Abiria wa mabasi ya mikoani hasa Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na Tunduma ni kama wafungwa

Abiria wa mabasi ya mikoani hasa Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na Tunduma ni kama wafungwa

Kilimanjaro dakika anaaza hesabu baada ya abiria wa mwisho kushuka na gari haiondoki mpaka abiria wote wawe wamepanda pia ukiacha Aljazeera Kilimanjaro anakamilisha Restaurant yake mwenyewe, Uwekezaji ni akili Kilimanjaro anawashika soon tu chuma zote zina Vipusa kwanini nipate tabu? View attachment 1273256View attachment 1273257

Kama kweli anajenga atasaidia sana, maana kwa uchafu wa aljazeera Hapana aisee
 
njoo kwenye Abood, full kukimbizana hakuna hata kuingia kwa mgahawa ili asipitwe, zimekua kama daladala, ampiku mwenzake awai ageuze ale vichwa, pambaf sana Abudu
 
Njia ya mwanza dar huwezi fanya ujinga wa namna hiyo
 
Punguzeni ,kulasana usiku wakuamkia safari kingine kilakitu barabarani utakaona stend yeyote unanunua unabaki unabugia tu rod .tumbo lisiume?
Hapo kwenye kula sawa.

Ila jiyo ya kuchimba dawa imekaaje?

Yaani watu wanaugua njiani kiasi cha kutafuta dawa za kuchimba njiani?
 
Panda kilimanjaro anatoa dk 30 mpka 45 hadi watu wanaenda kuoga kabisa
Very true hawa jamaa hadi raha nusu saa kula, nlisafiri nao wiki imepita, halafu hotel yao imekaa fureshiiii hasa pale counter ya vinywaji unaweza sahau kama unasafiri, hahahahaahahah
 
Mkuu usiombe ubwanwe na mkojo na ndo dereva haeleweki yani utaota ndoto za ajabu mara umkojolee dereva, mi nkaambiwa uwe unakaa na chupa ya uhai kweny basi ili uwe unajisevia.
Tupende kujipanga kusafiri na luxury choo ndani for short call, raha kinyama unayumba tuu huku unakojoa, ila usiombe yatokee ya kutokea ukiwa chooni..siombei.
 
Tunahutaji basi zenye choo ndani kwa ajili ya haja ndogo tu,shida ni kwamba basi ikiwa na choo lazipa ipoteze siti 4. Siti 4 ni laki na 60 Kwa trip,ukizidisha mara 10 kwa mwezi then mara 12 ni sawa na kupoteza m16 kwa mwaka.

Vipimo vya urefu wa mabasi tz ni mafupi, tanroads waruhusu basi ndefu kama kusini mwa Africa pamoja na ujazo zaidi wa mizigo kwenye mizani. Matajiri wataleta mabasi bora zaidi.
 
Tangu Scandinavia iondoke barabarani kwa kweli abiria wa njia hii wanasafirishwa kama wafungwa, hakuna utaratibu unaeleweka mkiwa safarini.

Kwa mfano, haieleweki abiria wanakula hoteli gani, wala haijulikani hata abiria anatakiwa kula kwa dakika ngapi, basi inasimama kwenye hotel yoyote ambayo dereva ameahidiwa chakula cha bure, abiria mnatangaziwa kutumia dk 10 tu kula na kuchimba dawa, wakati huo huo abiria wa siti ya nyuma anatumia zaidi ya dk 5 kushuka, maana ni lazima asubiri walio mbele yake washuke kwanza, wakiwemo wagonjwa na wazee ambao hutembea taratibu, Scandinavia ilikuwa inatoa dk 15 ambazo zilianza kuhesabiwa baada ya abiria wa mwisho kushuka (niko tayari kusahihishwa).

Haijawahi kutokea kwa binadamu aliye huru kula kwa muda wa dk mbili tu na akamaliza, labda wafungwa wa gerezani ambao ulaji wa namna hii ni sehemu ya adhabu kutokana na makosa waliyoyatenda.

Natoa wito kwa mamlaka kuhakikisha abiria wanapewa muda wa kutosha kula na kuchimba dawa ili wasipate matatizo ya kiafya, kwa mtu anayesafiri kwa zaidi ya masaa 15 kutoka Dar hadi Kyela kumshindisha na njaa ni uonevu mkubwa sana, bado hatujachelewa tunaweza kurekebisha.
Wewe unafikilia safari ya dar_mbeya_ sumbawanga ya kulinganisha na dar to Arusha eti? Sitaki kusema Sana Kama huna haraka panda bus ambazo hazina haraka inaingia tunduma saa 5 mpaka 6, sumbawanga inaingia saa 8 mpaka saa 9
 
Tangu Scandinavia iondoke barabarani kwa kweli abiria wa njia hii wanasafirishwa kama wafungwa, hakuna utaratibu unaeleweka mkiwa safarini.

Kwa mfano, haieleweki abiria wanakula hoteli gani, wala haijulikani hata abiria anatakiwa kula kwa dakika ngapi, basi inasimama kwenye hotel yoyote ambayo dereva ameahidiwa chakula cha bure, abiria mnatangaziwa kutumia dk 10 tu kula na kuchimba dawa, wakati huo huo abiria wa siti ya nyuma anatumia zaidi ya dk 5 kushuka, maana ni lazima asubiri walio mbele yake washuke kwanza, wakiwemo wagonjwa na wazee ambao hutembea taratibu, Scandinavia ilikuwa inatoa dk 15 ambazo zilianza kuhesabiwa baada ya abiria wa mwisho kushuka (niko tayari kusahihishwa).

Haijawahi kutokea kwa binadamu aliye huru kula kwa muda wa dk mbili tu na akamaliza, labda wafungwa wa gerezani ambao ulaji wa namna hii ni sehemu ya adhabu kutokana na makosa waliyoyatenda.

Natoa wito kwa mamlaka kuhakikisha abiria wanapewa muda wa kutosha kula na kuchimba dawa ili wasipate matatizo ya kiafya, kwa mtu anayesafiri kwa zaidi ya masaa 15 kutoka Dar hadi Kyela kumshindisha na njaa ni uonevu mkubwa sana, bado hatujachelewa tunaweza kurekebisha.


!
!
halafu kuna mtu anakuja anasema selikali haijafanya lolote
 
Nakulaga Heineken pale unakuta zimepoa vizuri sana pale
Very true hawa jamaa hadi raha nusu saa kula, nlisafiri nao wiki imepita, halafu hotel yao imekaa fureshiiii hasa pale counter ya vinywaji unaweza sahau kama unasafiri, hahahahaahahah
 
Back
Top Bottom