Abiria wa mabasi ya mikoani hasa Dar es Salaam, Iringa, Mbeya na Tunduma ni kama wafungwa

Unapenda ma yutong?
Hayo ndio huwa siyapendi kabisa.

Dar express ana mashine za ukweli lakini tatizo pale huduma za kipuuzi sana.

Angetafuta Watu serious na biashara badala ya kujaza cheap labour ambao hata hawajui wanachofanya.
 
Ukitaka kujua mkojo unabanaje panda kisbo...kuacha abiria sio ishu. Gari baya ndani mpka nje ila kuwahi linajitaidi. tusiwalaumu sana hawa watu wa mabasi...abiria wengine wanapenda hayo maisha ya mikiki.
pia,watu wanaofanya Biashara ya mabasi wanafanya kwenye mazingira magumu sana...hivi kweli MTU akutoe dar mpaka mwanza kwa 40,000?mkiongezewa nauli mpate huduma nzuri na magari mazuri, makelele.
mswahili hana jema...
 
Tangu Scandinavia iondoke barabarani kwa kweli abiria wa njia hii wanasafirishwa kama wafungwa, hakuna utaratibu unaeleweka mkiwa safarini.

Kwa mfano, haieleweki abiria wanakula hoteli gani, wala haijulikani hata abiria anatakiwa kula kwa dakika ngapi, basi inasimama kwenye hotel yoyote ambayo dereva ameahidiwa chakula cha bure, abiria mnatangaziwa kutumia dk 10 tu kula na kuchimba dawa, wakati huo huo abiria wa siti ya nyuma anatumia zaidi ya dk 5 kushuka, maana ni lazima asubiri walio mbele yake washuke kwanza, wakiwemo wagonjwa na wazee ambao hutembea taratibu, Scandinavia ilikuwa inatoa dk 15 ambazo zilianza kuhesabiwa baada ya abiria wa mwisho kushuka (niko tayari kusahihishwa).

Haijawahi kutokea kwa binadamu aliye huru kula kwa muda wa dk mbili tu na akamaliza, labda wafungwa wa gerezani ambao ulaji wa namna hii ni sehemu ya adhabu kutokana na makosa waliyoyatenda.

Natoa wito kwa mamlaka kuhakikisha abiria wanapewa muda wa kutosha kula na kuchimba dawa ili wasipate matatizo ya kiafya, kwa mtu anayesafiri kwa zaidi ya masaa 15 kutoka Dar hadi Kyela kumshindisha na njaa ni uonevu mkubwa sana, bado hatujachelewa tunaweza kurekebisha.
hilo basi la kilimanjaro wanakula hotel yao eti robo kuku 8000Tsh,dah nikauliza mara mbilimbili tena broiler,
 
hiyo route ya mbeya hovyo sana..yan ukipanda mabasi ya huko madereva wanapigia simu watu wao walio mbele wawaandalie misosi. nyie abiria wengine mtajijua
 
Hahahaha.... Hii ni kweli, na inaboa kiukweli.
Utashangaa tuu abiria wazoefu wanaletewa package za msosi, nyie wengine hamtaelewa what is happening!!
 
Kwa kweli hili ni tatizo! Mamlaka husika ziingilie kati.
 
Tangu Scandinavia iondoke barabarani kwa kweli abiria wa njia hii wanasafirishwa kama wafungwa, hakuna utaratibu unaeleweka mkiwa safarini.

Kwa mfano, haieleweki abiria wanakula hoteli gani, wala haijulikani hata abiria anatakiwa kula kwa dakika ngapi, basi inasimama kwenye hotel yoyote ambayo dereva ameahidiwa chakula cha bure, abiria mnatangaziwa kutumia dk 10 tu kula na kuchimba dawa, wakati huo huo abiria wa siti ya nyuma anatumia zaidi ya dk 5 kushuka, maana ni lazima asubiri walio mbele yake washuke kwanza, wakiwemo wagonjwa na wazee ambao hutembea taratibu, Scandinavia ilikuwa inatoa dk 15 ambazo zilianza kuhesabiwa baada ya abiria wa mwisho kushuka (niko tayari kusahihishwa).

Haijawahi kutokea kwa binadamu aliye huru kula kwa muda wa dk mbili tu na akamaliza, labda wafungwa wa gerezani ambao ulaji wa namna hii ni sehemu ya adhabu kutokana na makosa waliyoyatenda.

Natoa wito kwa mamlaka kuhakikisha abiria wanapewa muda wa kutosha kula na kuchimba dawa ili wasipate matatizo ya kiafya, kwa mtu anayesafiri kwa zaidi ya masaa 15 kutoka Dar hadi Kyela kumshindisha na njaa ni uonevu mkubwa sana, bado hatujachelewa tunaweza kurekebisha.
Siyo Njia hiyo Tu mkuu. Jaribu Dar_mwanza, Kagera.Mara na Simiyu!! Ole wako upate tumbo la kuharisha ukiwa Safari hizo. Hujamaliza kushusha nguo Dereva keshaondoa Gari wako Barabara I ukiwa msalani. Hawana utu wala Subra. Eti wanawahi kugeuza (kurudi).
 
Aiseeee !!
 
Pia na njia ya kwenda mikoa ya kanda ya ziwa dakika kumi bado ukienda msalani unakuta watu wamejaa maana basi sio moja zaidi ya mawili yaani safari nzima mtu unakojoa mara 2 tu ukizingatia safari inachukua masaa hadi kumi na 6
Mkuu kwani wastani huwa ni kukojoa Mara ngapi kwa safari moja!
 
Back
Top Bottom