Anasema alipolazwa hospitalini nchini Afrika Kusini serikali ilimtuma mtu mmoja kwenda kuona maendeleo yake. Uongozi wa hospitali uliamua kumficha ili kunusuru maisha yake.
jamani maumivu ya kung'olewa kucha na meno na kutobolewa jicho bila ganzi si mchezo. Anasema sasa ana ujasiri upi? Anajua fika kuwa wahusika wako juu ya sheria wakimtaka wanampata. Hii nchi jamani!!
kumbe alikuwa anaficha?????hili ndilo tatizo la wanahabari wa tanzania.wanaficha habari muhimu.BADILIKENI SASA.
Kama Dr. Ulimboka angeweka wazi yaliyompata, tendo hili lisingerudia kwa Mh Kibanda. Kauli ya Dr. Ulimboka ya kumwachia Mungu ni UWOGA au USALITI. Basi wale wahisani waliochanga kugharamia matibabu yake nao wangelisema "wanamwachia Mungu" ingekuwaje. M/Mungu anapenda kuwa mkweli na uwazi, sio kufichaficha. Ulimboka ni Adui wa harakati na ni Msaliti kama Mbatia na Lyatonga
Ngoja kibanda alipwe nae atamuachia Mungu
Anaogopa kutaja jina la hiyo "taasisi nyeti..." anaogopa kutaja huyo aliyeambiwa ajitahadharishe nae, anaogopa kutaja chochote halafu anatuambia kuanzia sasa atakuwa jasiri, ataandika kila kitu. Ridiculous.na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili.
Aliambiwa jambo ajiangalie wapi na mtu huyo....
gari limepaki la taasisi moja
Amekubali hali iliyompata kama chachu ya kusimamia anayoyaamini. Hata alipokuwa anasita sasa hatakuwa mwoga.
Kibanda is quite bright man
Waharifu walitumia utaalam katika kujeruhi ili kumuangamiza kibanda.
Anasema matukio mengi yalitangulia ya kuwadhuru waandishi wa habari kabla yake yeye.
Kibanda anasema alipata kutahadharishwa na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili. Aliambiwa jambo ajiangalie wapi na mtu huyo. Aliambiwa awe makini na getini na mahali anapokunywa.
Wiki 2 kabla aliona gari limepaki la taasisi moja na gari lilimfuata
Kibanda anasema viongozi wengi wa serikali wamekuwa na jitihada za kukwepesha ukweli. Amewaomba wanahabari wasonge mbele ushindi utapatikana. Vyombo vya dola vilihusika kupotesha ukweli.
Amekubali hali iliyompata kama chachu ya kusimamia anayoyaamini. Hata alipokuwa anasita sasa hatakuwa mwoga. Mambo mengi alikuwa anayafikiria sana. Lakini kwa sasa amejijua namna alivyo jasiri tofauti na awali. Hali ya afya yake madaktari walimuona ni jasiri.
Anasema lugha za kishabiki ziliandikwa wengine wakiwahusisha wanasiasa.
Ulimwengu anamuuliza kuhusu upelelezi ulipofikia:
Amepata mawasiliano ya viongozi wa vyombo vya dola kuwa wanalifuatilia hata viongozi wa ulinzi wa usalama wastaafu wanafuatilia. Kitu hiki kinampa faraja. Wameliangalia kama maisha binafsi ya kibanda. Kuna afisa wa jamii alitumwa kumhoji afrika kusini.
Alisema wazi kuwa tukio hilo ni la uhalifu na aliamini kuwa aliumizwa kwa sababu ya msimamo wake kwa masuala mbalimbali kitaifa. Lakini pia alitoa ruhusa kwa vyombo vya dola kufuatia maeneo mengine.
Kibanda akiri kuwa kuna watu wananguvu ambao wanashughulika na jambo hili ili ukweli usibainike ndio maana hata leo hakuna hata mmoja amekamatwa.
Hapa naanza kupata kapicha kidogo
1. Mahusiano ya Mwigulu na Rudovick,
2. Mwigulu kusema anaomkanda unaoonyesha Viongozi wa CDM wakipanga mauaji,
3. Siku Kibanda anatekwa naye Rudovick kusingizia katekwa pia.
4. Mwigulu kumtumia Rudovick kumrecord Lwakatare
5. Kukamatwa kwa Lwakatare kuhusishwa na kesi ya kutaka kuteka na kumzuru Denis
Nahitimisha kwa kusema wahusika wameishaanza kuanikwa - Rudovick, Mwigulu, Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya usalama Lengo ni kuihusisha CHADEMA na matukio yote haya lakini kwa maneno haya ya Kibanda ukweli unaanza kujulikana na ndo maana CDM wamekaa mbali sana na Rudovick.
Huyu jamaa Kibanda ni mwongo ama ni mwoga wa ajabu! NashangaA amepataje ujasiri wa kuongea kwenye kipindi cha Ulimwengu ambaye kwa kawaida huwa mtafuta uwazi. Kibanada hajasema lolote la maana zaidi ya kuelezea mkongoto alioupata! Hoja ya kwamba anahisi ni nani aliyempanga kumjeruhi hakuifafanua vizuri zaidi ya kuonyesha hisia za hapa na pale. Zaidi ya hapo Ukizingatia ajira yake, na mustakabali wa matamanio yake, huyu mtu ni mwongo tu! Bogus!
kubenea alisubiri sana uchunguzi mpaka leo, mtu akijua unajua ukweli atakumaliza kabla hujasema huo ukweli...
Hata mimi nimemkubali, hayuko kisiasa.