Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Abiria wa Tanzania akamatwa Hong Kong na heroin ikiwa ndani ya mashine

Hili ni janga lingine la kiutawala,mfumo wa utawala serikali hii upo taabani karibu kila nyanja!
 
Hii ni changamoto ya ukweli! inaendelea kudhihilisha ukweli kwamba kuna kiwanda au mtambo wa kutengeneza madawa hayo nchini!

mi nadhan hao jamaa wanaonekana kuwa na nguvu zaidi ya serikali! inatisha.
 
lakini hawa Wachina hawatutendei haki kwanini hawafanya uchunguzi w akutosha?
kila siku wanishia kuwafunga na kukamata mapunda tu, kwanini hawa wafuatilii wanaowatuma mapunda kama marekani wanavyofanya huko MEXICO ?

Hahahah kaka mkubwa nadhani unafahamu kuwa, "Aliyekamatwa na ngozi ndiye mchunaji na pasi na shaka ndiye mchinjaji"

Sheria za China huwa zipo very straight, ukikutwa na kosa utaadhibiwa ili uwe mfano kwa wengine...na kwa hawa hapa wanakutana na adhabu kali ili wengineo wakitumwa kwenda na mzigo huko wafikirie mara mbili mbili...
 
picha mbilii tofautii kabisa,check meno gear ya juu ni 4,na mwisho tofauti.chini nii meno gear 2 na mwisho wa round mbili tofauti,hata kama mashine ya kwanza iligoma ama kushndwa kukatwa na masine hata kufauliishwa kwenye mashine nyengiine mbona kilicho katwa pia ni tofauti?
 
Duh ndo tumefikia hatua hii jamani??? Kazi ipo kulisafisha jina la tanzania kwa staili hii.
 
[h=2]
icon1.png
Mtanzania aliyekamatwa Los Angeles akiri kuingiza heroin Marekani[/h] Mtu aliyetambuliwa kuwa Mtanzania yumo hatarini ya kufungwa miaka 40 jela nchini Marekani baada ya kukamatwa na dawa za kulevya dawa aina ya heroin zikiwa ndani ya kompyuta pakato (laptop).

Shirika la habari la The Associated Press tarehe 15 Agosti 2013 limechapisha habari hiyo na kusema kuwa Mtanzania huyo ametambulika kwa jina la Joseph Mackubi (miaka 33), alikamatwa katika kiwanja cha ndege cha LAX mjini Los Angeles akitokea Nairobi.

Mackubi alipandishwa atika kizimba cha mahakama (Federal court) jijini LA na kusomewa mashitaka siku ya


Jumatano, Agosti 14, 2013 ambapo alikiri kukutwa na dawa hizo zilizokuwa zimefichwa kwenye laptop isiyofanya kazi.

Inaripotiwa kuwa maafisa waligundua uzito usio wa kawaida wa laptop aliyokuwa nayo Mackubi mwezi Oktoba mwaka jana walipompekua. Walipompeleka kumpekua kwa mara ya pili kwa kina zaidi, walijaribu kuwasha komyputa hiyo bila mafanikio, na kugundua kuwa ilikuwa ina alama za kufunguliwa awali (tampered with), na ndipo walipoifungua kabisa ndani ambapo walikuta gramu 800 za heroin zimefichwa.

Mackubi alisema alikuwa akutane na mwanamke anayeishi jimboni Alabama, ambaye walifahamiana kwenye mtandao wa internet. Maafisa wamesema kuwa Watanzania ni miongoni mwa watu wanaokamatwa LAX wakisafirisha dawa za kulevya kwa njia hiyo.

Hukumu impasayo Mackubi imepangwa kutolewa tarehe 11 Septemba


 
Yaani biashara ilivyo changamkiwa tunawazidi hata wanaoizalisha!
 
picha mbilii tofautii kabisa,check meno gear ya juu ni 4,na mwisho tofauti.chini nii meno gear 2 na mwisho wa round mbili tofauti,hata kama mashine ya kwanza iligoma ama kushndwa kukatwa na masine hata kufauliishwa kwenye mashine nyengiine mbona kilicho katwa pia ni tofauti?

Hivi, umeisoma vizuri hiyo PRESS RELEASES? Au kienglish ndo vile?
 
Hii machine mbona Kama imechakaa ghafla baada ya kukata hicho Chuma au ilifungwa hapo kwanza kisha kikahamishiwa katika machine nyingine! Tazama kwa umakini hizo picha.

Hizo mbona ni gear mbili tofauti? Au ni za matukio tofauti? Isije ikawa mambo mengine mipakazo tu. Na je, hao wanaokamatwa ni watanzania kweli? Mwakyembe chunguza hili sakata vizuri tafadhali.

picha mbilii tofautii kabisa,check meno gear ya juu ni 4,na mwisho tofauti.chini nii meno gear 2 na mwisho wa round mbili tofauti,hata kama mashine ya kwanza iligoma ama kushndwa kukatwa na masine hata kufauliishwa kwenye mashine nyengiine mbona kilicho katwa pia ni tofauti?

Mkisoma vizuri hiyo press release ya Hong Kong wanadai kulikuwa na matukio mawili.

Tukio la kwanza lilitokea Agosti 2, 2013 baada ya kushtukia kuwa mashine zinatumika kusafirishia hizo dawa.

Walipoanza kufanya uchunguzi ndiyo wakakutana na tukio la pili lililotokea Agosti 15.

Inawezekana mashine moja ni ya tukio la mwanzo, na mashine nyingine ni ya tukio la pili.

Pia inawezekana moja ya tukio lilikuwa na mashine zaidi ya moja lakini moja ndiyo iliyokuwa na hayo madawa.
 
Badili title yako hamna abiria wa Tanzania hapo si wanasema ilikuwa mzigo unasafirishwa kama parcel ama?
 
Back
Top Bottom