Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Lakini Huyu ndg Si anayo kesi inayomkabili Mahakamani kisutu pambana wasikufunge
lamba viatu Vya mfalme Ndiyo usalama wako uliko wewe Si wakuandika utumbo Kama huu
kwa yule kibanda tunae mujua
 
- Na wewe kurukia treni kwa mbele ndio nini? Kumbe hujui shutuma nzito alizonazo Rais wako Dr. Slaa za kuiba mke wa mtu na kuongozwa na mkewe!! wacha siasa za makengeza bro!

- So what they are just shutuma kama vipi!!

Le Mutuz!!

W.J. Malecela,

..u can do better than that.

..mimi nilifikiri CCM mmeishaachana na hizi siasa za maji taka, zilizoanzishwa na wanamtandao.

..unakumbuka mwaka 95 wakati Mzee Msekwa alivyochukua fomu wakaanza kumshambulia kuhusu yeye na mama Ana Abdalah.

..ikaja Prof.Lipumba naye akashambuliwa kwa ajili ya ndoa yake na yule mama wa kichaga.

..baadaye uchaguzi mdogo wa temeke, Augustino Mrema akawa anaandamwa na mwanamke aliyekuwa kwenye payroll ya CCM.

..hizi hoja hazina msingi. mambo haya wamefanya watu wazima wenye akili timamu.

..sasa mwanamke ameshaamua anampenda Dr.Slaa, hivi mnategemea mtamlazimisha aishe na mtu asiyempenda??

NB:

..Dr.Slaa angejihusisha na uharamia wa pembe za ndovu kama Abdulrahman Kinana "mr.loliondo", nina hakika CCM mngeshamtia jela.
 
Mkuu,
Huyu LeTotoz ni chizi. Muulize nani anawatunza watoto wake marekani.................kazi kutukana baba za watu
 
- Na wewe kurukia treni kwa mbele ndio nini? Kumbe hujui shutuma nzito alizonazo Rais wako Dr. Slaa za kuiba mke wa mtu na kuongozwa na mkewe!! wacha siasa za makengeza bro!

- So what they are just shutuma kama vipi!!

Le Mutuz!!

Kakangu LeTotoz, Rais wa Ngwasuma. Muda mwingine unaonekana una akili kabla haujafungua mdomo wako.Vitu unavyoongea mara nyingi vinatisha sana. Hauna tofauti na yule ndugu yako Rais wa Akuda, anayefanana katoto kanako balehe, mwenye suruali nyeupe, anayepaki V8 kando kupiga picha kuja kutudanganya wadangayika kwamba anasafiri na bajaj ili apate sifa. Kwa taarifa yako, Mkeo ni wifi yangu

Hatudangayiki tena. Magamba nyie ni sikio la kufa hamsikii dawa. Nyepesi ni kwamba, Rais wetu ana ndoa, siyo sawa na wewe unayekimbia mke na watoto. Uliaga vipi ukiondoka marekani kurudi bongo? Kwa Obama naskia unatafutwa child support.....Jaribu kuwa na heshima kwa wazee wako. Tukianza ya Mzee Malechela na wakina Mama Kilango/Rita Mlaki utafurahi?
 
We mbona ndoa yako imekushnda?ulishndwa hata kutunza mpaka Mzee wako ndo akawa analeta hela ya matumizi!umekimbia familia mkeo na watoto,wanaume wenzako wanakulelea ,mbona sie hatusemi?
- Na wewe kurukia treni kwa mbele ndio nini? Kumbe hujui shutuma nzito alizonazo Rais wako Dr. Slaa za kuiba mke wa mtu na kuongozwa na mkewe!! wacha siasa za makengeza bro!

- So what they are just shutuma kama vipi!!

Le Mutuz!!
 
Kwa taarifa yako, mauzo ya Tanzania Daima yanaongezeka kila kukicha. Dunia inazungumzia Uhuru wa Uhariri wakati Watanzania wajinga kama wewe mnahubiri 'udikteta wa wamiliki'. Kama hatutajifunza kuheshimu maoni tusiyoyapenda tutaendelea kubakia pale pale tulipo.

Unatabia ya kupenda sana kutukana!
Ulimtukana JK na sasa wanampango wa kukufunga!! Unajisafisha kwa maji taka!!

Ongea ukweli kuna akili gani umetumia kwenye kuandika usaha ule? hamna hoja, ni watu watu tu! shame on you!!

Ansbert Ngurumo nadhani ni wakati muafaka wa kumkabidhi jahazi hili...huwa hajingiki kama wewe!
 
quote_icon.png
By Kibanda

Kibanda, unawezaje kutukana watu? Au tayari ndovu Ziko kichwani? Hapa ndo naona sasa umelewa au umenunuliwa. Mbona hata siye washabiki wako unatuweka njia panda with your crude language? You are not representing media freedom. you are simply representing crudeness.... sorry to say but your language has left me speechless. Get sober, then come and apologize to Tanzanians whom you have insulted
 
Umemwagia sifa kemkem kinana, but alikuwepo kwenye siasa za bongo, sasa anaanza kucopy na kupaste. Hakuna jipya ccm
Hoja si Kibanda kuajiriwa na Kampuni ya Mbowe hoja ni Kibanda kumpamba Kinana na kumpa sifa asizostahili huku akipuuza na kuziona si lolote kashfa ambazo zinamuandama kama za Meli yake kusafirisha nyara za Serikali/magendo. Lakini pia Kibanda ametumia sifa dhaifu kumvika ushujaa Kinana.

Jiulize tu Uluteni wa jeshi wa Kinana utauaje upinzani? Uzoefu wake wa Uwaziri utauaje upinzani? Kuwa kwake kampeni meneja wa Mkapa na Kikwete kutauaje upinzani? Ana utofauti gani na akina Mangula, Makamba, Mukama na makada wengine kibao wa CCM ambao wameshindwa kuutokomeza huo upinzani? Yeye hakuwepo kabla ameshushwa kutoka mbinguni? Mtu makini alitegemea Kibanda aunganishe dots za hoja zake na kuja na hitimisho lilisilo hojika lakini kapiga chini.

Ana uhuru wa kumuelezea Kinana anavyotaka lakini si kwa kupotosha na kuover look mambo ya msingi. Kwa mfano ni kwa vipi ampe Kinana uwezo wa kuuzika upinzani wakati miaka yote amekuwa ndani ya CCM akiwa mjumbe wa NEC na CC vyombo ambavyo decisionally ni vya juu? Ina maana Kinana mwenye mbinu za kuua upinzani amekuwa kimya muda wote akishuhudia mdororo na kuelekea kuzimu kwa chama chake cha CCM kutokana na upinzani kushika hatamu? Mbona Kinana huyohuyo kaja na kasi ya kuanza kukopi na kupaste ilani na sera za CDM kama kupunguza bei za vifaa vya ujenzi?

Kibanda katumia hoja rahisi sana unless kama kuna sehemu ya pili ya makala hiyo ambayo itaeleza namna Kinana anaweza kuvizika kweli vyama upinzani. Ametumia hoja hafifu katika masuala magumu na yanayogusa mustakabali wa taifa.
 
Acheni kuchambua personal life ya mtu, tuongelee siasa, mnaharibu thread. Kama hamna cha kuandika kaa kimya, utaheshimika
We mbona ndoa yako imekushnda?ulishndwa hata kutunza mpaka Mzee wako ndo akawa analeta hela ya matumizi!umekimbia familia mkeo na watoto,wanaume wenzako wanakulelea ,mbona sie hatusemi?
 
Ni jambo la kheri sana kusimama peke yako kuutetea ukweli. Ones man's freedom fighter is another man's terrorist. Kwangu mimi Kinana anazo sifa nilizozitaja na kimsingi ni tishio kwa ustawi wa upinzani. Sasa mnataka tuwe na taifa la watu wanaofikiri sawasawa kila siku? Huu hakika ni upuuzi wa kitaifa
 
Unatabia ya kupenda sana kutukana!
Ulimtukana JK na sasa wanampango wa kukufunga!! Unajisafisha kwa maji taka!!

Ongea ukweli kuna akili gani umetumia kwenye kuandika usaha ule? hamna hoja, ni watu watu tu! shame on you!!

Ansbert Ngurumo nadhani ni wakati muafaka wa kumkabidhi jahazi hili...huwa hajingiki kama wewe!

By Kibanda
Kwa taarifa yako, mauzo ya Tanzania Daima yanaongezeka kila kukicha. Dunia inazungumzia Uhuru wa Uhariri wakati Watanzania wajinga kama wewe mnahubiri 'udikteta wa wamiliki'. Kama hatutajifunza kuheshimu maoni tusiyoyapenda tutaendelea kubakia pale pale tulipo.

Kibanda, unawezaje kutukana watu? Au tayari ndovu Ziko kichwani? Hapa ndo naona sasa umelewa au umenunuliwa. Mbona hata siye washabiki wako unatuweka njia panda with your crude language? You are not representing media freedom. you are simply representing crudeness.... sorry to say but your language has left me speechless. Get sober, then come and apologize to Tanzanians whom you have insulted
Huyo ndio mtu anayejiona yeye ana maono na watu tusome na kuamini kile anachotusadikisha, matusi haya ni ishara kwamba anakerwa na watu jinsi walivyosema hapana kwa porojo hizi.

Sisi Watanzania kama ni wajinga basi yeye ni mjinga zaidi, haya maneno yake nimemuhifadhia na hatoamini siku yatakapomlipukia mwenyewe.Badly he is trying to play with Invisible. (not Admin )
 
Ni jambo la kheri sana kusimama peke yako kuutetea ukweli. Ones man's freedom fighter is another man's terrorist. Kwangu mimi Kinana anazo sifa nilizozitaja na kimsingi ni tishio kwa ustawi wa upinzani. Sasa mnataka tuwe na taifa la watu wanaofikiri sawasawa kila siku? Huu hakika ni upuuzi wa kitaifa
U Better shut up ur bad mouth, huwezi kutukana watu kilejaleja hapa kwa sababu tumekupinga ujinga wako, kama umelewa pombe za offer za bure kalale uje hapa kesho, unazidi kujidhalilisha hata ile heshima ndogo uliyobaki nayo naona sasa unaipeperusha, are u Intoxicated ?
 
Great Thinkers,
Baada ya kuisoma makala hii ya Absalom Kibanda Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, nimejikuta napata mashaka sana na zaidi kupoteza imani na uzalendo wake. Pia nimejikuta nikiamini maneno niliyokuwa nikiyapata kijiweni kwamba Kibanda ni mmoja wa beneficieries wa Ufisadi kutoka tasnia ya Habari nchini

NAMUOGOPA ABDURAHMAN KINANA

Na Absalom Kibanda

Kwa mara nyingine tena, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandika historia mpya baada ya kufanya mabadiliko mazito katika safu yake ya uongozi wa kitaifa.

Ni mabadiliko mazito si kwa sababu tu yamefanywa na CCM ambayo imekuwa na rekodi ya kubadili sura za watendaji wake kwa namna na kwa njia tofauti, bali kutokana na ukweli kwamba safari hii mabadiliko hayo yamehusisha watu wazito, wenye historia ya kipekee katika medani ya uongozi ndani na nje ya chama hicho.

Ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka, mabadiliko hayo yanaweza yakaonekana kuwa ni ya kuyabeza au kuyapuuza kama ilivyotamkwa na baadhi ya wadadisi wa mambo wakiwamo wachambuzi wa masuala ya siasa na hata wanazuoni, ukweli unabaki pale pale kwamba kile kilichofanywa na CCM kinaweka alama ya kipekee katika mwenendo wa siasa za kitaifa za siku zijazo.

Wasifu mzito na historia za kutukuka za baadhi ya wateule wanaounda timu ‘mpya’ ya viongozi watendaji wa CCM kwa kiwango kikubwa ndicho kitu kikubwa pekee kinachosababisha mtu yeyote makini ajikute akipata shida kuyabeza yale yaliyofanywa na chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kule Dodoma.

Msuko mpya wa safu ya wakuu wa idara za CCM uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji una kila sababu ya kutafutiwa dawa mahususi na makamanda wa kambi ya upinzani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana kuing’oa CCM madarakani.

Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha wa makala ya leo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

Hupaswi kuwa na akili nyingi kutambua kwamba, umahututi wa CCM kisiasa, kulikokifikisha chama hicho tawala kufikia hatua ya kupoteza dira na kuanza kuliona kaburi la kupoteza madaraka ya dola ndiko kulikorejesha hekima za usikivu kichwani mwa Kikwete hata akalazimika kuwarejesha akina Kinana, Mangula, Seif Khatib na Meghji katika kilinge cha siasa za ushindani mkali ndani na nje ya CCM.

Siyo siri hata kidogo kwamba, hekima hii mpya ya Kikwete ya kumrejesha Kinana ulingoni, ambaye siku chache tu zilizopita alitangaza kustaafu siasa huku akisema alikuwa akikusudia kuwaachia vijana kusukuma gurudumu la uongozi, inahusisha kichwa zaidi ya kimoja kutoka ndani na nje ya CCM.

Kama ilivyo kwa wengi wengine nilianza kulisikia jina la Kinana likihusishwa na ukatibu mkuu wa CCM miaka miwili au mitatu iliyopita hali ambayo ilipata kusababisha nifikie uamuzi hata wa kumuuliza yeye mwenyewe kuhusu taarifa hizo.

Jibu ambalo Kinana mwenyewe alipata kunipa kwamba alikuwa akipenda kuona akiendelea kupata fursa ya kukitumikia chama chake kama mshauri na kwa nyakati mahususi kama zile za kampeni na si kwa nafasi ya ukatibu mkuu lilikuwa likinipa sana faraja.

Kilichokuwa kikinipa faraja si kingine chochote bali fikra zangu (sahihi au potofu) ambazo siku zote zilikuwa zikinifanya niamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Katika mazingira ambayo CCM imeweza kuepuka zahama ya kumeguka vipande viwili kwa kuzingatia maono aliyokuwa nayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwangu mimi Kinana wa zama hizo alikuwa na anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam nikiwa nimeongozana na mhariri wangu, Muhingo Rweyemamu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.

My Take:
-Hapo kwenye RED
naona Kibanda kajikita katika kueleza kifo tarajiwa cha upinzani kwa kumezwa na rekodi ya kinana tu bila hata kuzingatia nyakati zilizopo za kisiasa, kupwaya kwa ushindi wa JK kwneye matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na zaidi mchoko wa kimaisha walionao watanzania sasa. Kibanda amejaza mahaba binafsi kwa Kinana pasipo kuzingatia muktadha wa kisiasa uliopo nchini.

Lakini pia Kibanda amejikita katika kusisitiza hatari ya upinzani kufa kutokana na Kinana kuwa GS wa CCM bila kueleza ni kwa vipi anaweza kupambana na hoja zinazotoka kambi ya upinzani hasa CDM au ni Uluteni wake tu Jeshini ndiyo utamfanya aue upinzani.

Aidha, Kibanda anatumia Umeneja Kampeni wa Kinana kwa wagombea wa urais wa CCM bila hata kusumbua kichwa chake,kwamba kuwa meneja haina maana unakuwa incharge wa ushindi wa mgombea bali timu nzima ya kampeni ya Chama ndiyo hufanya kazi hiyo. Mathalan, utamsifu vipi Kinana kwa ushindi wa Mkapa mwaka 1995 wakati Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kivuri chake kilikuwa bado kinaishi ndani ya mioyo ya watanzania? Ni kweli hili si la kubeza lakini si la kumpa credit kubwa kiasi anachotoa Kibanda

-Kwenye Blue,
Kibanda kawa kipofu kiasi kwamba kwakwe yeye tuhuma za ufisadi zinazomkabili Kinana na baadhi ya wana safu wa Sekretarieti mpya ya CCM anaziona nyepesi na zisizo na mashiko. Kwake yeye (Ufisadi ni mwepesi na si hoja kwa sasa) bali hoja ni Kinana na rekodi yake tu tena ya huko nyuma.

Tujadili kwa pamoja hii makala.

hakuna mwandishi wa habari tanzania asiyekuwa na price tag, waandishi wa habari ni bidhaa kwa sababu ya njaa na malipo duni. kwa habari ya kinana nataka niikumbushe hii bidhaa inayoitwa kibanda kuwa huyo kinana mbali na kuwa ni fisadi sugu, pia hana jipya analoweza kufanya CCM huyu uchaguzi wa 2010 alipewa jukumu ambalo baadae alizidiwa akili na miraji kikwete aka hijack office yake yeye akabaki kama mdoli, sasa leo ametoa wapi ujanja wa kuweza kuisaidia CCM, kama alizidiwa akili na yule misheni town sioni msaada wala kitisho cha kinana.
 
Ni jambo la kheri sana kusimama peke yako kuutetea ukweli. Ones man's freedom fighter is another man's terrorist. Kwangu mimi Kinana anazo sifa nilizozitaja na kimsingi ni tishio kwa ustawi wa upinzani. Sasa mnataka tuwe na taifa la watu wanaofikiri sawasawa kila siku? Huu hakika ni upuuzi wa kitaifa

i guess you are either sold out or married to kinana,and relatively your poverty or your love is your weakness, but you reserve the right to speak your mind lakini hili ungeweza kulisema kimoyomoyo au verbally sio kulitia katika maandishi u can not be trusted umekuwa kama chotara wa kipalestina na kiyahudi huaminiki ubabani na ujombani, wewe ni wa kutupwa na kupuuzwa.
 
Mbona ye Le Totoz kamuongelea Dr Slaa na ndoa yake?amejibiwa kwa namna ya maandishi yake..ukija na kashfa,unajibiwa kwa kashfa..ukileta hoja utapata hoja
Acheni kuchambua personal life ya mtu, tuongelee siasa, mnaharibu thread. Kama hamna cha kuandika kaa kimya, utaheshimika
 
Swali la kizushi kwa wana JF...hivi Kinana kaoa?
 
U Better shut up ur bad mouth, huwezi kutukana watu kilejaleja hapa kwa sababu tumekupinga ujinga wako, kama umelewa pombe za offer za bure kalale uje hapa kesho, unazidi kujidhalilisha hata ile heshima ndogo uliyobaki nayo naona sasa unaipeperusha, are u Intoxicated ?

Mkuu Matola taratibu hoja hujibiwa kwa hoja! Jinsi unavyojibu napata majibu sahihi ni nani mlevi kati yenu

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Huyo ndio mtu anayejiona yeye ana maono na watu tusome na kuamini kile anachotusadikisha, matusi haya ni ishara kwamba anakerwa na watu jinsi walivyosema hapana kwa porojo hizi.

Sisi Watanzania kama ni wajinga basi yeye ni mjinga zaidi, haya maneno yake nimemuhifadhia na hatoamini siku yatakapomlipukia mwenyewe.Badly he is trying to play with Invisible. (not Admin )
Matola ulitaka Kibanda aandike habari gani za kukufurahisha? Mpaka sasa hivi nashindwa kukuelewa umegeuka Rush Limbaugh? anayebishana na ukweli kila siku?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom