Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwakyembe si anakesha hapo kiwanjani..sasa huyu kapitia wapi tena?
halafu mwakyembe anatuletea sanaa za kumakamata ras wa kuchonga ili ionekane ccm wanapambana na madawa.Mwakyembe kamkamate idd azan na ridhiwan nyambaf we.
Kwa mara nyingine, maafisa wa Hong Kong katika kiwanja cha ndege wamefanikiwa kukamata dawa za kulevya zilizokuwa zinasafirishwa kutokea Tanzania safari hii zikiwa zimefichwa katikati ya chuma cha mashine.
Dawa hizo aina ya heroin zilikamatwa katika nyakati mbili tofauti kwa jumla zikiwa na kilo 1.5 na thamani ya dola milioni 1.3 za Marekani.
Maafisa hao wanasema kwa kuwa wamekuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo za wauza dawa na mbinu za kuficha dawa hizo, walilazimika kukikata chuma cha mashine hiyo ili kuziona.
Adhabu ya kupatikana na dawa za kulevya huko Hong Kong ni faini ya dola milioni 5 za Kimarekani.
Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Serikali ya nchi hiyo na picha zinazoambatana na taarifa hiyo vimepachikwa hapo chini.
![]()
![]()
![]()
Wewe ulitaka afanye nini?
Hii machine mbona Kama imechakaa ghafla baada ya kukata hicho Chuma au ilifungwa hapo kwanza kisha kikahamishiwa katika machine nyingine! Tazama kwa umakini hizo picha.