisha yao utagundua Watoto wa kiume tu.
Je Kaini na seth walioa dada zao?
 
Aliewaumba ndo alieruhusu ndugu wa damu pia waoane. Kuna uwezekano watoto wa Adam walioana wenyewe. Hiyo mila iliendelea hata waebrania walikuwa wanaoana ndugu. Mfano Ibrahim alimwoa sara mdogo wake, baba moja ila mama tofauti. Hivo ni watoto wa mzee Tera walioana. Ndo maana kila anakofika ibrahimu alimtambulisha mkewe ni dadake. Ndugu kuoana kwa waebrania si jambo geni sana ingawa baadae walipunguza mila hizo
Hata leo kuna jamii za watu wanaoa ndugu zao mfano waarabu
 
Mkuu Apollo nashukuru sana kwa maelezo yako kuhusu maoni ya vitabu tofauti vya kidini (vitakatifu). Mimi kama mwanadamu wa kawaida sipingani na imani yeyote ile, napenda sana kusoma Quran, Torati na misahafu mingine ili kupata busara ya kila upande. Tukirudi kwenye mada ya kitabu cha mwanzo hiki ndio msingi wa Biblia yote, hivyo unapokuwa na shaka nayo basi Biblia nzima itakuwa batili. Uandishi wa kitabu cha mwanzo upo simple sana kama vile unapotaka kumweleza mtoto wa miaka mitano jinsi ulivyojenga nyumba, utatumia lugha rahisi sana ili aweze kuelewa.
Wengi wanajaribu kuingiza sayansi kwenye sura hii lakini tukumbuke tofauti kubwa kati ya sayansi na Maandiko matakatifu. Sayansi inahusika zaidi with physical or material truth yaani lini na kwa njia gani ulimwengu uliumbwa wakati Maandiko matakatifu yanahusika zaidi with moral and supernatural truth, yaani nani na kwa nini kaumba ulimwengu.
 
biblia imesema watu wakuu ni akina nani?
Kwa kusema watu wakuu ina maanisha 'main characters'
upo mstari kwenye biblia unaokiri kwamba mengi hayakuandikwa kwa vile kama kila kitu kingeandikwa hata ulimwengu usingekuwa na nafasi ku accommodate maandishi hayo! Yaani waandishi wa biblia walijikita zaidi kusimulia part yenye makusudi zaidi na sio kila tukio/kila mwanadamu aliyekuwepo.
 
Mkuu Apollo
Wengi wanajaribu kuingiza sayansi kwenye sura hii lakini tukumbuke tofauti kubwa kati ya sayansi na Maandiko matakatifu. Sayansi inahusika zaidi with physical or material truth yaani lini na kwa njia gani ulimwengu uliumbwa wakati Maandiko matakatifu yanahusika zaidi with moral and supernatural truth, yaani nani na kwa nini kaumba ulimwengu.

Yeah mkuu. You makes points nzuri.

Mimi kwa ipande wangu nafahamu kuwa sayansi na dini vilikuwa ni kitu kimoja. Kila jamii ilitumia dini kuelewa ulimwengu na mwanadamu. Baada ya Renaissance years maeneo mengi kama Europe na Asia kukaanza kutokea mvutano baina ya sayansi na dini. Ilitokana na kuboreshwa usafiri wa majini na watu kusafiri kwenda mabara mengi kama Australia, America na kugundulika kwa Subsaharan Africa. Watu wakaanza kuhoji mbona kuna watu mabara mengi na walifikaje? Mbona ni tofauti na wanadamu wa jamii zingine na waliumbwa na nani?

Ikaja kukua kwa tafiti ambazo zilikuwa zinadhaminiwa na makanisa. Mfano kanisa la Roma lilikuwa na vyuo vyake na maabara tangu kale zilikuwa mali za Antiquities. Wakatokea watafiti kama Gregory Mendel wakasema kuwa sio Mungu anayepanga mtoto aweje bali ni genes. Akatokea Lucretius na mapaka Galileo Galileo na kusema kuwa dunia haipo katika kama walivyokuwa wanadhani. Zamani kutokana na kutumia biblia watu waliamini dunia ni flat, ipo kwenye centre ya ulimwengu kwa sababu ndipo makao makuu ya lengo la ulimwengu na hawakujua kuna mabara ambayo watu hawakujua ukristu kabisa wala hawakuwa na dini zozote zilizofahamika katika Europe na Middle East.

Kutokana na zamani watu walikuwa wanapenda kukusanya vitu vya upekee kama vitu vya kihistoria watu walikusanya mawe wakayaita "Thunderbolts". Mawe haya yalikuwa ni mawe yamechongwa kama ncha (hivi sasa ni yanafahamika kama ni stone tool). Waliamini ni mawe ambayo yalikuwa yanayoka katika radi ikipiga. Waliita ni ncha za radi kwa jinsi yalivyochongwa. Mawe haya yalipatikana kwa mara ya kwanza katika bonde la Acheul nchini Ufaransa. Tazama Thunderbolt myth.

https://www.folklore.ee/folklore/vol42/johanson.pdf

Wakatokea watu kama Darwin ambao nao walikuwa wanasomeshwa na sponsorships za makanisa. Walikusanya mabaki ya mifupa ya kale na kugundua kuwa mwanadamu ameishi miaka mingi sana duniani kabla ya maandiko ya Adam na Hawa. Ikawa na mzozo mkubwa sana kati ya kanisa na watafiti. Kwa sababu sayansi na dini vilikuwa pamoja na dini ndio zilikuwa zinadhamini sayansi ili zipate nguvu ya ushahidi wake kuwa dini ni kitu cha kweli na vitabu vya imani vilisema kweli.

Utata ule wa kuuliza uumbaji ulifanyika miaka gani ukapelekea kanisa kutengeneza chronology kupitia masimulizi ya Biblia. Walijumlisha kila miaka ya Characters wa biblia, uzao mpaka uzao na kuangalia mwanzo kabisa ilikuwa miaka mingapi kabla ya Yesu. Hiyo njia inaitwa "Generation Chronology". Askofu Usser na mwenzake wakasoma biblia mwanzo mpaka mwisho wakasema ulimwengu uliumbwa mwaka 4004 kabla ya Yesu. Miaka hiyo ni miaka ambayo Biblia inasema kutokana na kujumlisha miaka ya uzao mpaka uzao na kila characters na kuongeza miaka.

Ussher chronology - Wikipedia, the free encyclopedia

4c0e828fc7696d9fa4013946d3899ad4.jpg

Nakala za Chronology kupitia miaka ya Biblia kuangalia uumbaji ulianza mwaka gani.

e8c9854ca239233a989c18c538ef3a74.jpg

Archbishop Ussher

Ikapita miaka na kila mtu akaridhika na utafiti wa Biblia kujibu hilo swali.

Ikaja miaka ya Enlightenment period. Ndipo utengano wa sayansi na dini ulipoanzia. Ni baada ya ugunduzi wa geology.

Charles Lyell aligundua theory ya Uniformitarianism na Sedimentary theory. Aligundua kuwa dunia kila siku inajiumbwa. Dunia inachange over time to time. Kwa kufahamu miamba, ulimwengu unavyokua, akagundua kuwa kila siku Earth changes slowly. Mazingira ya sasa hayapo exactly kama zamani. Earth geology yake inabadilika. Hapo ikawa against na biblia kuwa milima iliyopo hivi sasa ipo tangu mungu alipoumba. Na uumbaji ulishaisha. Haiwezi kutokea mlima kutokea tena kwa sababu kila kitu kipo static tangu uumbaji. Hiyo ilikuwa theory ya uniformity. Theory ya sedimentary aligundua kuwa vitu vilivyofukiwa vinaweza kuonyesha kipi ni cha kale zaidi. Vitu vilivyo chini kabisa ya ardhi vina uwezekano kuwa ni vya kale kuliko vilivyopo juu ya ardhi.

d70dbda9db927376e4498612f2339d66.jpg

Sir Charles Lyell

Theory hizo zikazaa Geology. Charles Lyell akawa baba wa Geology na akatoa theory ambazo watafiti wakaanza kugundua kuwa kama dunia haipo static inachange basi hata mwanadamu hawezi akawa ni yule yule static tangu uumbaji yupo sawa. Pia wakaanza kuchimba ili kugundua mabaki ya kale yaliyopo chini na walikuwa hawana dating methods. Hivi wakawa wanatumia theory ya Lyell ya sedimentary kuwa kilichopo chini zaidi ndio cha kale.

Wakagundua mifupa ya wanyama ambayo haipo kwenye biblia kabisa. Mifupa ya Dinosaurs ambayo walikuwa ni wanyama wakubwa sana. Walipatikana katika tabaka la miamba ambayo hakuna ushahidi wa mabaki ya binadamu. Wakagundua kuwa dinosaurs hawakuwa wanaoshi kipindi ambacho mwanadamu alikwepo. Kitu ambacho mpaka leo ni kweli. Miaka ya dinosaurs homo sapiens hakwepo. Na mwanadamu angekwepo asingeweza kuishi. Hivyo wakapinga biblia na kusema biblia ni kitabu cha hivi karibuni sana.

Akaja Charles Darwin akachunguza mifupa ya mwanadamu wa kale na kugundua kuwa mwanadamu zamani hakufanana na mwanadamu wa sasa. Wanadamu na viumbe vyote vinabadilika kutokana na mazingira katika kipindi kirefu cha miaka. Akajibu swali la kwanini tunatofautiana rangi na baadhi ya maumbile wanadamu na akaelezea inakuwaje viumbe vinabadilika.

Akatoa theory ya Evolutio ambayo imeshika nafasi mpaka leo. Ikapinga theory ya creationism iliyoamini mwanadamu aliumbwa kama alivyo sasa na waliumbwa wanyama wote kama walivyo sasa na hawabadiliki.

Evolution ikapewa kipaumbele kutokana na ushahidi mzuri na ushahidi unaoonekana.

Tangu enlightenment era wanasayansi walianza kufanya tafiti zao kwa siri kwa sababu walikuwa wanatengwa kutokana na kuwa tofautu kiimani na wengine walikuwa wanauawa. Wakafanya kazi zao underground kwa vificho.

Mpaka miaka ya 1800 sayansi ikaanza kuwa taasisi binafsi isiyo na muingiliano wa dini.



Lakini sasa mkuu tazama utaona conflict kubwa ya sayansi na dini ipo katika Abrahimic religions. Ukisoma imani za kihindu, wao huwezi kusikia wanapingana na sayansi. Ukisoma Taoism na Buddhism nao wanaaminika ni religions ambazo zina 90% ya kuwa sawa na sayansi. Kwa sababu zinabadilika na hazishikilii imani bila evidence. Mfano Buddhism inakubali kubadilishwa kama jambo litakuwa na ukweli na lina ushahidi wa kweli. Pia imani kama Buddhism na Tao hazina Maelezo ya kuwa kuna Mungu, anaitwa nani, aliumbaje dunia ila zimekaa katika msingi wa nidhamu tu. Wao uwe atheist au religious hiyo haijalishi. Kinachojalisha ni jinsi mtu unavyoishi na unayotenda.

Kama unatenda mazuri hata uwe mwanasayansi au religious person its okay lakini kama unatenda mabaya haya uwe atheist, padre au sheikh we bado hujitambui. Hivyo what matters sio beliefs bali ni matendo yako. Kutoua, kutozini, kutoiba, kutotumia vilevi na madawa, na kutosema uongo. Ndio misingi ya imani.

Kwao mambo ya dunia iliumbwaje wao wanaachia sayansi. Na ndio maana huwezi kuona Asia spirituality ina gombana na sayansi hata kidogo. Kwa sababu wanabadilika kuendana na facts, kwao imani sio muhimu bali ni matendo, sio lazima uamini kila kitu na wanafundisha jinsi ta kuishi kwa manufaa yako na wanadamu wengine kwa sasa na katika mazingira na viumbe vyenye uhai katika maisha haya ya sasa bila kujali baadaye ninj kitafuata baada ya kifo. Just use this life kutenda mema.

Mkuu naomba niishie hapo naamini kama umesoma mwanzo mpaka mwisho utakuwa umekusanya mengi.

Karibu.

10e0972d965bc1df27eb16c05f45513a.jpg


2465464cf7b5e06a36fa412095abaedb.jpg
 
Nilisikia walizaa mapacha wa kike na kiume kwa hiyo wakaoana kwa kubadilishana yaani mfano amuoe pacha wa abeli na ukiziangatia zamani hawakuhesabu wanawake. Mi mwenyewe sijui ila nimejibu kutokana na kusoma huhkuhuku JF.
Very tishable [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
majibu yaliotolewa naamini yamekidhi swali lako, kama bado nakushauri uweke biblia yako pembeni na uingie google utafute 'human evolution'
 
Ndio ubaya wa story za kutunga....mara nyingi zinaishia hewani pasipo na majibu ya maswali yatakayo ibuka....kama Mungu ndiye aliyeumba watu basi angeumba wanawake na wanaume wakutosha ili wasizalishane ndugu kwa ndugu.....na kama aliruhusu ndugu kuzaliana, kwa nini akataze sasa hivi???
God is very clever, kwa hili la kukataza ndugu kuzaliana hata wanasayansi wasiomjua Mungu wanalikubali becoz of genetic reasons
 
God is very clever, kwa hili la kukataza ndugu kuzaliana hata wanasayansi wasiomjua Mungu wanalikubali becoz of genetic reasons
Yeah! ni kweli wanasayansi wanakataza ndugu kuzaliana ili kupunguza ule uwezekano wa kusambaza magonjwa ya kijenetiki.Ila hilo la kusema Mungu ni clever kuna shaka hapo,....kama Mungu ni 'clever' kwa nini aumbe magonjwa ya kijenetiki?
 
Binadamu wa kwanza kuumbwa Na Mungu ni Adam Na Hawa.Watoto waliowazaa ni Abel Na Kaini.Abeli Na Kaini walioa je Wake zao ni kizazi cha nani?
Abel na kaini hawakua watoto pekee wa Adam na Eva!..biblia imeandika au imesimulia upande wa dhambi ilipoanzia,kutawanyika hadi alipozaliwa mkombozi!! ...haielezi tu kila sehem!!
Ni sawa tu ilivoeleza upande wa yakobo zaid kuliko wa Esau!! Kwa sababu tu upande wa yakobo ndio alipatkana mkombozi !!!
 
Yeah! ni kweli wanasayansi wanakataza ndugu kuzaliana ili kupunguza ule uwezekano wa kusambaza magonjwa ya kijenetiki.Ila hilo la kusema Mungu ni clever kuna shaka hapo,....kama Mungu ni 'clever' kwa nini aumbe magonjwa ya kijenetiki?
Ni kitabu gani kwenye Bible kinachosema Mungu aliiumba magonjwa? Mungu ni mwema sana, magonjwa yalikuja baada ya dhambi na dhambi haikuletwa na Mungu. Hebu kasome the Book of Genesis vizuri
 
Back
Top Bottom