Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Tangu Scandinavia iondoke barabarani kwa kweli abiria wa njia hii wanasafirishwa kama wafungwa, hakuna utaratibu unaeleweka mkiwa safarini.
Kwa mfano, haieleweki abiria wanakula hoteli gani, wala haijulikani hata abiria anatakiwa kula kwa dakika ngapi, basi inasimama kwenye hotel yoyote ambayo dereva ameahidiwa chakula cha bure, abiria mnatangaziwa kutumia dk 10 tu kula na kuchimba dawa, wakati huo huo abiria wa siti ya nyuma anatumia zaidi ya dk 5 kushuka, maana ni lazima asubiri walio mbele yake washuke kwanza, wakiwemo wagonjwa na wazee ambao hutembea taratibu, Scandinavia ilikuwa inatoa dk 15 ambazo zilianza kuhesabiwa baada ya abiria wa mwisho kushuka (niko tayari kusahihishwa).
Haijawahi kutokea kwa binadamu aliye huru kula kwa muda wa dk mbili tu na akamaliza, labda wafungwa wa gerezani ambao ulaji wa namna hii ni sehemu ya adhabu kutokana na makosa waliyoyatenda.
Natoa wito kwa mamlaka kuhakikisha abiria wanapewa muda wa kutosha kula na kuchimba dawa ili wasipate matatizo ya kiafya, kwa mtu anayesafiri kwa zaidi ya masaa 15 kutoka Dar hadi Kyela kumshindisha na njaa ni uonevu mkubwa sana, bado hatujachelewa tunaweza kurekebisha.