Abiria wa Pugu anafuata nini kwenye SGR kama sio upigaji

station ya pugu ilikuwa ya kushusha ng'ombe, wakati wa mkoloni pugu ikuwa msituni na iliwekwa pale pia kwa shughuli za kijeshi, kwa sasa haina maana tena, funga hiyo station fullstop
 
We kwenda zako huko! Kuwa na station sio lazima ipakie abiria anaetoka Dar na kwenda Dar! Matumizi mabaya ya raslimali.
 
Dawa ni kila kituo kuweka geti litakalofunguka na abiria kuweza kupita baada ya kuwa amescan tiketi yake. Hiyo itasaidia kuzuia hao wote wababaishaji, kama unalipa nauli ya kuishia Pugu halafu ukaendelea mpaka Moro, ukifika kule manake geti litakataa kukurusu kupita maana tiketi yako ilikuwa ya kuishia Pugu. Matumizi ya teknolojia ndio suluhisho hapo, hakuna hata haj ya walinzi ndani ya mabehewa
 
We kwenda zako huko! Kuwa na station sio lazima ipakie abiria anaetoka Dar na kwenda Dar! Matumizi mabaya ya raslimali.

siyo lazima ndiyo kama mambo yote siyo lazima, hata treni ya umeme inayokwenda 160 km/ h siyo lazima pia, ajabu unaongelea matumizi mabaya ya rasilimali kivipi? kutakuwa na treni ya ya express pia ambayo haitasimama vituo vidogo na kutakuwa na treni nyingine ambayo itasimama kila kituo kilichojengwa kwani watu wa Pugu na kwingineko ni walipa kodi pia …
 
station kujengwa pugu ilikua ni makosa, ila ndo ishajengwa, msijari mtakua mnalipia nauli ya morogoro kwenda hapo pugu kwenu😊

ni makosa kivipi? isitoshe kama ni hivyo kwa nini wa morogiro wasilipie nauli ya dodoma pia kwani treni ya dodoma kusimama morogiro ni makosa pia kwa logic yako …
 

Serikali sijui inafeli wapi ,hao wahuni ni kuwapa kesi ya uhujumu uchumi na wakija kwenye plea bargain unawapiga milioni 100 ili watoke...wakiwafanyia watu 10 huo upuuzi utaisha.
 
Huna akili
 
Ajabu kabisa nimejaribu hapa ni kweli ukikata tiketi ya pugu, siti inakuwa close maana yake mtu akitaka hiyo siti kwenda dom atakosa
Hili sasa ni tatizo la hao watu wa software, ilitakiwa hiyo seat iwe released baada ya abiria huyo kushuka pugu ili abira wa hapo hapo pugu aweze kuninunua tena hiyo seat.
Kwa mtindo huo mtu akiwa na laki anaweza hujumu behewa zima kwa kukata tu tiketi za pugu.
 
Huna akili

wewe mwenye akili nijibu kama ukipenda kwa nini kuna wamejenga station ya treni hapo kwa kutumia mabilioni ya fedha ? na siyo wao tu hata mkoloni pia alipojenga reli aliweka station miji midogo pia ni kwa nini unafikiri au wote hawana akili isipokuwa wewe tu ? maisha siyo kuangalia matakwa yako tu bali ya kila mmoja wetu pia …
 
Wanashindwa kuwa wabunifu. Watengeneza mabehewa ya Abiria wa njiani.

Na kwa treni inayoanzia Dar na kituo cha kwanza kiwe Ruvu siyo Pugu.

Shida tumejaza watu wasiofikira katika hizi Taasisi.
Wewe unafikiri behewa ni kama gari la mabox? Sio haraka hivyo, sema wasitishe huduma kwa vituo vya karibu mpaka hapo baadae watakapopata behewa nyingi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…