Absalom Kibanda awakosoa vikali CHADEMA, asema "Ukishakula nyama ya mtu huachi", Lema amjibu

View attachment 2229699

Mwanahabari mkongwe na Mchambuzi wa siasa Absalom Kibanda amekosoa maamuzi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake 18.

“Ni kweli Mdee na wenzake 18 walikosea. Msingi wa makosa yao ni kupinga ubabe wa kihistoria wa viongozi wenzao na kudai kwao haki kibabe. Ni kweli pia viongozi wakuu CHADEMA waliwahukumu kabla ya vikao. Kosa la kimaadili limetolewa 'hukumu ya kifo'.

“Huu ni ulaji wa kisiasa. CHADEMA inadai haki yake, akina Mdee wanapigania jasho lao. Orodha inaongezeka, hawakuanza na Davidi Kafulila, Zitto Kabwe, Wilbroad Slaa wala Kitila Mkumbo na hawatamaliza na hawa Wanawake 19. Ukishakula nyama ya mtu huachi,” – Kibanda.

Kumbuka kuwa Kibanda ni mmoja wa waandishi wakongwe waliowahi kufanya kazi kwa ukaribu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na walikuwa na ukaribu hata nje ya masuala ya kikazi.

Kibanda aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari ambayo ni mali ya Mbowe, pia Kibanda amewahi kuinia matatizoni mara kadhaa kwa kuikosoa Serikali na kuonekana yupo upande wa CHADEMA, hivyo kwa kauli hiyo ni wazi kuna vitu havipo sawa.

GODBLESS LEMA AMJIBU
Baada ya kauli hiyo, mwanachama mkongwe wa CHADEMA, godbless Lema naye akamjibu kwa kuandika hivi:

"Kama utaendelea KUKAUKIWA nakushauri uende kwa Mwamposa niliambiwa anatoa mafuta ya kuvunja nira ya KUKAUKIWA. Hata hivyo jambo gumu ktk jamii ni pale wazee wenye masharti ya kula wanapo kuwa na njaa kuliko vijana wasio na masharti na diet. Sijui njaa ni nini sasa ?"
Karma
 
Forgery is a criminal offence na inahitaji forensic investigation. Hivyo mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika kuhusiana na hizo hand writing na kugundulika ni forged then we will be in the good position kusema wamefoji ila kwa wakati huu hatuna evidence za kusema walifoji. Tuwatendee haki pia hao wakina mama!

Nimecheka, unaambiwa fomu zinatakiwa kujazwa na katibu mkuu, hadi leo ziko ofisini hazijajazwa. Ww unasema hadi upate udhibitisho wa forgery!
 
Forgery is a criminal offence na inahitaji forensic investigation. Hivyo mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika kuhusiana na hizo hand writing na kugundulika ni forged then we will be in the good position kusema wamefoji ila kwa wakati huu hatuna evidence za kusema walifoji. Tuwatendee haki pia hao wakina mama!
Kama idadi ya form toka Tume zipo zote kwa katibu mkuu wa chama hizo zilizorudishwa zilitoka wapi?
 
Wanaodai wabunge hao waligushi nyaraka kwa Nini CHADEMA hawakuwabuluza mahakamani kwa kosa hilo na badala yake wachukue mkondo waloeenda nao?
 
Maza kashammaliza huyu jamaa...kumbe ni mzee wa vibomu bomu ha ha ha mzee wa mizinga

Kibandaaaa !!! Kwishaa
 
View attachment 2229699

Mwanahabari mkongwe na Mchambuzi wa siasa Absalom Kibanda amekosoa maamuzi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake 18.

“Ni kweli Mdee na wenzake 18 walikosea. Msingi wa makosa yao ni kupinga ubabe wa kihistoria wa viongozi wenzao na kudai kwao haki kibabe. Ni kweli pia viongozi wakuu CHADEMA waliwahukumu kabla ya vikao. Kosa la kimaadili limetolewa 'hukumu ya kifo'.

“Huu ni ulaji wa kisiasa. CHADEMA inadai haki yake, akina Mdee wanapigania jasho lao. Orodha inaongezeka, hawakuanza na Davidi Kafulila, Zitto Kabwe, Wilbroad Slaa wala Kitila Mkumbo na hawatamaliza na hawa Wanawake 19. Ukishakula nyama ya mtu huachi,” – Kibanda.

Kumbuka kuwa Kibanda ni mmoja wa waandishi wakongwe waliowahi kufanya kazi kwa ukaribu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na walikuwa na ukaribu hata nje ya masuala ya kikazi.

Kibanda aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari ambayo ni mali ya Mbowe, pia Kibanda amewahi kuinia matatizoni mara kadhaa kwa kuikosoa Serikali na kuonekana yupo upande wa CHADEMA, hivyo kwa kauli hiyo ni wazi kuna vitu havipo sawa.

GODBLESS LEMA AMJIBU
Baada ya kauli hiyo, mwanachama mkongwe wa CHADEMA, godbless Lema naye akamjibu kwa kuandika hivi:

"Kama utaendelea KUKAUKIWA nakushauri uende kwa Mwamposa niliambiwa anatoa mafuta ya kuvunja nira ya KUKAUKIWA. Hata hivyo jambo gumu ktk jamii ni pale wazee wenye masharti ya kula wanapo kuwa na njaa kuliko vijana wasio na masharti na diet. Sijui njaa ni nini sasa ?"
Kibanda amepitwa na Wakati , Hana hoja
 
Kwa hiyo ni haki yao kufoji nyaraka ili mradi kupinga matumizi ya nguvu kudai haki?
Hii nchi ikija kupata maendeleo hata angalau kuwafikia Kenya basi ujue Mungu amekufa.
Nchi ina akili takataka sana.
Kama zako na wanao

USSR
 
Huu ni mtazamo wa mwandishi wetu, ila naona kakurupuka hajapata habari ya kilichojirai labda au anawakilisha mtazamo na shinikizo toka kwa kundi jingine, Uandishi unalipa umenikumbusha gazeti la Suns la uingereza. Unapeleka habari za uongo wanaipima je tunaemtuhumu akienda mahakamani kudai fidia atalipwa nini, je sisi tutaweza kulipa kwa kuuza hii habari? wakiona inalipa wapanda nayo hewani. Ukienda mahakamani wakuwekea mawakili wajuzi wa kupangua hoja utapambana nao hata wakishidwa wanakulipa na wao wantengenea faida yao.
 
Hahahahahahahahaahahaha.....
Aiseh!!
Vijana wa mbowe ni kiboko,kwa matusi tu..
 
Hii nchi ina watu wanafiki sana, washabiki wa siasa chafu, wajipendekezaji na tabia nyingine kama hizo. Cha labda angeanza kwa kuuleza umma mchakato wa uteuzi wa hao 19 uliendeshwaje, halafu ajiulize na kujijibu kuhusu uhalali wa wao kuwa wawakilishi wa chama chao ambacho kimeshawafukuza na kisheria chama chako kikishakufukuza na ubunge wako unakoma.
 
Back
Top Bottom