JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwanahabari mkongwe na Mchambuzi wa siasa Absalom Kibanda amekosoa maamuzi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake 18.
“Ni kweli Mdee na wenzake 18 walikosea. Msingi wa makosa yao ni kupinga ubabe wa kihistoria wa viongozi wenzao na kudai kwao haki kibabe. Ni kweli pia viongozi wakuu CHADEMA waliwahukumu kabla ya vikao. Kosa la kimaadili limetolewa 'hukumu ya kifo'.
“Huu ni ulaji wa kisiasa. CHADEMA inadai haki yake, akina Mdee wanapigania jasho lao. Orodha inaongezeka, hawakuanza na Davidi Kafulila, Zitto Kabwe, Wilbroad Slaa wala Kitila Mkumbo na hawatamaliza na hawa Wanawake 19. Ukishakula nyama ya mtu huachi,” – Kibanda.
Kumbuka kuwa Kibanda ni mmoja wa waandishi wakongwe waliowahi kufanya kazi kwa ukaribu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na walikuwa na ukaribu hata nje ya masuala ya kikazi.
Kibanda aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari ambayo ni mali ya Mbowe, pia Kibanda amewahi kuinia matatizoni mara kadhaa kwa kuikosoa Serikali na kuonekana yupo upande wa CHADEMA, hivyo kwa kauli hiyo ni wazi kuna vitu havipo sawa.
GODBLESS LEMA AMJIBU
Baada ya kauli hiyo, mwanachama mkongwe wa CHADEMA, godbless Lema naye akamjibu kwa kuandika hivi:
"Kama utaendelea KUKAUKIWA nakushauri uende kwa Mwamposa niliambiwa anatoa mafuta ya kuvunja nira ya KUKAUKIWA. Hata hivyo jambo gumu ktk jamii ni pale wazee wenye masharti ya kula wanapo kuwa na njaa kuliko vijana wasio na masharti na diet. Sijui njaa ni nini sasa ?"