Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Katika mambo kama haya ndipo ama werevu au ujinga wa Watanzania walio wengi unapoweza kupimwa.

Kwanza binafsi nichukue fursa hii kumpongeza sana Absalom Kibanda kwa kuwa katika hili Kibanda amedhihirishia uma kuwa anachoheshimu yeye ni uhuru wake wa kusema yale anayoyaamini lakini vile vile yeye hayuko confined ndani ya box i.e si mtu wa kupewa ama wa kushurutishwa kuandika yale ambay yeye hataki au haoni haja, tija, na mantiki ya kuyaandika. Kwa maana nyingine nyepesi ni kwamba Kibanda anaheshimu TAALUMA yake na kaonesha kuwa kapikika kitaaluma.

Ila sisi Watanzania mi nadhani huu ushabiki na ujinga tunaojijengea kwamba kunya anye kuku akinya bata kaarisha utatugarimu vibaya mno. Yani hatuna hoja hatuna sababu ya msingi bali tunasimamia ushabiki na ile dhana kwamba kwa kuwa huyu yuko Uhuru ama Tz Daima basi anapaswa siku zote kuandika mema tu ya ule mrengo tunaoutaka sisi. Kwangu huu ni ubatili na upuuzi zaidi ya upuuzi wenyewe.

Kibanda kaelezea anavyomfahamu Abdulrahman kuanzia Jeshini, Uwaziri, mpaka alivyoendesha Kampeni za CCM na namna ambavyo yeye alikutana na kuzungumza na Kinana kwa mara ya kwanza. Hivyo kwa ufupi Kibanda anasema haya anayoyaandika ameshayafanyie tafiti hivyo ana haki kimsingi kuyasema na jamii ijue.

Sasa sisi wengine tafiti hatujawahi kufanya huyo Kinana mnamfahamu tu kwa kumsikia kwa watu wengine hasa wale ambao tunawaona kama Miungu yetu ambao wao wakisema basi nasi tunasujudia yale waliyoyasema na hatuna kazi ya kujiridhisha juu ya hayo waliyoyasema huu kwangu bado ni ulofa na uvivu wa kutafuta ukweli na kushabikia ujinga.

Watanzani ifikie mahali turidhike na tukubaliane kutokubaliana manake haitatokea siku sote tufanane kimtazamo, kifikra, kimawazo na hata kiitikadi haiwezekani utake Kibanda aseme yale ambayo wewe unataka ayasema. Mijitu mingine mko na elimu ya kutosha lakini bado tu mnadhalilisha hata hicho mlicho nacho. Kweli nimeamini kwenye msafara wa Mamba...............

Narudi tena Kibanda kwa namna alivyoandika hili kajipambanua kuwa yeye hayuko ndani ya box bali mawazo yake na fikra zake ziko kitaaluma zaidi. Wewe ujuaye tofauti na Kibanda weka yako nawe humu na si kumshambulia kijinga namna hii. Tunadhani na kuamini kuwa anachopaswa Kibanda ni kutupia mawe CCM, Serikali yake na Viongozi wake basi akienda kinyume hapo basi kakosea. Huu si uungwana kwangu huu utadndelea kubakI kuwa ulofa, upuuzi, ujinga, na kufilisika kimtazamo na kifikra na ni udhalilishaji wa mtu mwenyewe.

Eti Kibanda kanunuliwa guyz!!!!! Aibu kwenu; jipangeni kuheshimu fikra na mawazo ya wengine katika njanya zote iwe hasi ama chanya na tusiendelee kutamani kusikia yake tuyapendayo tu bali hata yale tusiyoyapenda. Kimsingi tujiamini na tuwe na uwezo wa kujibu na kupambanua yote...... Manake kama tukiendelee kuutendea hivi huu mti mbichi ule mkavu je???

Kibanda sina shaka hata kidogo na wewe pamoja na uwezo wako wengine umekuwa ukitugonga sana kuoita maelezo ila tumeendelea kutambua kuwa hatuna budi kutofautiana hivyo na vile vile kuheshimu tofauti hizo manake huo ndio uhuru wenyewe. Hivyo kwa hili umezidi kudhihirisha wewe ni kiwango cha namna gani.

Haihitaji uwe na Phd ama uwe Pro kujua na kuamini haya aliyoyasema Absalom Kibanda "Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete"

Absalom Kibanda critics are our friends........ Aluta continue
 
we pompo do you think females are rubbish? please apologise, kila male anayemess anafananishwa na female? tunakusamehe bure
Apology
:majani7: Nyie ndio mama, nami!nisamehewe bure :majani7:
 

Kibanda ni fisadi kama hamjui kibanda tayari amesain mkabtaba na kampuni ya new habari ya mtanzania rai anakuwa maneging group editor
 
Waungwana, mimi naona makala ya Kibanda ina mambo mawili makubwa, la kwanza kwamba yeye anamkubali sana kinana kiasi cha kwamba kwa mjibu wa yeye anaona sasa muda wa CCM kurudi kwenye hadhi yake umefika. Anamkubali kiasi kwamba eti alistaafu jeshini mwaka 1972 baada ya kutumikia jeshi kwa miaka 20?? Ina maana kinana alijiunga jeshini mwaka 1953 au hesabu zinanishinda hapo? La pili ambalo nami nalikubali kwa kiasi fulani ni kwamba tofauti na mtangulizi wake Mukama kinana anauwezo wa kujieleza na anaweza hata akashiriki mijadala ya kisoma na akajenga hoja na kueleweka. Nadhani kibanda anasema between za line kuwa Kinana anauwezo mkubwa sana kuiba kura kwa kutumia mbinu zake za kijeshi na hivyo ni hatari kwa wapinzani ambao watashinda ila kinana anaweza kuwa kikwazo cha kukubali kukabidhi nchi kwa amani.
Anachokisahau Kibanda ni kuwa wakati ni ukuta ukifika umefika, hata ufanyaje, vijana wa leo ambao ndiyo wapiga kura wengi hoja zao hazijibiwi majukwaani ila kwenye matendo na watendaji. Mfano kwenye kata yetu, sisi baada ya kuona unyanyasaji wa mtendaji wa kata na kushabikiwa kwake na diwani tukasema CCM hatuwapi tena udiwani hapa. Tukafanya uchaguzi CDM wakachukua, Mungu si Athman na mtendaji wakamhamisha. Sasa kata zingine nao wakisema shule zetu mbovu, wengine wakasema vituo vya Afya havina dawa wala dawa, wengine wakasema nauli kubwa mno na wengine wakaseama manyanyaso ya wawekezaji yamezidi, kwa pamoja wakaamua kupigia upinzani, kinana atakuwa na ujanja gani hapo? Hili sio suala la mtu mmoja ni la timu nzima
 

Acha siasa za makengeza wewe Mwita Maranya, hivi hunajua kuwa mke mkubwa wa Dr Slaa, Mama Rose Kamili Slaa, kafungua kesi mahamakani kumshtaki Dr Slaa kwa kutelekeza familia mke pamoja na watoto wake anadaiwa fidia ya milioni 150.

CC.. chama,
 
Last edited by a moderator:

Tatizo kubwa la makala ya Kibanda linaanza na hicho ulichokiandika hapo juu. Kama kweli kafanya utafiti wake kuhusu Kinana ndiyo alipaswa kuuweka kwenye andishi lake lakini hajafanya hivyo.Badala yake ameishia kutaja vyeo alivyowahi kushika Kinana na kuvihusisha na kaburi la upinzani nchini. Kwa ujumla ametoa profile ya Kinana tu ambayo kila mtu anaifahamu. Pili, Kibanda anauona ufisadi kama si tatizo, hoja dhaifu na isiyo na mashiko.
 
haya ayawi ayawi sasa yamekuwa makala ya kibanda kuhusu kinana alikuwa anajua nn anafanya sasa saizi anakuja kufanya kazi new habari kwa rostam aziz na inasemekana mzee lowasa kainunua new habari kazi kwel kweli
 

Nafikiri ndg Kibanda kesi iliyoko mahakamani inamsumbua, anatafuta pa kutokea, hata hivyo ametoa hoja zisizo na mashiko zaidi ya kutoa maelezo ya jumla jumla, haelezi kwa nini Kikwete alipata kura chache nusura kushindwa (Kama si uchakachuaji) katika uchaguzi uliopita ilhali Kinana huyo huyo anaemsifia ndie alikuwa Meneja wa Kampeni. Kinana alionesha umahiri gani katika kampeni hizo? analo jipya gani nje ya mfumo wa CCM ambalo litampambanua yeye na wenzake?
 
Mh! Kibanda kajidharirisha jamani, hivi alidhani anawaandikia watu wa mtaa wa lumumba!
 
Lakini Kibanda si kasema amekuwa akimfuatilia Kina.Its seems he fell in love with his CV. Sasa CV inaweza kuisafisha CCM kweli. Kinana anaweza kuhakikisha kuwa Kagoda amewekwa ndani. Au ana uwezo wa kusisma jukwaani na kusema kuwa CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi? Au eti nchi yetu inaoongozwa kwa misingi ya ujamaa na kujitegemea kama katiba ya CCM inavyosema? The CCM has simply put a perfumed lipstick on a pig! It will remain a pig. Yaani secretariat mpya ndiyo lipstic and pig ni CCM. This voda fasta thinking,the likes of Kibanda is going to kill us!
 
...mwanaume mzima unatangazia umma kuwa unamuogopa mwanaume mwezio...mambo ya ajabu sanaaaa....nyambafu kabisa..
 
Jamani, mbona wapuuzi tupo wengi! Mimi mwenyewe hapa mpuuzi , kwa mujibu wa bwana kibanda . Hivi kwanza wakuu, kesi ya huyu jamaa inaendeleaje
?
Uoga wa kwenda jela sasa umemfikisha hapa kuanza kuandika makala za kuwafurahisha majambazi ili kesi yake apewe favor ya Nole.
 
Bado nasisitiza watu engi humu hamumjui kinana,wapo wengine wanadhani kinana ni mtu wa karibu na lowassa,wanakosea sana,wengine wanadhani ni mtu unaweza kumtumia kirahisi wanakosea sana,kumjua kinana ni mpaka ukae nae na kuongea nae ndio utamjua ni mtu wa dizaini gani,nashukuru mimi ni mmoja pia wa watu waliowahi kukutana na kuongea nae,jamaa ni kichwa sio msomali wa aina ya Rage ama Bashe,yuko tofauti sana,mnaofahamiana na kubenea jaribuni kumuuliza atawapa stori za huyu mtu,huwa sikubaliani na kibanda lakini kwa andishi lake hili ni kweli anamfahamu kinana.Mwenye hoja na anaetaka kushindana nae kwa hoja lakini,naomba niitoe namba yake hapa bila ridhaa yake lakini kwa nia njema ajaribu kuwasiliana nae..0787 051051,please uwe na hoja lakini,sio usumbufu.Ni mtu wa watu atakupa ushirikiano unaostahili.thanx.
 
haya ayawi ayawi sasa yamekuwa makala ya kibanda kuhusu kinana alikuwa anajua nn anafanya sasa saizi anakuja kufanya kazi new habari kwa rostam aziz na inasemekana mzee lowasa kainunua new habari kazi kwel kweli
kinana sio mtu wa lowassa kabisa,mnachanganya mambo
 

tatizo hawa jamaa zako wa chadema mmewazoesha vibaya,kupenda kusifiwa tu hata kama hawana sifa zozote,hii ndio inakupa shida leo,natabiri hali hii kumtokea kubenea pia siku za usoni,unless aendelee kuandika habari wanazopenda kusikia tu hawa jamaa
 
Sasa Lowassa atapitia wapi kupewa ugombea urais na CCM?
Watu sema hawataki kukubali,hii sekretariat mpya sio rafiki kabisa kwa lowassa na genge lake,na imewekwa pale purposely,ndio mana unaona mtu kama Nape yuko happy sana na mabadiliko haya,watu wanataka kulazimisha kwamba eti lowassa bado ana ushawishi kwenye sekretariet hii,sio kweli.Kinana ni anti lowassa,chukua maneno yangu,na nikweli anavosema kibanda mara kadhaa amekata teuzi za jamaa kwa kuwa alikua anamuona jamaa bado amefungamana na kina lowassa,alikataa pia hii nafasi aliokalia mama makinda sasa ambayo jamaa alitaka akae yeye
 
Hizi porojo na Propaganda zako peleka Lumumba, asiyemjuwa Kinana labda kijana aliyezaliwa miaka ya 90. labda hapa ungetupa Contact ya kampuni ya kusafirisha pembe za ndovu ili na sisi tukiwa na shehena zetu tusafirishe kwa usalama.

Kinana amekuwa mjumbe wa Kamati kuu, chombo kikuu cha maamuzi katika chama je alifanya nini cha ajabu? je ni kwa nini Amekimbia Arusha? Ngongo hebu tusaidie hapa kuna watu wanatulazimisha chupa tuiite Almasi.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…