Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Absalom Kibanda: Namuogopa Abdurahman Kinana

Kuna mdau aliandika hii thread jana lakini haraka ikatolewa na kusababishwa watu wengi kuikosa.,inafanana na haya ambayo yameandikwa hapa;

KIBANDA NI MUHANGA WA ALICHOKIANDIKA..? Connected dots…!
Jana usiku limetokea tukio baya la kuvamiwa na kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Ndugu Abdalom Kibanda. Tukio hilo ambalo limesababisha sintofahamu kubwa miongoni mwa watanzania wanahabari, wapenda uwazi na ukweli na wale wenye kusimamia misingi ya Amani na utulivu katika nchi hii.
Aina ya tukio lenyewe na upekee wa utokeaji wake umegubikwa na utata mkubwa kiasi kwamba akili yangu ikanituma kutafakari kwa kina na kuyaandika haya, ikiwa ni miongoni mwa YAWEZEKANAYO kuwa ndiyo yaliyosababisha tukio ilo la kusikitisha kutokea kwa Mtanzania mwenzetu huyu kipenzi cha wanahabari.
• Mengi yanahusuanishwa na tukio hili, lakini wengi wakihusianisha tukio hili na kazi ya mhusika ya Uandishi, ambapo tukio hili linamkuta katika kipindi ambacho mtindo wa uandishi wake umebadilika na mfumo wa hoja zake umekuwa wa mlengwa wa kati. Lakini pia wapo wachache wanaohusianisha tukio hilo na ujambazi ama unyang’anyi, hisia ambazo binafsi nazipinga kwani Watu waliomvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake hawakuchukua kitu chochote katika vitu ambavyo Mhariri huyo anavimiliki kuanzia gari, simu na pesa.
• Hivyo, nalihusianisha tukio hili na aina ya kazi ambayo mhanga anaifanya, kazi ya UHARIRI WA HABARI katika vyombo vya habari, na hisia zangu zimenipeleka huko baada ya kuzingatia kwa umakini mkubwa matukio yafuatayo.
a) 14th November 2012, Baada ya kuundwa kwa sekretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kibanda akiwa ni Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima ambalo linafahamika wazi kuwa ni chombo cha propaganda cha Chadema chini ya Mbowe, aliandika makala ambayo ilikuwa ikisifu safu hiyo mpya ya uongozi ya CCM,
huku akinukuu kauli mbalimbali za viongozi wa upinzani akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Znz, Mhe. Maalim Seif Sharif. Baada ya tukio hili wakuu wa gazeti hilo walimuita na kumuonya juu ya makala yake hiyo.
Lakini katibu Mkuu wa Chadema hakuishia na kuridhishwa kwa kuonywa kwa Kibanda bali alienda mbele zaidi na kumjibu; ambapo tarehe 16th November 2012, sehemu ya nukuu yake alipokuwa akimjibu Kibanda inapatikana katika link hii; http://www.habarimasai.com/en/zilizopita/item/397-dk-slaa-awashambulia-walioteuliwa-sekretarieti-mpya-ya-ccm-asema-wapo-kwenye-kashfa-ya-epa

Na link nyingine ndani ya Tanzania Daima la ijumaa ya tarehe 16 th Nov 2012 ni hii;

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=42529

b) Lakini mara tu ya jibu hilo la Slaa kwa Kibanda, Mhariri huyo kwa ufundi mkubwa aliandika makala nyingine ambayo ilikuwa ikimsifu zaidi Katibu Mkuu mpya wa CCM, ndugu Abdulrahaman Kinana, ambae Slaa alimkosoa katika majibu yake dhidi ya Kibanda. Mhariri huyo makini alieleza bayana kuwa kuiponda sekreatieti mpya ya CCM ni sawa na kukosa akili, akaendelea kufafanua na kutaja wasifu wa kila kiongozi kwa kadri alivyowafahamu yeye, akielekeza nguvu zaidi kwa Katibu Mkuu Kinana na kuelezea umahiri wa kinana kama strategist tangu akiwa jeshini, lakini akataja uzoefu wake ndani ya chama na pia kutaja alivyoshiriki katika chaguzi mbalimbali na kuwawezesha wagombea urais wa Awamu ya tatu na Nne kushinda kwa kishindo.
Baada ya Makala hiyo ya pili, ulizaliwa mgogoro wa haja ndani ya kampuni hiyo ya freemedia uliomuhusisha Kibanda na wamiliki wa kampuni na Chama kinacholitumia gazeti hilo. Mgogoro ambao ulipelekea Kibanda kuihama Freemedia na kuhamia katika New Habari Corporation ambayo kimsingi ni ya wadau wa Chama Cha Mapinduzi na kampuni ambayo kwa namna moja ama nyingine inaruhusu kuandikwa habari katika mandhari na tafsir ya HABARI bila propaganda wala upendeleo. Kwa maana nyingine ni kuwa Ndugu Kibanda alikuwa akihariri habari ambazo zinasema ukweli wa mazuri ya chama cha Mapinduzi na kuimwagia sifa kwa mipango yake ya kuiletea nchi Maendeleo lakini pia kwa kasi ya utekelezaji wa Ilani ya chama.
Baada ya Uamuzi huo wa Kibanda kuhamia New Habari Corporation na kuiandika habari zenye mlengwa wa Kati, wakuu wa Free media walimuita ili kufanya nae mazungumzo ya kumtaka kurejea katika kampuni yao, hasa baada ya Gazeti lao la Tanzania Daima kuanza kupoteza dira na kuandika habari ambazo hazina mvuto hivyo kulifanya kushuka kimauzo na kipropaganda dhidi ya Chama Cha Mapinduzi. Lakini Kibanda aliendelea kukataa kurudi na kuwa pamoja na viongozi hao wasiojua nini maana ya kuwa kiongozi, hawaheshimu taaluma wala hawataki kuruhusu fikra huru kuchukua nafasi katika chama na Kampuni zao.
Kulingana na ukweli huo wa kuwepo kwa uhasama baina ya Mhariri Huyu makini na mabosi wake wa kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi hapo awali, hisia zangu zinanipelekea kuamini kuwa yawezekana kabisa mpango huu wa kumvamia, kumshambulia na kuhatarisha maisha yake umeratibiwa na viongozi hao ambao hali nao sahani moja, na ndiyo asili ya swali JE, KIBANDA ni muhanga wa alichokiandika..?
 
Tunajua kuwa mmetumwa humu jf ili kuhamisha ukweli wa serikali kuwadhuru wanahabari, watanzania tunatambua kuwa usalama wa wanahabari yapo hatarini kwa kuweka wazi uozo wa watawala
 
nimekuwa na muheshimu kibanda katika mtamo wake wa kisiasa kitambo sana. ni kati ya watu wachache waliyo kataa kabisa kumfagilia kikwete tokea aingie madarakani, alikuwa na maono ya mbali ambayo, sisi ndiyo leo tuna kuja kugundua tuli lamba bad card "garasa/ garasha to hell...kibanda alikubwa na kesi ya ya blau blah. Tanzania daima. kibada ni binadamu CCm wana mwambia inabidi awatumikie ili waipotezee kesi, kibadnda anakubali si kutoka rohoni lakini inabidi. kibanda ni mwana mapinduzi anajua jinsi nchi hii inavyo liwa na wachache. katika kukubali kwame anajikuta mwili umeungana na mafisadi kujihepusha na hukumu lakini roho inaumi, na hapo ndiyo matatizo yanapo anza baada ya mafisadi kugundua huyu bwana si mwenzetu...wasemakweli watatishwa, wata bembelezwa kuhogwa. na hata kuuwawa ili mradi uandike wao wana chotaka
nafikiri kwa mtu ambaye ameisoma hiyo makala vizuri between lines ataona hichi kitu hapo 'ilikuwa imekaa kimahaba' mno!!in view ya kaliba ya Kibanda unaona kabisa kama kuna kitu kinampush aandike kwa mtindo aloandika!analysis ya WOWOWO ilikuwa fupi lakini ukiitafakari kwa umakini utaona hii kitu-the guy(Kibanda) wasnt writing this article akiwa na free mind!!
All in all tunamwombea kheri na quick recovery!
Kuwakamata culprits wa hiyo incident,i dont expect much from this gvt,the police etc!
 
CCM Mnahangaika sana.Mwangosi chadema wamemuua,Ulimboka Chadema wamemtesa,Walimu wakigoma chadema,madaktari wakigoma chadema,polisi kuua morogoro chadema wameua,kupigwa risasi mwandishi wa tanzania daima na Majira pia ni chadema.Imebaki kusema mimba za wake zenu wamepewa na chadema...Silly you

Mkuu Nakusalut!! Ni ukweli usiopingika kwamba nchi hii sasa hivi imekuwa kama inaongozwa na Chadema!

Likitokea la Kutokea Chadema,hawatakawia kusema kesho kwamba hata Wake zao kuwa Wajawazito ni Chadema omewapiga Mimba!
Hata Mama zao kuolewa na Masikini,na Wao Kuzaliwa Masikini pia ni Chadema!!

MAGAMBA bwana kwa NGONJERA hawajambo.Serikali ni ya CCM, Polisi ni CCM, Usalama wa Taifa ni CCM! Sasa kama chadema wanaweza kufanya mambo haya na wasishugulikiwe, basi kuna haja ya CCM na Vibaraka wake kukaa Pembeni na Kuichia CDM, iongoze Dolla,kwani Serikali ya CCM imeshindwa!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 
Dentist wa Tembo, kweli anatisha...... Rangi ya nguo zake pia ni poa sana.

images
 
Ukiacha kufikiri kwa kutumia kichwa banaa!!!Michoshoooooooooooo!!!.Na yaelekea masaburi yanakuwashaUnatumalizia charge umeme wenyewe mgao.
 
Mmmmh inawezekana mtu yeyote akimua kutengeneza story inaweza kushabikiwa na wa2 hata kama story ya kufikirika(fiction).sijui kama tutafika kwa njia ya kudivert attention za wa2 kwenye matukio makubwa.mind you,you can not fool all people at a time.Mungu ibariki Tanzania na wa2 wake.
Mkulu angalia vizuri hii thread kimantiki ukianzia na alieianzisha na wenye michango ya kukubaliana naye, utakuta ni wale wale waanzilish wa thread za namna hii zilizoanzishwa kipindi cha marehemu Mwangosi na kupigwa kwa Ulimboka!. Kuna id zingine huwa zinaibuka janvini kipindi cha matukio kama haya binafsi nazitambua!
 
Kuleta hapa jamvini si suluhu la pekee bali mnatakiwa muhisaidie paolisi kwa kupeleka ushahidi wenu hili ufanyiwe kazi ikiwezekana tukutane mahakamani!
yap, lakini vitu kama hivi vinaweza kutoa dira. Mleta mada anastahili sifa na hata wengine wenye hints kama hizi waziweke jamvini ili tuweze sasa kuepukana na propaganda za hapa na pale.
 
Well said!

Mkulu angalia vizuri hii thread kimantiki ukianzia na alieianzisha na wenye michango ya kukubaliana naye, utakuta ni wale wale waanzilish wa thread za namna hii zilizoanzishwa kipindi cha marehemu Mwangosi na kupigwa kwa Ulimboka!. Kuna id zingine huwa zinaibuka janvini kipindi cha matukio kama haya binafsi nazitambua!
 
Kibanda ameumizwa Ccm wanatake oportunity, huku ni kukosa ubinadamu..nakumbuka ile issue ya Chacha Wangwe walifanya hayahaya, tunashukuru Mungu wanatarime waliwadhalilisha vibaya sana na uchafu wao ukafia hapo
 
Wewe thatha haya unayoyaleta yanahitaji Ushahidi usio na shaka hata chembe , ukiambiwa thibitisha hutaweza , Hizi ID'S fake zisitufanye kuandika upuuzi wowote tu , ni kweli Jf tupo huru kuandika chochote , lakini siyo uongo , Mbowe amdhuru Kibanda kwa lipi ? Mbona pamoja na Kibanda kuondoka Tz Daima linaendelea ? Uzushi kama huu ndiyo unasababisha Jf inadharauliwa , hivi baada ya uchunguzi Ikibainika kwamba ndugu thatha umeleta Uzushi tukufanyeje ? Unayajua yaliyomkuta Le Mutuz na uzushi kama huu ?
 
Huyo thatha hajui maana ya hayo unayo muandikia na hajui mdahara yake!
Wewe thatha haya unayoyaleta yanahitaji Ushahidi usio na shaka hata chembe , ukiambiwa thibitisha hutaweza , Hizi ID'S fake zisitufanye kuandika upuuzi wowote tu , ni kweli Jf tupo huru kuandika chochote , lakini siyo uongo , Mbowe amdhuru Kibanda kwa lipi ? Mbona pamoja na Kibanda kuondoka Tz Daima linaendelea ? Uzushi kama huu ndiyo unasababisha Jf inadharauliwa , hivi baada ya uchunguzi Ikibainika kwamba ndugu thatha umeleta Uzushi tukufanyeje ? Unayajua yaliyomkuta Le Mutuz na uzushi kama huu ?
 
Back
Top Bottom