Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Absalom Kibanda: Sasa sitaogopa kitu na sina cha kupoteza, nitafichua kila kitu

Anasema alipolazwa hospitalini nchini Afrika Kusini serikali ilimtuma mtu mmoja kwenda kuona maendeleo yake. Uongozi wa hospitali uliamua kumficha ili kunusuru maisha yake.

Serikali ilimtuma mtu! Basi mchawi si anajulikana kwanini asiwe wazitu sasa kulikoni anavyoumauma maneno na mwisho wake watamtambarizia mbali kabla ya kufunguka, ama anataka apate shavu kama la ulimboka?
 
jamani maumivu ya kung'olewa kucha na meno na kutobolewa jicho bila ganzi si mchezo. Anasema sasa ana ujasiri upi? Anajua fika kuwa wahusika wako juu ya sheria wakimtaka wanampata. Hii nchi jamani!!

Sasa si awaani kabla hawajamtaka na kumpata?
 
kumbe alikuwa anaficha?????hili ndilo tatizo la wanahabari wa tanzania.wanaficha habari muhimu.BADILIKENI SASA.

Na kuanika za ovyo na zisizokuwa na manufaa kwetu, mara cjui owoya na nani cjui wafumwa live ujinga mtupu mimi na yule watajifunza nini hapo sasa
 
Kama Dr. Ulimboka angeweka wazi yaliyompata, tendo hili lisingerudia kwa Mh Kibanda. Kauli ya Dr. Ulimboka ya kumwachia Mungu ni UWOGA au USALITI. Basi wale wahisani waliochanga kugharamia matibabu yake nao wangelisema "wanamwachia Mungu" ingekuwaje. M/Mungu anapenda kuwa mkweli na uwazi, sio kufichaficha. Ulimboka ni Adui wa harakati na ni Msaliti kama Mbatia na Lyatonga

Ngoja kibanda alipwe nae atamuachia Mungu
 
Ulimboka alisalitiwa na madaktari na yeye akaamua kula chake na kusaliti wengine
 
Bwana ABSALOM KIBANDA aliyasema hayo jana wakati anajibu swali na mmoja wa watu waliokuwa wakifuatilia kipindi cha JENERALI ULIMWENGU ON MONDAY kinachorushwa na kituo cha television cha CHANNEL TEN.

Mwananchi huyo alimshambulia yeye na watu wengine kama akina STEPHEN ULIMBOKA kuwa wamekuwa wakiahidi kufunguka na kusema ukweli lakini wanapopewa nafasi ya kusema hawasemi chochote cha maana.

Aidha Bwana KIBANDA alivishukuru vyombo vya dola na hasa jeshi la POLISI, viongozi binafsi wa dola waliostaafu na walioko kazini kwa jinsi ambavyo wako karibu naye kusaiidia kuupata ukweli wa tukio lililomkumba.

Mytake: Binafsi nilifurahishwa na majibu ya Bwana KIBANDA kwani alionesha ukomavu yeye kama Mwandishi wa habari. Hakuna sababu yoyote ya yeye kuanza kulalalmikia vyombo vya dola, watu fulani fulani ama kikundi cha watu wakati hana uhakika wa nani hasa anahusika na tukio hili.

Watu wengine waige mfano wa KIBANDA wa kuheshimu na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pindi wanapofikwa na matukio kama haya badala ya kuingiza chuki, siasa na kuepuka kutumiwa na watu kwa ajili ya kujipatia umaarufu katika jamii kisiasa, kijamii na hata kiuchumi.
 
na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili.

Aliambiwa jambo ajiangalie wapi na mtu huyo....

gari limepaki la taasisi moja

Amekubali hali iliyompata kama chachu ya kusimamia anayoyaamini. Hata alipokuwa anasita sasa hatakuwa mwoga.
Anaogopa kutaja jina la hiyo "taasisi nyeti..." anaogopa kutaja huyo aliyeambiwa ajitahadharishe nae, anaogopa kutaja chochote halafu anatuambia kuanzia sasa atakuwa jasiri, ataandika kila kitu. Ridiculous.
 
Ngoja apigwe mwingine kwa unafki huu wa kibanda na ulimboka mptapigwa tu waandishi wa habari
 
Waharifu walitumia utaalam katika kujeruhi ili kumuangamiza kibanda.
Anasema matukio mengi yalitangulia ya kuwadhuru waandishi wa habari kabla yake yeye.

Kibanda anasema alipata kutahadharishwa na mtu toka taasisi nyeti ya taifa hili. Aliambiwa jambo ajiangalie wapi na mtu huyo. Aliambiwa awe makini na getini na mahali anapokunywa.

Wiki 2 kabla aliona gari limepaki la taasisi moja na gari lilimfuata

Kibanda anasema viongozi wengi wa serikali wamekuwa na jitihada za kukwepesha ukweli. Amewaomba wanahabari wasonge mbele ushindi utapatikana. Vyombo vya dola vilihusika kupotesha ukweli.

Amekubali hali iliyompata kama chachu ya kusimamia anayoyaamini. Hata alipokuwa anasita sasa hatakuwa mwoga. Mambo mengi alikuwa anayafikiria sana. Lakini kwa sasa amejijua namna alivyo jasiri tofauti na awali. Hali ya afya yake madaktari walimuona ni jasiri.
Anasema lugha za kishabiki ziliandikwa wengine wakiwahusisha wanasiasa.


Ulimwengu anamuuliza kuhusu upelelezi ulipofikia:
Amepata mawasiliano ya viongozi wa vyombo vya dola kuwa wanalifuatilia hata viongozi wa ulinzi wa usalama wastaafu wanafuatilia. Kitu hiki kinampa faraja. Wameliangalia kama maisha binafsi ya kibanda. Kuna afisa wa jamii alitumwa kumhoji afrika kusini.
Alisema wazi kuwa tukio hilo ni la uhalifu na aliamini kuwa aliumizwa kwa sababu ya msimamo wake kwa masuala mbalimbali kitaifa. Lakini pia alitoa ruhusa kwa vyombo vya dola kufuatia maeneo mengine.

Kibanda akiri kuwa kuna watu wananguvu ambao wanashughulika na jambo hili ili ukweli usibainike ndio maana hata leo hakuna hata mmoja amekamatwa.

Vipi kuhusiana na Kujiondoa Free Media ameongelea?
 
Hapa naanza kupata kapicha kidogo
1. Mahusiano ya Mwigulu na Rudovick,
2. Mwigulu kusema anaomkanda unaoonyesha Viongozi wa CDM wakipanga mauaji,
3. Siku Kibanda anatekwa naye Rudovick kusingizia katekwa pia.
4. Mwigulu kumtumia Rudovick kumrecord Lwakatare
5. Kukamatwa kwa Lwakatare kuhusishwa na kesi ya kutaka kuteka na kumzuru Denis

Nahitimisha kwa kusema wahusika wameishaanza kuanikwa - Rudovick, Mwigulu, Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya usalama Lengo ni kuihusisha CHADEMA na matukio yote haya lakini kwa maneno haya ya Kibanda ukweli unaanza kujulikana na ndo maana CDM wamekaa mbali sana na Rudovick.

umeiona na kuisikiliza vzr ile video ya lwakatare? Kaisikilize km utaongea haya tena
 
Huyu jamaa Kibanda ni mwongo ama ni mwoga wa ajabu! NashangaA amepataje ujasiri wa kuongea kwenye kipindi cha Ulimwengu ambaye kwa kawaida huwa mtafuta uwazi. Kibanada hajasema lolote la maana zaidi ya kuelezea mkongoto alioupata! Hoja ya kwamba anahisi ni nani aliyempanga kumjeruhi hakuifafanua vizuri zaidi ya kuonyesha hisia za hapa na pale. Zaidi ya hapo Ukizingatia ajira yake, na mustakabali wa matamanio yake, huyu mtu ni mwongo tu! Bogus!

mawazo yako yana mapungufu sana, kama unasema Kibanda ni mwongo tupe ukweli unaoujua wewe.
 
Hivi hawa watu wakishang'olewa meno na kucha na akina Ramadhani Ighondi (read TISS) Pia wanakuwa wameng'olewa AKILI?!

Ni mambo ya ajabu sana akina Harrison Mwakyembe, Dr. Ulimboka na sasa huyu Kibanda wote walitishia Nyau kwamba watasema kila kitu. Lakini walipopewa fursa ya kusema kama huyu Kibanda wote wameishia kusema ETI WANAMUACHIA MUNGU.

Kama Kibanda anafikiri hao wabaya wake wamelala, he is absolutely wrong. Tena kwa matamshi yake hayo ya CH 10 ndiyo amaweka MAISHA YAKE REHANI.
 
Tatizo hawa nao ni awanafi itakuaje mpaka leo amekalia ukweli wakati anajua yeye ni mtu muhimu katika mustakabali wa hali ya mabo na migogoro ya kisiasa inayoendelea nchini mwetu?

MY take: Watanzania tunataka watu wenye dhamira safi na maendeleo ya kweli ya demokrasia ya taifa hili wawe wawazi ili watutoe wasiwasi sisi wananchi kutokana na hofu tunayopandikizwa na wanasiasa kama
mwigulu
 
kubenea alisubiri sana uchunguzi mpaka leo, mtu akijua unajua ukweli atakumaliza kabla hujasema huo ukweli...


You are damn right; na usikute hata ulimboka naye amekuwa contained kwa technique hiyo-hiyo ya kusubirishwa kitu. Kesi ya Ulimboka kwa mfano ndo ipo obvious kabisa kama jua kutoka Mashariki. Somebody got terribly hurt kwenye department ile and that's all you'd need ku-prove involvment. Call them to the parade, mwenye kovu pale mahala ndo huyo aligongwa.... eti intelligence.; stupid fools. Nyerere alikuwa ana-contain political challenge, but he was very careful with the human body. Waseme tu ukweli taifa lijue.
 
Back
Top Bottom