Kwa kuwa kuna uhuru wa habari waache amuandike kisha kupiti kitabu hicho tayari tutajua nyanya ni ipi na nyanya tonle ni zipi,toka hapo basi itakuwa kazi lahisi sana mbinu mpya ya kuwanyonga mafisadi itakuwa imepatikana.
Wale wote wanaompinga kibanda kama kwa kutumwa au si kutumwa ,kama ni kwa hiari au si hiari, kama ni kwa kulipwa au si kwa kulipwa yote bado ni heri tupu,kwa kuwa tutajifunza jambo au mambo ambayo yanalikabili Taifa kama
1: Ukweli kiasi, ukweli Mwingi,Uongo au uchonganishi ambao unaweza kuwa ni wa upande wa Mh Sita au wa Mafisadi au wa Wengineo wengi ndani na Nje ya Serikali,kwa kuwa yeye kama Mhandishi atakuwa na chanzo [Source] ya taarifa zake na kuwa ili yathibitishwe na wahusika au kukanushwa na wahusika au Kibanda mwenyewe.Kwa kuwa huko mbele ya haki mikononi mwa Watanzania kitakuwa ni Kitanzi cha yeye Mwenyewe Kibanda au Sita au Mafisadi au Wapiganaji wa Ufisadi,kwa kutegemea Ukweli [Reality] ambao jamii itaupima kupitia kitabu hicho.
2: Kitatusaidia kujua Nguvu za Mafisadi kifedha,kupitia uwezo wa upatikanaji wa vitabu hivyo kwa kuwa Watanzania wanajua uwezo wa kifedha wa Absolum Kibanda,wengi wetu tunajua Msemakweli alipotoa kitabu chake cha Mafisadi wa Elimu kimemchukua muda kufika kwa umma kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.Hivyo upatikanaji mkubwa wa vitabu hivyo kwa wnye akili zao itabidi waajue nyuma ya pazia [Who is a Big Shark behind it]
3: Kitatusaida kujua nani na nani wa kutiwa kitanzi pindi ukweli wa Taifa utakapokuwa ,Manake Mapinduzi ya umma ya Morocco yamewezesha kujua kumbe mjane wa Yassel Alafat kwa kushirikiana na Mke wa Rais wa Morroco wameifisadi Morocco kwa mgongo wa Rais.
4: Tutakuwaa tumeongeza ufahamu wa chachu, chungu na tamu ya UFISADI wa Taifa letu na hivyo kuongeza KASI NA HAMU YA WATANZANIA KUONYESHA HISIA ZA KUTAKA KUCHUKUA SERIKALI YAO,NA HIVYO KULIFANYA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA [JWTZ] KUCHUKUA HATAMU KABLA MAMBO HAYAJAHARIBIKA.Kwa kuwa JWTZ ndio chombo cha Umma pekee kilichobaki chenye uhalali wa Kuwavusha Watanzania Kwenye Kipindi hiki cha Mpito.
5: Kwa hayo machache yatakayokuwemo ndani ya kitabu tayari tutakuwa tumepata hata kumbukumbu kama ni ya uchonganishi, uongo, ukweli, ya kuyumbisha Ukweli,au ya Kuficha Ukweli,tayari tutakuwa na mhuri.
Muache aje!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ni Mtanzania ana haki yake,Ukweli wa Mbivu tutaujua