Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

..Kama walivyokuwa viongozi wengi wa Tanania hawatofautiani..Kinana kama Kinana anabakia kuwa Kinana... ni yule yule hajabadilika.. inawezeekana kuwa baada ya kukaa nje kwa utendaji wa moja kwa moja wa Chama alidhani kwamba watu wamesahau kumbukumbu zake... hii ni pamoja waliompa huo uteuzi..lakini Kabanda kama Kabanda makala yake imeeangalia musakabali mzima wa utendaji wa Kinana kwamba ni mtu anayeweza kufiti mahali popote yani kwenye utendaji mzuri lakini pia kwenye maswala ua kifisadi nako hachezi mbali.. hivi ndivyo walivyo viongozi wengi wa TZ
 
Bora ume muuliza maswali mazuri na wanaonekana kujua mipango yote na wana ushahidi kwanini wana ukalia wanaogopa nini?
Kwao wanataka kusema serikali ya ccm inawaogopa chadema?

Lakini nimegundua wanaogopa kwani hawana ushahidi wowote ni allegations tuu,!

basi kama ni mpango wa akina slaa na kanisa basi hii siyo serikali ni matakataka, hizi ni roho za watu zina potea kama serikali ninjua kuna mipango ya kidharimu inasubiri nini kuchukua hatua stahiki? kova naye kaingia aje katika ngonjera za ki sh ga. mnafanya utani na roho za watu haya mambo yatarudi tu. imekuwa kama michezo ya kuigiza kwanini hamkulitumia mwana harisi liwasaide uchunguzi, usijipumbaze amka!
 
Tarehe 21 Novemba 2012 mwana JF mmoja kwa jina WOWOWO aliandika mada yake yenye kichwa cha habari
ABSALOM KIBANDA: NAMUGOPA ABDURAHMAN KINANA. Katika mada hiyo bwana WOWOWO aliweka jamvini Makala iliyoandkwa na ABSALOM KIBANDA, makala ambayo ilikuwa ikisifia uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM taifa DR. JAKAYA KIKWETE alioufanya wa kumteua ABDURAHMAN KINANA kuwa Katibu mkuu wa CCM. Bwana WOWOWO ambaye katika mada hiyo alionesha waziwazi kuwa ni mnazi wa CDM alimshambulia waziwazi bwana KIBANDA kwa kitendo chake cha kusifia uteuzi huo wa CCM. Aidha katika makala hiyo bwana KIBANDA naye alionesha wazi kuwa ni mwanahabari-Mwanasiasa na mnazi wa CDM pale alipowatahadharisha makamanda wake (CDM) kutochukulia poa uteuzi wa KINANA kwa vile ni mchapa kazi na kwamba atawapa tabu katika harakati zao za kutaka kuchukua nchi.

mytake: Pamoja na KIBANDA kuwa mwanahabari na mwanaharakati, lakini kwa makala yake hii ni wazi pia kuwa ni mwana-CDM na ndiyo maana alikuwa akiwatahadharisha viongozi wa CDM kuwa makini na KINANA.
Hatumjui mwenye ID ya WOWOWO, aweza kuwa SLAA, MBOWE au MNYIKA au mwana-CDM yeyote ambaye kwa namna moja au nyingine hakufurahishwa na makala hii, hasa ukizingatia kuwa KIBANDA alikuwa anafanyia kazi gazeti la Tanzania Daima.
Kwa maana hiyo inawzekana kabisa miongoni mwa sababu za KIBANDA kuondoka FREEMEDIA na hivyo, na kama hiyo ni sababu basi uwezekano wa uhasama huo kuendelea ni mkubwa na kupelekea kutokea kwa matukio kama hili liliomkuta KIBANDA.

Nakala ya hiyo makala hii hapa chini.


Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Great Thinkers,
Baada ya kuisoma makala hii ya Absalom Kibanda Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, nimejikuta napata mashaka sana na zaidi kupoteza imani na uzalendo wake. Pia nimejikuta nikiamini maneno niliyokuwa nikiyapata kijiweni kwamba Kibanda ni mmoja wa beneficieries wa Ufisadi kutoka tasnia ya Habari nchini


NAMUOGOPA ABDURAHMAN KINANA

Na Absalom Kibanda

Kwa mara nyingine tena, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandika historia mpya baada ya kufanya mabadiliko mazito katika safu yake ya uongozi wa kitaifa.

Ni mabadiliko mazito si kwa sababu tu yamefanywa na CCM ambayo imekuwa na rekodi ya kubadili sura za watendaji wake kwa namna na kwa njia tofauti, bali kutokana na ukweli kwamba safari hii mabadiliko hayo yamehusisha watu wazito, wenye historia ya kipekee katika medani ya uongozi ndani na nje ya chama hicho.

Ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka, mabadiliko hayo yanaweza yakaonekana kuwa ni ya kuyabeza au kuyapuuza kama ilivyotamkwa na baadhi ya wadadisi wa mambo wakiwamo wachambuzi wa masuala ya siasa na hata wanazuoni, ukweli unabaki pale pale kwamba kile kilichofanywa na CCM kinaweka alama ya kipekee katika mwenendo wa siasa za kitaifa za siku zijazo.

Wasifu mzito na historia za kutukuka za baadhi ya wateule wanaounda timu ‘mpya’ ya viongozi watendaji wa CCM kwa kiwango kikubwa ndicho kitu kikubwa pekee kinachosababisha mtu yeyote makini ajikute akipata shida kuyabeza yale yaliyofanywa na chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kule Dodoma.

Msuko mpya wa safu ya wakuu wa idara za CCM uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji una kila sababu ya kutafutiwa dawa mahususi na makamanda wa kambi ya upinzani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana kuing’oa CCM madarakani.

Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha wa makala ya leo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa,nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

Hupaswi kuwa na akili nyingi kutambua kwamba, umahututi wa CCM kisiasa, kulikokifikisha chama hicho tawala kufikia hatua ya kupoteza dira na kuanza kuliona kaburi la kupoteza madaraka ya dola ndiko kulikorejesha hekima za usikivu kichwani mwa Kikwete hata akalazimika kuwarejesha akina Kinana, Mangula, Seif Khatib na Meghji katika kilinge cha siasa za ushindani mkali ndani na nje ya CCM.

Siyo siri hata kidogo kwamba, hekima hii mpya ya Kikwete ya kumrejesha Kinana ulingoni, ambaye siku chache tu zilizopita alitangaza kustaafu siasa huku akisema alikuwa akikusudia kuwaachia vijana kusukuma gurudumu la uongozi, inahusisha kichwa zaidi ya kimoja kutoka ndani na nje ya CCM.

Kama ilivyo kwa wengi wengine nilianza kulisikia jina la Kinana likihusishwa na ukatibu mkuu wa CCM miaka miwili au mitatu iliyopita hali ambayo ilipata kusababisha nifikie uamuzi hata wa kumuuliza yeye mwenyewe kuhusu taarifa hizo.

Jibu ambalo Kinana mwenyewe alipata kunipa kwamba alikuwa akipenda kuona akiendelea kupata fursa ya kukitumikia chama chake kama mshauri na kwa nyakati mahususi kama zile za kampeni na si kwa nafasi ya ukatibu mkuu lilikuwa likinipa sana faraja.

Kilichokuwa kikinipa faraja si kingine chochote bali fikra zangu (sahihi au potofu) ambazo siku zote zilikuwa zikinifanya niamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Katika mazingira ambayo CCM imeweza kuepuka zahama ya kumeguka vipande viwili kwa kuzingatia maono aliyokuwa nayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwangu mimiKinana wa zama hizo alikuwa na anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam nikiwa nimeongozana na mhariri wangu, Muhingo Rweyemamu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.


My Take:
-Hapo kwenye RED
naona Kibanda kajikita katika kueleza kifo tarajiwa cha upinzani kwa kumezwa na rekodi ya kinana tu bila hata kuzingatia nyakati zilizopo za kisiasa, kupwaya kwa ushindi wa JK kwneye matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na zaidi mchoko wa kimaisha walionao watanzania sasa. Kibanda amejaza mahaba binafsi kwa Kinana pasipo kuzingatia muktadha wa kisiasa uliopo nchini.

Lakini pia Kibanda amejikita katika kusisitiza hatari ya upinzani kufa kutokana na Kinana kuwa GS wa CCM bila kueleza ni kwa vipi anaweza kupambana na hoja zinazotoka kambi ya upinzani hasa CDM au ni Uluteni wake tu Jeshini ndiyo utamfanya aue upinzani.

Aidha, Kibanda anatumia Umeneja Kampeni wa Kinana kwa wagombea wa urais wa CCM bila hata kusumbua kichwa chake,kwamba kuwa meneja haina maana unakuwa incharge wa ushindi wa mgombea bali timu nzima ya kampeni ya Chama ndiyo hufanya kazi hiyo. Mathalan, utamsifu vipi Kinana kwa ushindi wa Mkapa mwaka 1995 wakati Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kivuri chake kilikuwa bado kinaishi ndani ya mioyo ya watanzania? Ni kweli hili si la kubeza lakini si la kumpa credit kubwa kiasi anachotoa Kibanda

-Kwenye Blue,
Kibanda kawa kipofu kiasi kwamba kwakwe yeye tuhuma za ufisadi zinazomkabili Kinana na baadhi ya wana safu wa Sekretarieti mpya ya CCM anaziona nyepesi na zisizo na mashiko. Kwake yeye (Ufisadi ni mwepesi na si hoja kwa sasa) bali hoja ni Kinana na rekodi yake tu tena ya huko nyuma.

Tujadili kwa pamoja hii makala.​
Last edited by WOWOWO; 21st November 2012 at 17:39.​

Pasco, Thesi, Ame and 10 others like this.
SIASA ZETU ZIMEKOSA DIRA NA KWA MAANA HIYO TIJA KWA MAENDELEO YETU-MIMI


Kazi imeanza sasa, tusubiri tuone mwisho wake.
 
NI muhimu sna sasa tubadilike, tuache kushabikia upuuzi kwasababu tukipiga propaganda kuisafisdha serikali tutapata vyeo tutasifiwa na wakubwa. hakuna mtu mwenye haki ya kuua awe CDM awe CCM, kama unapewa ujira wako kwa kumnyamazisha mwana mapinduzi inakusaidia nini..mfano waliomtesa ulimboka. hebu kaa chini ufikilie kazi yako ni kuuwa watu wanaoichana selikari, ukiisha toa roho ya mtu unakwenda kwa mkubwa wako wa kazi unamwambia nimemaliza kazi, basi unafurahi unapewa mshaara wako unakwenda kula na watoto wako nyumbani na bia hiyo siku unakunywa, na unakuwa ukisikiizia kwa makini kama utapandishwa cheo kwa kuua bila huruma, na unajiopna wewe ni bianadanu.
" na ukitaka kujua ni kazi ya laana hawawezi kuitangaza hadharani, kama mimi ni muhasibu, mimi mkulia...kwasababu wana jua wana fanya uchafu mkubwa sana.n alaana iwe juu yao
 
HIvi kitu ambacho naiuliza na nashidwa kupata jibu, hivi huyo mtu anye ingia umu kushabikia matendo machafu yanayo fanywa na serikali ni binadamu kweli au nimizuka isiyo kuwa na roho. "TANZANIA KISIWA CHA AMANI< TUNAJIVUNIA UMOJA WETU. kazi kweli kweli
 
hudhani nini. kwamba kibanda kaandika upuuzi au hudhani kama CHADEMA na Mbowe wanahusika na tukio la kibanda

Lakini hapa wote tunatwanga maji katika kinu tu.

Kama ile tume iliyoundwa kuchunguza tukio la Dr. Ulimboka na ile ya marehemu Mwangosi zingelikuja na majibu basi haya matukio yasingeliendelea kutokea.

Lakini bado hatukupewa matokeo ya tume zile na leo imeundwa tume nyingine tena bila shaka haitaleta majibu kwetu walipa kodi kama kwa tume zilizoitangulia (FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE).

Utesaji wa Kibanda na ule wa Dr. Ulimboka unafanana, bila shaka wahusika ni wale wale.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Mungu yuko karibu zaidi na watanzania, hivi hii aibu ya ulimboka wana ifichia wapi? ulisikia ushahidi wa polisi kuhusu mwangosi! ni kinywa kilicho laaniwa ndiyo kinaweza kutoa maneno awaliyo toa askari ambao tuna tegemea walinde usalam wetu, nini maan ya kitu kizito, huu ni wendawazimu. nchi imelw=aaniwa hiii. moto tunao ulilia unakuja na tuna fanya hivi kwasababu tanzania ni nchi ya amani raia ni wapole hawataki matata, wakati huuu unaisha


haya yote yanasabaishwa na wanasiasa. Wanapandikiza chuki miongoni mwa wananchi ilimradi tu kujitafutia umaarufu. Sasa kama hili za KIBANDA limetokana na makala hii si ni hatari sana, mbona hakuna jambo baya aliloliandika hapa zaidi ya kusema ukweli mtupu. Mbona hivi sasa CDM hawalali usiku kucha utasikia NAPE, MWIGULLU, MANGULA, KINANA, mara Wasira, utafikiri kazi yao ni kuongelea CCM. Mungu amsaide KIBANDA apone haraka jamani.
 
ni wazi kwamba makala kama hizi haziwapendezi wana CHADEMA na muda si muda itaondolewa. lakini pia inatufumbua macho kuwa KIBANDA alikuwa mkweli na aliamua kufunguka ijapokuwa alijua kuwa kwa watu wa visasi kama akina MBOWE na SLAA hawezi kupona kwa makala kama hiyo. Hatua ya kwanza waliyoifanya chadema ni kumshinikiza aondoke freemedia na hatua ya pili ni hii iliyofanyika juzi. lengo lao halikuwa kumuua bali kumfanya ashindwe kutekeleza au achukue muda mrefu kutekeleza majukumu yake akiwa huru kutoka katika makucha ya madhalimu wa CHADEMA. bila shaka anayo mengi moyoni na ambayo chadema hawataki yajulikane. thanks kwa kutukumbusha maana walio wengi waliidharau makala hiyo lakini kwa watu makini kama akina Mbowe, walichukua hatua na wataendelea kuchukua dhidi ya wale wengine waliojitambua kama kibanda


Unaleta mahubiri ya ustaadhi ILUNGA?!!!...
 
haya yote yanasabaishwa na wanasiasa. Wanapandikiza chuki miongoni mwa wananchi ilimradi tu kujitafutia umaarufu. Sasa kama hili za KIBANDA limetokana na makala hii si ni hatari sana, mbona hakuna jambo baya aliloliandika hapa zaidi ya kusema ukweli mtupu. Mbona hivi sasa CDM hawalali usiku kucha utasikia NAPE, MWIGULLU, MANGULA, KINANA, mara Wasira, utafikiri kazi yao ni kuongelea CCM. Mungu amsaide KIBANDA apone haraka jamani.

Umekula kiti moto?!..
 
Mkuu hilo ni suala la mgongano wa kimaslahi wewe. Hivi unawezaje kusema Tanzania Daima siyo la CHADEMA wakati mmiliki wake ni Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Mwandika makala anaandika akiwa Tanzania Daima halafu, mabya kabisa anasifia chma hasimu na CHADEMA, usiwe mtumwa wa kushabikia siasa, simama katika ukweli utaonekana wa maana katika jamii.

Umesema ni la mwenyekiti wa CHADEMA na hapo hapo unasema ni la chadema???? Kwa hio Kampuni ya kusafirisha meno ya tembo,Ile ya katibu mkuu wa CCM ,Bwana kinana pia hiyo kampuni ni ya CCM? Kweli wewe poyoyo
 
ukiweza kufanya analysis vizur bila kua bias wakati wa issue ya ulimboka niliona upande wa pili kwa mtizamo wangu na mateso ya Kibanda yanazid kunifungua macho.
iko hivi issue ya ulimboka ilikua ni ya uchonganishi kunawatu walijipenyeza kati na kwakujua kua kufanya vile kutazidisha ugomvi kati ya Madaktar pamoja na wananchi dhidi ya Serekali ili wao kupitia huo ugomvi wapenye katikati na kuanekana mbadala.(a) wamijisahau wakautumia mbinu zile zile kwa adui yao anayejulikana wazi kama ndivyo sikutegemea
(b) Mchezo walioufanya wao thidi ya ugomvi kati ya ulimboka na serekali wamefanyiwa wao kuchonganishwa na waandishi wa habari.
tumefika mbali sana na huu mchezo wa uchonganishi kwani hata maswali na kidini yanafinyika kwa kutumia mchezo mchafu unamwagia tindikali mwenzako ili useme upande wa pili unahusika, mnatoa uhai wa mwingine ili kusingizia flani ndo wahisika.haya yote yana malipo.
 
Ili mradi yupo hai
basi yeye ndo aisaidie polisi kutaja suspects...

mengine yote porojo

Kwa uduni wa haw awatu mara wapatiwapo dozi ya Uli au ya mwakyembe, utashangaa wakiwa useful ------ zaidi.Wakirudi sijui wanakuwa wame wa format au.Mwone hata Zitto.

Jamaa anaponea tundu la sindano akirudi airport cha kwanza ni kumshukuru JK na serikalia yake sikivu.Halfu anaongeze akuwa atapambana na hao watu .Full stop.Hutamsikia tena zaidi ya kutoa smile mbaya ya majeraha na mapamabo kwa JK.
 
NDO KUSEMA HATA MWAKYEMBE ALIFANYIZIWA NA CDM, mh! Pole ndugu zangu wanambeya! Ulimboka, Mwangosi, Mwakyembe, na yule jaji nani aliyefia getini kwa kupigwa risasi! Duh! mbombo ghafu!

Mwigulli anao mkanda wa mipango ya mauji inawezekana, tusubiri mbona unahamaki mkuu, kwani kama mtandao wao ni mkubwa watashindwa nini kuwadhuru hao uliowataja?
 
NI muhimu sna sasa tubadilike, tuache kushabikia upuuzi kwasababu tukipiga propaganda kuisafisdha serikali tutapata vyeo tutasifiwa na wakubwa. hakuna mtu mwenye haki ya kuua awe CDM awe CCM, kama unapewa ujira wako kwa kumnyamazisha mwana mapinduzi inakusaidia nini..mfano waliomtesa ulimboka. hebu kaa chini ufikilie kazi yako ni kuuwa watu wanaoichana selikari, ukiisha toa roho ya mtu unakwenda kwa mkubwa wako wa kazi unamwambia nimemaliza kazi, basi unafurahi unapewa mshaara wako unakwenda kula na watoto wako nyumbani na bia hiyo siku unakunywa, na unakuwa ukisikiizia kwa makini kama utapandishwa cheo kwa kuua bila huruma, na unajiopna wewe ni bianadanu.
" na ukitaka kujua ni kazi ya laana hawawezi kuitangaza hadharani, kama mimi ni muhasibu, mimi mkulia...kwasababu wana jua wana fanya uchafu mkubwa sana.n alaana iwe juu yao

naona mnaanza kuweweseka. kama mnafanya kwa lengo la kupata posho hiyo imekula kwenu. Mna kesi ya kujibu Mbele ya Mungu aliye Mkuu
 
Kwa uduni wa haw awatu mara wapatiwapo dozi ya Uli au ya mwakyembe, utashangaa wakiwa useful ------ zaidi.Wakirudi sijui wanakuwa wame wa format au.Mwone hata Zitto.

Jamaa anaponea tundu la sindano akirudi airport cha kwanza ni kumshukuru JK na serikalia yake sikivu.Halfu anaongeze akuwa atapambana na hao watu .Full stop.Hutamsikia tena zaidi ya kutoa smile mbaya ya majeraha na mapamabo kwa JK.

na mbowe aliyemsifia kikwete kwa kujenga barabara kwao utamwitaje?
 
Mmmmh inawezekana mtu yeyote akimua kutengeneza story inaweza kushabikiwa na wa2 hata kama story ya kufikirika(fiction).sijui kama tutafika kwa njia ya kudivert attention za wa2 kwenye matukio makubwa.mind you,you can not fool all people at a time.Mungu ibariki Tanzania na wa2 wake.
 
Umesema ni la mwenyekiti wa CHADEMA na hapo hapo unasema ni la chadema???? Kwa hio Kampuni ya kusafirisha meno ya tembo,Ile ya katibu mkuu wa CCM ,Bwana kinana pia hiyo kampuni ni ya CCM? Kweli wewe poyoyo

kampuni na propaganda kama FREEMEDIA haiwezi kujitenga na CHADEMA. ndiyo maana katika hiyo makala, Kibanda kaandika kama Mhariri Mkuu wa FREEMEDIA lakini anajinasibisha na CHADEMA na anaowahadharisha ni viongozi wa chadema. hutumii nguvu kufikiri hapo
 
Me ninachotaka ni kwamba hawa wanao sema ni chadema wapeleke ushahidi hili ushsughulikiwe mapema pengine si wanajua na wana uhakika ni chadema labda tume italeta majibu!

Lakini hapa wote tunatwanga maji katika kinu tu.

Kama ile tume iliyoundwa kuchunguza tukio la Dr. Ulimboka na ile ya marehemu Mwangosi zingelikuja na majibu basi haya matukio yasingeliendelea kutokea.

Lakini bado hatukupewa matokeo ya tume zile na leo imeundwa tume nyingine tena bila shaka haitaleta majibu kwetu walipa kodi kama kwa tume zilizoitangulia (FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE).

Utesaji wa Kibanda na ule wa Dr. Ulimboka unafanana, bila shaka wahusika ni wale wale.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Huyo zakia meghji muheshiwa si anazo scandal kibao za wiki kipindi akiwa wizara ya fedha na maliasili,sema lingine yani hapo katolewa afadhali kaingia potelea kwa mbali yote magamba

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom