Absalom Kibanda: Kilichobaki ni Kuandika kitabu cha Maovu yako Samwel Sitta!

Mkuu kama haujui Kibanda yupo kwenye payroll ya Lowasa mpango wa kumshambulia Sita ni maagizo ya Lowasa! Kama anaandika vitabu vya mafisadi kwanin aanze na Sita na siyo wale ambao wamejulikana tangu mwanzo?

Sisi haituhusu yupo kwenye payroll ya nani! tunachotaka ufisadi wa Sitta uanikwe then wewe utaandika kuhusu mafisadi amabo wamejulikana tangu mwanzo au vipi?
 

Mzee Kipara, you are the one who needs the book more than anything to know who is Sitta! Sitta cannot be separated from RACHEL, he might be even worse bse he has been investing in people's mind and deceiving them by singing their song and dancing to their rythm! Once you know the true colours of him you will speak differently! take my word bro!
 

Haaa! na wewe ulikuwa wapi siku zote hizo ndio leo unasema utatoa series za Kibanda? ndio walewale!!!! Kibanda mlipue Sitta...muanike usiogope kelele za mlango! By the way hata Kibanda ana haki ya kutoa maoni yake Kikatiba, au umesahau kuwa hata yeye ni Mtz ana haki hiyo Kikatiba? Watu mmedata nyie!
 
It is very cumbersome to believe this at the moment. Many Tanzanians believe that Mr. Six is clean and is in the front seat fighting against UFISADI. I am anxiously looking foward to see what the book will tell us about Mr. Six's other side. Something that I should remind Kibanda is that the book MUST be enclosed with undisputable evidence. Short of that, it will be a little bit difficult to differentiate it with UDAKU newspepers.
 

Kibanda hajajichanganya popote, wewe ndio umejichanganya! Maelezo ya Kibanda hapo juu yamekaa sawa kabisa. Usuri ni kuwa maneno mleta hoja aliyomlisha kinywani amayakanusha, kuwa hamlengi Sitta kama Sitta bali ugomvi wake upo pale anapojipambanua kama mpinga mafisadi, kitu ambacho ni fake! Sitta ni mnafiki unless abadili tabia yake ndipo na jina litabadilika.
 

Hawamjuwi Sitta hawa, waambie kaka!
 
 
Mimi naona ni rahisi sana kuandika ufisadi wa EL na RA kuliko kuandika habari za ufisadi wa SS. Ukimaliza kuandika habari za SS naamini utahamia kwa hao wengine.
 
Kwanini alizima sakata la Richmond kihuni? Wacha achambuliwe kama karanga. Yeye na EL,RA,AC na wengine ni janga la kitaifa, hata ikibidi kuuwawa wauawe tu hawana faida yoyote kwa nchi yetu.

Lingeendelewa kujadiliwa,Kikwete asingekuwepo madarakani...watu mnabaki Lowasa , lowasa...!!! Lowasa , jk na wengine wengi wangeondoka
 
Kwa kweli mimi binafsi uwa simuelewi Sitta, anapigania nini serikalini
 
Kwa kweli mimi binafsi uwa simuelewi Sitta, anapigania nini serikalini

Tutajieni ufisadi wa sitta na amenufaika nao vipi ndio tutawaelewa mnaotaka kumlinganisha sitta na mafisadi papa....tutajieni tu tuko tayari na yeye kumwambia apime uzito wa shutuma zinazomkabili ambazo zinahusisha yeye kwa kujinufaisha kwa kutumia nafasi yake mtakazo tumwagia hapa,kama mtu aliweza kupewa 10% akiwa nje ya nchi akampigia simu baba wa taifa mwl nyerere kumuuliza na nyerere kumruhusu achukue hizo fedha aje azikabidhi serikalini nyie mnaongea nini,wengi wenu ni watoto wa juzi hamuyajui haya msiingie kichwa kichwa kucheza ngoma msiyoijua,nani anaweza kupewa 10% hapa tena kwa kuwekewa kwenye account yake nje ya nchi akapiga simu kumuuliza bosi wake,sokoine mwenyewe hakuwahi kufanya hivyo!!!mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,kumlinganisha Sitta na Ngonyani Lowassa na genge lake ni sawa kulinganisha kifo na usingizi kisha ukadai viko sawa,hata mtoto wako wa chekechekea atakushangaa sema atashindwa kukwambia tu kwamba baba naona umeanza kuchanganyikiwa nadhani malaria imepanda kichwani.
 
Lingeendelewa kujadiliwa,Kikwete asingekuwepo madarakani...watu mnabaki Lowasa , lowasa...!!! Lowasa , jk na wengine wengi wangeondoka

..JK angeondolewa na Bunge ambalo zaidi ya 90% ya Wabunge wake walikuwa ni wa CCM?haupo serious..

Sitta aliupeleka mjadala ule mpaka pale alipoweza kuufikisha, hatua ya kwenda mbele zaidi ilipaswa ifanywe kwa msaada wa pressure ya umma, na bahati mbaya sana wakati vitendo vinapohitajika tunajificha nyuma ya PC, na pale jambo linaposhindwa tunatoa maneno mengi ya kuwalaumu tena wale waliojitahidi kadri walivyoweza.

Naikumbuka busara ya Mwalimu "Kuwa na akili ni pamoja na kujua jambo unaloliweza na lile usiloliweza", na kwenye mjadala wa Richmond,pale ndipo Sitta alipoishia, kama ulitegemea zaidi ya alichokifanya basi uliishi zaidi kwenye ndoto kuliko uhalisia.

Naamini kama wakati ungerudi nyuma, Augustino Lyatonga Mrema asingeuchukua uamuzi aliouchukua 1995, Watanzania wengi ni wanafiki, wanapiga sana domo lakini hawapo tayari kabisa kubeba gharama za ukombozi, na mwelekeo huu bado upo sana kwenye fikra za kinafiki zilizojaa kwenye jamii yetu.
 

Kama wali side na mafisadi, mbona mafisadi haohao walipanga njama za kuhakikisha sita harudi kwenye uspika? Narudia tena kwamba sikufurahishwa na sita kufunga mjadala wa richmond, lakini aliuruhusu hadi lowasa kujiuzuru, na hakuna katika historia ya bunge la tanzania spika aliyewahi kufanya hilo. Kisa tu anapinga dowans isilipwe ndo ameshakuwa adui namba moja wa tanzania? Nyie watu kama hamjanunuliwa nendeni mkapime akili, na ndo maana tanzania hatuataendelea kamwe pamoja na kuwa na raslimali nyingi.
 

Sasa huo ndo unafiki, kama unajua madhambi yake kwa nini usiyataje hapa? At least wengine wamesema alifunga mjadala wa richmond, alijenga ofisi ya spika bungeni, anaendelea kukaa kwenye nyumba ya spika etc.
 
Watu wengine mnakurupuka tu kumwandama Kibanda. Hamjui chanzo chake ni Sitta kuliandama Tanzania Daima na MwanaHalisi kwamba wamenunuliwa. Kwa mujibu wa Sitta kwenye dakika 45 za ITV alitaka magazeti yambebe kama Mpambanaji wa ufisadi. Baada ya shutuma hizi Kibanda laindika kwenye safu yake Tuendako kwamba Sitta sio msafi na kwamba hiyo vita ya ufisadi ni agenda iliyotekwa tu kutoka kwa Chadema
 
Kwa hiyo mnasema kibanda anafanya kazi na Mbowe na CDM then amenunuliwa na akina RA, EL..sasa hapa mnaninchanganya mnataka kusema hawa wote ni wamoja au wana adui mmoja inabidi washirikiane au kibanda anakula huku n kule, wallah! kweli ni mazingira ya biashara huria haya
 
umetueleza stori nzuri ila hujasema unamchukuliaje SITTA???
 

Hii dhana ya eti "vita dhidi ya ufisadi na mafisadi imetekwa" mi hata siielewi kiukweli,mi nilidhani hii ni vita ambayo kila mwenye uzalendo na nchi hii anapaswa kuishiriki bila kujali imaeanzishwa na nani,ni kweli pengine inaweza ikawa imeanzishwa na CDM sawa,lakini hiyo bado haimzuii tlp,cuf,ama ccm yeyote mwenye uchungu na rasilimali za nchi hii kuamua kuingia na kuongeza nguvu za mapambano,ndicho alichokifanya sitta,baada ya chadema kuianzisha nayeye akaiunga mkono moja kwa moja ndio maana akawa kipenzi cha wanachadema na upinzani kiujumla,na alifanya kazi vizuri sana akiwa spika kushirikiana na cdm katika vita dhidi ya ufisadi na mafisadi,na matunda tuliyaona pale kinara wa ufisadi nchi "alipopima" uzito wa tuhuma nzito juu na kuamua kufanya "maamuzi magumu" ya kuachia uwaziri mkuu licha ya kupewa nafasi ya kujitetea akaishia kujiuzulu kwa aibu mbele ya mkewe pale dodoma!Je niwaulize sitta "asingeiteka" hiyo ajenda na kushiriakiana na cdm na wabunge wengine wazalendo wa ccm Mzee wa kufanya maamuzi magumu si mpaka leo angekua bado anatutafuna!sitta na wapiganaji wengine wa ufisadi bila kujali vyama ni watu muhimu sana kwenye hii vita.
 
umetueleza stori nzuri ila hujasema unamchukuliaje SITTA???

Namchukulia kama mpambanaji wa ufisadi asiyechoka wala kukata tamaa kama wenzake kina kibanda na kubenea ambao wamekata tamaa ya kupambana na ufisadi pamoja na mafisadi na kuamua kujiunga nao!pamoja na vizingiti na hujuma kibao za ndani ya chama chake dhidi ya vita ya ufisadi bado kasimama kwenye mstari licha ya kupewa uwaziri ili kumnyamazisha lakini hanyamazi,umewahi kumuona mtanzania wa aina hiyo hivi karibuni?kuna watu hapa wamenunuliwa corolla tu mnaona walivyobadilika!
 

Haa ha ha...na huu ndio ujumbe wa leo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…