Abiria wanusurika kifo baada ya kulishwa biskuti zenye dawa za kulevya

Abiria wanusurika kifo baada ya kulishwa biskuti zenye dawa za kulevya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
95628f2c8fb2c1a0b6effa976b518120

Lindi. Abiria wawili waliokuwa wakisafiri na basi la Buti la Zungu kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara nchini Tanzania wamenusurika kifo baada kula biskuti zinazodaiwa kuwa na dawa za kulevya wakiwa ndani ya basi hilo.

Abiria hao ni Dadi Rashid (49) ambaye ni ofisa elimu taaluma Utete wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na Omary Burian (27) mfanyakazi wa bodi ya korosho Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Novemba 27, 2019, Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi, Idrisa Chande amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao jana usiku Jumanne wakiwa hawajitambui na kwamba wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Poudence Proteus amesema amepokea taarifa hiyo na atalizungumzia baada ya uchunguzi kukamilika leo Jumatano.

Chanzo: Mwananchi

======


UPDATES:


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pudenciana Protas amesema tayari wameshawakamata Vijana watatu wanaodaiwa kuwapa Biskuti zinazoaminika kuwa na Dawa za kulevya abiria wawili waliosafiri nao kwenye basi la Buti la Zungu kutoka DSM kuelekea Mtwara na kisha kuwaibia vitu mbalimbali.

Vijana hao wamekamatwa wakiwa kwenye Gesti moja Lindi Mjini na tayari wapo mikononi mwa Polisi wakiendelea kuhojiwa.

"Tumewakuta na Laptop, simu walizoiba kwa abiria, mabegi, nguo za wale abiria, kadi za Bank, vyeti mbalimbali, vitabu na mbaya zaidi waliwavua viatu wale abiria tumewakuta navyo, tumewakuta pia na zile Biskuti zinazoaminika kuwa na Dawa za kulevya" -RPC LIndi

Abiria hao ni Dadi Mohamedi (49) na Omary Burian (27), wote wawili wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi 'Sokoine' kwa matibabu zaidi.
 
Abiria hao ni Dadi Rashid (49) ambaye ni ofisa elimu taaluma Utete wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani
Huwa tunaamini kuwa watoa elimu ndiyo kioo cha jamii, siku zinavyokwenda mambo yanakuwa kinyume chake, suala la kuwa makini na vyakula kwenye mabasi linazungumzwa sana kwenye vyombo mbali mbali vya usafiri for decades now.
 
Au wamefanya kwa makusudi kufanya au kukwepa ishu flani..'any way' Mungu awasaidie wapate afya njema ili waendelee na majukumu ya kulijenga taifa letu.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa anasafiri kutoka Dar-Mbeya 2009 kama kawaida ya wabongo ujirani mwema akapewa biskuti aisee jamaa anasema aliharisha mwanzo mwisho. Kilichofata hapo ni madonda ya tumbo baadae jamaa akawa chizi kabisa na mpaka sasa amekuwa mtu wa clinic kila mwezi.
 
Huwa tunaamini kuwa watoa elimu ndiyo kioo cha jamii, siku zinavyokwenda mambo yanakuwa kinyume chake, suala la kuwa makini na vyakula kwenye mabasi linazungumzwa sana kwenye vyombo mbali mbali vya usafiri for decades now.
Kaka hata ukiwa makini vipi arobaini ikifika lazima likukute haina kukwepa
 
Back
Top Bottom