Abiria wafurahia usafiri wa treni Moshi - Dar

Abiria wafurahia usafiri wa treni Moshi - Dar

1575899916373.png


SERIKALI kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuwa kutokana na mwitikio wa wasafiri katika safari mpya ya treni ya abiria kati ya Dar es Salaam – Tanga – Moshi, itaongeza siku za safari pamoja na idadi ya mabehewa.

Aidha, wakazi wanaoishi mikoa ya Kanda ya Kaskazini ikiwamo Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga wamemtaja Rais John Magufuli kuwa ni kiongozi aliyeletwa na Mungu kuwakomboa maskini nchini.

Treni hiyo iliyokuwa imekufa kwa takriban miaka 25, ilianza safari kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi kupitia mkoani Tanga Ijumaa saa 10:00 jioni na ilifika kituo cha mwisho Moshi mkoani Kilimanjaro saa 5:00 asubuhi juzi Jumamosi. Iligeuza siku hiyo jioni na jana ilifika Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya TRC, treni hiyo itakuwa ikifanya safari kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi kila siku za Jumanne na Ijumaa na kuondoka Moshi kila Jumamosi na Jumatano.

Lakini jana akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa meli na chelezo katika ziwa Victoria jijini Mwanza, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema mwitikio wa usafiri huo umekuwa mkubwa na sasa wataongeza siku za kusafiri.

Kamwelwe alisema juzi treni hiyo ilikuwa na mabehewa tisa na ilibeba abiria 420, lakini kumekuwa na mwitikio mkubwa, hivyo kupitia TRC wataongeza safari hasa wakati huu wa msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

“Tunataka sasa kutokana na mwitikio huu treni hii isafiri kila siku, tumeongeza na watu wa TRC ili kuhakikisha safari hii inawezekana,” alisema Kamwelwe.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alisema treni hiyo ilikwama kwa miaka 26 kutokana na kutokuwa na vipaumbele vya matumizi ya fedha, lakini sasa kwa kutumia fedha zinazorejeshwa kutoka kwa mafisadi, treni hiyo na nyingine zitaendelea kukarabatiwa na kujengwa kwa manufaa ya Watanzania.

“Wenzetu hawa kila walipokuwa wakienda Moshi kwenye Krismasi na sikukuu zao tulikuwa tunasikia wanapata ajali…ni miaka 26 sasa treni haijakanyaga Moshi. Miaka 26 haijakanyaga Moshi, kwa Kisukuma tungesema why (kwa nini). Tumeamua kuifufua, mwanzo hatukujipanga. Hatukuwa na vipaumbele kwa fedha za wananchi. Lazima tuseme ukweli,” alieleza Rais Magufuli katika sherehe za jana. Kwa upande wao, wakazi wanaoishi mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga wamesema Rais Magufuli ni kiongozi aliyeletwa na Mungu kuwakomboa binadamu maskini nchini.

Wameyasema hayo juzi wakati wa mapokezi na uzinduzi wa treni ya abiria katika stesheni ya Moshi Mjini baada ya kuwasili mjini humo, wakieleza kuwa Rais Magufuli anawajali wanyonge. Mkazi wa Moshi, Saimon Massawe alisema Rais Magufuli anajali wanyonge nchini Tanzania kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo tofauti na marais wenzake waliopita.

Alisema kitendo cha Rais Magufuli kufufua usafiri wa treni ya abiria mikoa ya Kanda ya Kaskazini ameleta ukombozi mkubwa kwani walipata tabu ya usafiri kwa muda mrefu.

Alieleza kuwa usafiri huo una gharama nafuu tofauti na usafiri wa mabasi ambao bei zake zimekuwa za juu na hivyo watu wengi kushindwa kusafiri kuelekea katika mikoa hiyo hususani wakati wa msimu wa sikukuu.

Mkazi wa Mabogini, Jane Mosha alieleza kuwa ameukubali uongozi wa Rais Magufuli na kwamba ameletwa na Mungu kwa ajili ya kuwakomboa wananchi wa Tanzania ambao ni wanyonge kwa kuleta usafiri wa treni ya abiria.

Aliyataja mazuri yaliyofanywa na Rais Magufuli katika uongozi wake ni kufufua treni hiyo ya abiria, usafiri wa ndege, usafiri wa bahari kwa kupanua bandari, kujenga miundombinu ya barabara, sekta ya afya, maji, kuongeza mitambo ya kufua umeme, kujenga Reli ya Kisasa, kufufua uchumi wa viwanda, kurudisha TTCL, Posta, kuwabana mafisadi, kuwafukuza watumishi wenye vyeti na kubana mishahara hewa na kuongeza ukusanyani mapato.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SOLAR yenye makao yake makuu Dar es Salaam, Abdallah Meta alisema kuanza kwa usafiri huo abiria kutaleta frusa kubwa kwa wananchi wa kipato cha chini kusafiri kwa bei nafuu.
 
Hili linatofautiana nini na lile la juzi
 
Kweli,nimeona tena treni,old moshi sekondari,mawenzi hospitali nani aseme tazama na macho tunayo.
 
TRAIN BUFFET HAKIKA INAKILA KINYWAJI NA JIKO LIKO POA SANA KWA NYAMA CHOMA NA MAYAI YA NYANYA AU SPANISH EGGS,+NDIZI CHOMA HAKIKA CHRISTMAS INAANZIA KWENYE TRAIN SAFI SANA.
 
Nauliza, wakazi wa Marangu na Rombo hiyo treni inawafaa, kulingana na geografia ilivyo. Naomba kufahamishwa. Nilipanda treni hiyo mwaka 1994 nikiwa mdogo so sikumbuki mengi.
 
Nauliza, wakazi wa Marangu na Rombo hiyo treni inawafaa, kulingana na geografia ilivyo. Naomba kufahamishwa. Nilipanda treni hiyo mwaka 1994 nikiwa mdogo so sikumbuki mengi.
Dahhh wabongo bhana ,tusishangae kesho hapa kila mtu akataka treni hii ipite hadi mlangoni kwake ! Guys let's us learn to appreciate a little thing then we will later be awarded big
 
Back
Top Bottom