Waanzilishi wa JF na Moderators,
Nina ushauri ninataka niutoe kwenu leo, nimejiunga na JF tangu mwaka 2008 na mambo yalikuwa yanakwenda sawa ni hivi karibuni tu baada ya kuibuka wimbi la vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha nne kwa kuchora mazombie ndipo uchangiaji wa mada hata kwa masuala nyeti umekuwa ni wa mzaha, matusi na hoja dhaifu zisizokuwa na mashiko, haiwezekani habari ya kushtusha, kusikitisha, kuhuzunisha na kughadhabisha kama hii baadhi ya watu waandike mambo ya hovyo hovyo kama haya.
Nionavyo mimi ni kuwa perception za baadhi ya watu kuhusu JF kwa ujumla ni kwamba hii ni forum ya recreation kwa ujumla wake na hivyo unapokuwa umechoka basi unarelax kwa kuja huku na kufanya mzaha ( Ninaelewa yapo majukwaa ya mizaha lakini yapo mengine ambayo sio ya mizaa mathalani JF Doctor, Habari za Kisiasa, Jamii Intelligence n.k)
USHAURI WANGU:
Futeni membership zote JF na watu wajiandikishe tena lakini this time kwa kutoa kamtihani fulani hivi cha kutest IQ za wanaotaka kujiunga. Imenisikitisha sana tukio kama hili na mengine kama haya yaliyowahi kutokea then watu wanacomment mzaha, mbaya zaidi unakuta wengi ni vijana wenzangu ambao walitakiwa wawe smart kwenye kufikiria, kuongea, kuandika na hata kutenda kila jambo.