Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

Usalama wa Taifa au TRC management/board walikuwa wapi muda wote huo. Bila ku-anticipate kuwa kuna risk ya watu kulipa nauli ya pugu akaenda mpaka Dodoma?
 
Project ilishafeli tayari. Nchi ilishatekwa na wajanja miaka mingi. Sijawahi kuona Basi la Mkoani likitoka Mbezi lipakie abiria wa kibaha. Iweje iwezekane kwenye SGR? Soon tutasikia vichwa vimeenda kufanyiwa ukarabati na ndio itakua mwisho wa Hilo dubwana.
 
Hii nchi ina vituko sana. Nakumbuka walipotoa chati ya nauli miezi kadhaa iliyopita nikawa namsomea dereva wangu tukiwa safarini. Nauli ya Dar hadi pugu.
Deveva wangu alikataa kabisa kuwa mtu anaweza kushukia Pugu. Sasa ndio ushangae kama dereva wa gari tu aliona ni tatizo, hao waliosomea railway management wanaweza wasione? Au ni ujanja tu
 
Hili Taifa kila mtu mwizi. Asipo shika bunduki, atashika kisu, akikosa kisu atashika nondo, akikosa nondo, atashika fatuma, akikosa fatuma atashika bisibisi, akikosa bisibisi ataweka roba ya mbao, akiona yote hayawezi anahamia kalamu, akikosa nafasi ya kalamu anaweka mbogo hapa ndio tunasikia maagizo kutoka juu, kuuza Mafuta na maji ya upako, uganga na urozi, mwisho ikibidi anakuwa hadi chawa ili mladi tu apate kitu ambacho hakustahiki Kwa haki. Akifeli kote anaishia kuhujumu tukose wote.

Ujenzi tu wa uiyo reli watu wameiba sana, cement, nondo, mchanga, Mafuta. Japo juhudi zimefanyika kidhibiti lakini ni shughuli, ndio maana miradi inabidi iwe na bei jui kufidia hasara ya wizi wa waTz.
 
hivi kweli abiria wa pugu anapanda first class na anakunywa na chai, whats the hell, nauli ziwe mbili tu dom na moro, tena, ziwekwe scanner wakati wa kupanda na kushuka ukipitiliza faini lakimoja
 
we ni mshenzi sana, hao wanaoishi pugu daladala hazipo? watu wa daladala wafunge biadhara zao kisa sgr? acheni ujinga kutaka kuua mradi, nauli iwekwe flat rate, kutoka dar hadi moro na dar -dodoma, pia moro-Dodoma

mnaoshukia njiano mfano nyie wa pugu na maeneo mengine njiani mnalipa nauli ile ile ya dar-moro, huwezi kapande daladara utafika tu😠 , serikali wekeni flat rate prices mkitaka kunusuru mradi
 
Ajabu kabisa nimejaribu hapa ni kweli ukikata tiketi ya pugu, siti inakuwa close maana yake mtu akitaka hiyo siti kwenda dom atakosa
 

Attachments

  • Screenshot_20240818-144037_Chrome.jpg
    156.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20240818-144130_Chrome.jpg
    134.1 KB · Views: 2

kwa nini station imejengwa hapo sasa kama haina maana? hata wewe kama hautaki treni isimame Pugu au station yoyote ile ndogo unaweza kupanda abudi au shabibi pia siyo lazima upande treni …
 
kwa nini station imejengwa hapo sasa kama haina maana? hata wewe kama hautaki treni isimame Pugu au station yoyote ile ndogo unaweza kupanda abudi au shabibi pia siyo lazima upande treni …
anza kuzoea tu daladala mkuu kwenda pugu, cas either ulipe nauli ya dar moro then hata ukishuka pugu sawa tu utajua mwenyewe, cas maoni yangu yashapokelewa huko TRC na majibu yamekuja ndio watafanya hivyo cas washaona changamoto iliopo. Bye mkuu rudi barabarani tu kadandie magari ya pugu
 
Nchi wa kifala sana hii.
SGR inatakiwa i set standards zake.
Minimum inatakiwa iwe 10,000. Hata iwe kilomita moja.
Vinginevyo haitaweza kujiendesha.
Bila ya hivyo
 
kwa nini station imejengwa hapo sasa kama haina maana? hata wewe kama hautaki treni isimame Pugu au station yoyote ile ndogo unaweza kupanda abudi au shabibi pia siyo lazima upande treni …
station kujengwa pugu ilikua ni makosa, ila ndo ishajengwa, msijari mtakua mnalipia nauli ya morogoro kwenda hapo pugu kwenu😊
 
You have got a point...
Wenye akili wangeweza kufanya hivi...
1. Kuwe natrain shutle ya kushusha njiani ambayo sio express ya Dar-Moro-Dom.
2. Au waweke behewa moja la watu wa njiani.


However, kupakia watu wa Pugu ni uwendawazimu wa kipekee sana.
 
hawazuii mtu kushuka ila kama unaenda pugu lipa nauli ya moro, nikama kilimanjaro express harakama utashukia chalinze utalipa nauli ya arusha
 
Sio makosa. Inawezekana kuweka behewa la watu wa njiani, au kuwa na train tofauti design ya daladala.

However, kukatia watu ticket za Pungu ni uwendawazimu wa aina yake.
nikupotezeana muda tu, tuache siasa kwenye uchumi treni ya dom kituo cha kwanza kiwe moro then dom. nauli mbili tu moro na dom, lakini naona kuna shida kwenye ticketing system, iweje mtu akate ticket ya pugu na apate seat hadi moro?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…