twende mbele turudi nyuma, SITTA NI MNAFIKI!!!
1)Kwenye vikao vya bunge wakati akiwa spika, ni mara ngapi dr Slaa alikuwa akiomba kuzungumzi au kuomba ufanyike uchunguzi juu ya malipo yaliyofanywa kwenye kagoda, tangold, meremeta etc? je spika sitta alikuwa akimpa huo uhuru? mara ngapi alikuwa akimkatiza?je hapa sitta kama yeye mpambanaji kwa nini alikuwa akiwazuia wapinzani wasiseme maneno mengine ?
2)spika siita, kwenye bunge hili la bajeti mwezi julai 2011, amewaponda wapinzani kwa kuwaita wanafiki kwa sababu wamekataa kupokea posho, mimi nilitaraji angeunga mkono hoja hiyo ili posho zile zikasaidie kutatua matatizo ya wananchi
3)sitta, aliongoza bunge limfukuze zitto kabwe mwaka 2007 alipozungumzia mkataba wa buzwagi, mbona baadae ilikuja dhihirika kuwa wao sitta na ccm yake ndo wanafiki?
4)sitta, alienda kujenga ofisi ya spika jimboni kwake urambo, huo ni wizi!!!na ni matumizi mabaya ya pesa za umma!!! tangu lini ofisi ya spika ikajengwa jimboni????? kwani yeye angekuwa spika au mbunge milele?kwani mbunge atakaemrithi nae atakuwa spika???
5)sitta hana adabu, analalamika kuwa mafisadi wamemtoa kwenye uspika, so inamaana spika aliyewekwa amewekwa na mafisadi? hiyo ni kauli mbaya dhidi ya kiongozi wako, maana naamini spika ni kiongozi kwa sitta kwa sasa
6)sitta ana skendo nyingi zilizoandikwa mwaka 2008, kuhusu vimada wake, malipo hewa ya madawa, lugha za ubabe na dharau, na habari hizo ziliandikwa na tanzania daima mwaka 2008, so hawa daima wamenunuliwa leo au wamenunuliwa toka 2008?kama wamenunuliwa toka kipindi hicho, hivi freeman mbowe(mmiliki wa tanzania daima/mwenyekiti CHADEMA) anawezaje kukaa na mhariri aliyenunuliwa miaka yote hiyo?basi kama mbowe anamlea halikadhalika MBOWE NAYE KANUNULIWA!!!!!
7)Kila siku mimi hujiuliza, iweje hawa watu waiponde CCM ilhali wamo humohumo? kwa nini wasitoke kama hawaridhishwi na mwenendo wake?bila shaka hawatoki kwa sababu na wao wanafaidika na serikali hii ya CCM!!sasa kubaki humo huo ni undumilakuwili na unafiki wa hali ya juu!
8)unafiki wake mwingine ni kukanusha kwake kujiunga au kuanzisha CCJ, aliyetoa madai ni fred mpendazoe, mbona hampingi mpendazoe badala yake ana wakimbilia daima walioripoti? tatizo wana-sihasa wetu wanapenda kuandikwa in a positive way, wakiandikwa mabaya yao wanakurupuka wanasingizia umetumwa!! hivi kila mtu katumwa basi sasa!
lakini ukweli na yaliyo moyoni watu wanayajua wenyewe, maana sie twafanya kusikia hayo maugomvi yote ni hasira na chuki za kukosa vyeo na dili tu wala hakuna jingine, watu walitaraji wangekuwa mawaziri wakuu 2005 wakatoswa basi wakaanza chuki , haya wengine walikuja na dili yao ya umeme wa upepo huko singida, ilipokosa dili, wakateuana wakaja kwenye richmond kumalizia hasira!!
tanzanoia zaidi ya uijuavyo! wanafiki wamejaa kila kona na watu wamejificha kwa ngozi za kondoo kumbe ni mambwa mwitu makubwa!