Mbona Kibanda ameandika kwa mihemko sana?
Anaposema; "Ni wazi kuwa viongozi wa Chadema waliwahukumu kabla ya vikao" anamaanisha nini?
Vile vikao vya KK na baadae Baraza Kuu hakuviona?
Ajabu Kibanda anazungumzia haki ya kina Mdee, haki ipi, ya kufoji? au ya mtu kuchomolewa gerezani kimya kimya usiku? Hawa waandishi na njaa zao wanataka tuwe na taifa lisiloheshimu sheria.
Sasa naanza kuamini, kuna kundi la waandishi wa habari [ wakujitegemea na wa vyombo mbalimbali] wamenunuliwa na serikali ili kuichafua Chadema, kwa kuwatetea wale wahuni 19 bungeni.
Yule wa kwanza ameshajulikana yupo humu ndani, huyu Kibanda ni wa pili, tusubiri wa tatu, wanne, .....
Samia na serikali yake ni corrupt, kuwalipa wale wahuni posho na mishahara kule bungeni, na kuwapa posho hawa waandishi njaa kueneza uzushi.Mbowe jitoe kwenye meza ya mazungumzo.