Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Katika mambo kama haya ndipo ama werevu au ujinga wa Watanzania walio wengi unapoweza kupimwa.
Kwanza binafsi nichukue fursa hii kumpongeza sana Absalom Kibanda kwa kuwa katika hili Kibanda amedhihirishia uma kuwa anachoheshimu yeye ni uhuru wake wa kusema yale anayoyaamini lakini vile vile yeye hayuko confined ndani ya box i.e si mtu wa kupewa ama wa kushurutishwa kuandika yale ambay yeye hataki au haoni haja, tija, na mantiki ya kuyaandika. Kwa maana nyingine nyepesi ni kwamba Kibanda anaheshimu TAALUMA yake na kaonesha kuwa kapikika kitaaluma.
Ila sisi Watanzania mi nadhani huu ushabiki na ujinga tunaojijengea kwamba kunya anye kuku akinya bata kaarisha utatugarimu vibaya mno. Yani hatuna hoja hatuna sababu ya msingi bali tunasimamia ushabiki na ile dhana kwamba kwa kuwa huyu yuko Uhuru ama Tz Daima basi anapaswa siku zote kuandika mema tu ya ule mrengo tunaoutaka sisi. Kwangu huu ni ubatili na upuuzi zaidi ya upuuzi wenyewe.
Kibanda kaelezea anavyomfahamu Abdulrahman kuanzia Jeshini, Uwaziri, mpaka alivyoendesha Kampeni za CCM na namna ambavyo yeye alikutana na kuzungumza na Kinana kwa mara ya kwanza. Hivyo kwa ufupi Kibanda anasema haya anayoyaandika ameshayafanyie tafiti hivyo ana haki kimsingi kuyasema na jamii ijue.
Sasa sisi wengine tafiti hatujawahi kufanya huyo Kinana mnamfahamu tu kwa kumsikia kwa watu wengine hasa wale ambao tunawaona kama Miungu yetu ambao wao wakisema basi nasi tunasujudia yale waliyoyasema na hatuna kazi ya kujiridhisha juu ya hayo waliyoyasema huu kwangu bado ni ulofa na uvivu wa kutafuta ukweli na kushabikia ujinga.
Watanzani ifikie mahali turidhike na tukubaliane kutokubaliana manake haitatokea siku sote tufanane kimtazamo, kifikra, kimawazo na hata kiitikadi haiwezekani utake Kibanda aseme yale ambayo wewe unataka ayasema. Mijitu mingine mko na elimu ya kutosha lakini bado tu mnadhalilisha hata hicho mlicho nacho. Kweli nimeamini kwenye msafara wa Mamba...............
Narudi tena Kibanda kwa namna alivyoandika hili kajipambanua kuwa yeye hayuko ndani ya box bali mawazo yake na fikra zake ziko kitaaluma zaidi. Wewe ujuaye tofauti na Kibanda weka yako nawe humu na si kumshambulia kijinga namna hii. Tunadhani na kuamini kuwa anachopaswa Kibanda ni kutupia mawe CCM, Serikali yake na Viongozi wake basi akienda kinyume hapo basi kakosea. Huu si uungwana kwangu huu utadndelea kubakI kuwa ulofa, upuuzi, ujinga, na kufilisika kimtazamo na kifikra na ni udhalilishaji wa mtu mwenyewe.
Eti Kibanda kanunuliwa guyz!!!!! Aibu kwenu; jipangeni kuheshimu fikra na mawazo ya wengine katika njanya zote iwe hasi ama chanya na tusiendelee kutamani kusikia yake tuyapendayo tu bali hata yale tusiyoyapenda. Kimsingi tujiamini na tuwe na uwezo wa kujibu na kupambanua yote...... Manake kama tukiendelee kuutendea hivi huu mti mbichi ule mkavu je???
Kibanda sina shaka hata kidogo na wewe pamoja na uwezo wako wengine umekuwa ukitugonga sana kuoita maelezo ila tumeendelea kutambua kuwa hatuna budi kutofautiana hivyo na vile vile kuheshimu tofauti hizo manake huo ndio uhuru wenyewe. Hivyo kwa hili umezidi kudhihirisha wewe ni kiwango cha namna gani.
Haihitaji uwe na Phd ama uwe Pro kujua na kuamini haya aliyoyasema Absalom Kibanda "Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete"
Absalom Kibanda critics are our friends........ Aluta continue