AC Milan vs Man UTD...

AC Milan vs Man UTD...

ha ha, BJ uzuri wako hukimbii matokeo...hivi CHELSEA wanacheza lini vile na Mourinho? Masa huugua mechi hizi za ECL!

Dah, kwa mtaji huu Mshafuzu nyie Semis,...hawa AC wamekuwa 'kiyoyozi' kweli leo.

Si unajua hata nikikimbia nitarudi,inauma kufungwa ila nikumuv on!..
Chelse hao ni J5 ijayo, Masa ajiandae na yeye ajiandae na wapinzani)):
Umenichekesha eti AC wamekuwa kiyoyozi,kweli kimepuliza ipasavyo....I'm happy for Man!..
 
Phewwwwwwwwwwwwwwwwwwwwww.........wat a match!, hawa hawana lao OT.

Tunawataka Barca sasa,
 
...ha ha ha....
mtihani huo, AC wanaweza kabisa kuwafunga 2 na zaidi mechi ijayo.

Ahhh mkubwa, na wewe wayasema hayo kweli?, kwa lepi na lepi?, OT?, save ur energy pal. Embu tuleteeni Barca, safarii hii twawataka mapemaaaaa!
 
Phewwwwwwwwwwwwwwwwwwwwww.........wat a match!, hawa hawana lao OT.

Tunawataka Barca sasa,

Imagine tungefungwa🙂pasingekalika...Bora mechi imeisha kweli, mwanzilishi wa thread naona kakosa hata neno la kiswahili kuandika mana sasa ananena kitaliano aliko!..Man Utd Huree!!!!
 
United next match inabidi wafanye kazi ya ziada!!
 
Nina wasiwasi twaweza kuwa tumempoteza Gang Chomba ndani ya JF maana ukiangalia post za kwanza za thread hii alivoanza kwa mbwembwe na majisifu juu ya ACM mhhhhhhhh....Forza Milan
 
_47316137_rooneyfirst_getty.jpg


Chomba aliyekuua huyu hapa.
 
Ahhh mkubwa, na wewe wayasema hayo kweli?, kwa lepi na lepi?, OT?, save ur energy pal. Embu tuleteeni Barca, safarii hii twawataka mapemaaaaa!

Hongereni sana kwa ushindi watani...Ila game ijayo inabidi mkomae hasa...Hawa jamaa wanaweza kubadilisha KIBAO pale Old T......(Kwa defense ya dizaini ya Rio lolote lawezekana)
 
AC Milan vs Man UTD...
Gang Chomba 4th February 2010, 02:18 AM
UWANJA - Sansiro
MAHALI - Milan
WATAZAMAJI - 85,700
ULIANZA KUJENGWA - 1925
KUFUNGULIWA RASMI - 19 SEP: 1926
BARABARA YA KUINGILIA - PICCOLONINI.

Siku chache zimebaki kabla ulimwengu kushuhudia tena mtanange ambao miaka kadhaa iliyopita tulishuhudia timu moja ikitupwa nje ya mashindano na nyingine kupeta kama ilivyo ada.

Huu ni mpambano kati ya AC Milan na klabu ya Manchester UTD.
Mpambano huu unazidi kuvuta hisia za watu wengi ukizingatia kuwa Man UTD wanataka talaka yao kwa lazima ili wakaanzishe maisha mapya yasiyo na vipigo vya kila msimu, huku AC nao wakijipanga kuendeleza ubabe kwa wanyonge wao.

Leo niko hapa kwa ajili ya kuizungumizia timu yangu kipenzi AC Milan.
Milan kama Milan ilipoanza ligi ilionekana wazi kuwa isingemudu mikiki ya mashindano yoyote yale.

Lakini kuwa fit kwa wachezaji wake kulipelekea haraka kuaminiwa kuwa ni timu ambayo kwa msimu huu yaweza nyakuwa baadhi ya vikombe.

Hofu ya wapinzani wetu ilipanda maradufu pale AC walipotua ktk uwanja wa el Santiago Bernabeu na kuibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya timu iliyopewa nafasi ya kufanya vizuri kutokana na usajili waliofanya.

Hali hii imepelekea kuanzia kocha wa Man UTD mpk mshabiki aliye hapo Tanzania kujawa hofu huku wakiwa hawapati usingizi.

Milan ina wachezaji wenye vipaji kama uncle Seeldorf, pirlo, Beckham, Pato, nesta, Ambrosini, silva, dinho, Pippo na wengine weengi ambao mara kwa mara wamekuwa wakielewana sana wawapo uwanjani.

IVAN ''RHINO'' GENNARO GATTUSO...
huyu ni mtumishi wa klabu.
Mara kadhaa Gattuso amekuwa akiwashikisha adabu wachezaji wanaopambwa na sifa za mashabiki.
Siku hiyo Gattuso atakabidhiwa Rooney huku akipokea msaada toka kwa Beki bora wa kati Duniani Alesandro Nesta.

ANDREAS PIRLO...
hii ni Injini ya Milan.
Anasifika kwa kupoza mpira ili kuendana sawa na spidi ya Milan.
Ana pasi zenye akili na uwezo mkubwa wa kupiga mipira iliyokufa.

DAVID JOSEPH ROBERT BECKHAM...
Ttumemtaka asihangaike na kukaba siku hiyo. Bali amimine majalo yenye upako yatakayofika kwa Hitman Pato.

UNCLE SEERDOLF...
kila mtu anafahamu kuwa kadri siku zinapozidi kwenda, basi nae anazidi kuwa imara.
Kizazi chake amebaki kwenye Ramani yeye pmj na kipa Van Der Sir.

SUPER PIPPO...
Ktk washambuliaji ambao sir Alex anawachukia basi Inzaghi anaongoza.
Na kama atapewa muda wa kucheza ni wazi ukuta wa Man UTD utakuwa busy kwa kipindi choote mpk filimbi ya mwisho.

PATO & BORIELLO
Ni double snipers.
ni wauaji hatari na wenye mbinu kali.

RONALDO ''ASSIS'' de MOREIRRA...
sina cha kumzungumzia.
Ila nauliza je ni wachezaji wangapi wa Man UTD watakaojitolea kudhalilishwa na mchezaji huyu anayefananishwa kiuchezaji na wachezaji wa ligi za mbinguni?

FRANCO BARRESI, ALESANDRO COSTACURTA NA PAOLO MALDINI...
Hawa watakuwepo jukwaa kuu wakihamasisha.

Hakika Milan tuna kila sababu za ushindi, kwani tupo ktk ari na pia tuna uzoefu mkubwa ktk mashindano haya kuliko wapinzani wetu.

Milan imebeba kombe hili mara 7, wakati wagosi wao wana mara 3.

Forza Milan.
 
Only a small distance from the truth. My prediction was cut by Rafael for his easy loose of the ball. But N'way Man Utd has got what most f us prayed for....win

Hureee Man Utd for helping get a nice night.
 
Kudos! Mashetani wenzangu, shetani wa ukweli hakimbii jukwaa unless aishiwe data bundles.
Am Out!..Lol!
 
Lakini vijana wamecheza mpira mzuri sana,ila jamani ile namba ya carrick nani atacheza pale??Maana angekuwa carrick,fletcher na Scholes ingekuwa vizuri sana yaani ila sasa mmoja hayupo pale kuna pengo kidogo,ila bora katolewa carrick kuliko kutolewa fletcher
 
Mdau aliyeanzisha thread naona kaona mambo magumu kaingia mitini,Tatizo ACM wazee ni wengi sana!!
 
Mdau aliyeanzisha thread naona kaona mambo magumu kaingia mitini,Tatizo ACM wazee ni wengi sana!!

Sijakimbia sheikh lakini nina wakati mgumu sana hapa nilipo.
kuna wachezaji wa Milan wamenisononesha saaana.
hakika Milan ni timu kipenzi changu na najivunia hilo.
Ila narudia KUNA WACHEZAJI WA MILAN WAMENISONONESHA MNO.
 
Sijakimbia sheikh lakini nina wakati mgumu sana hapa nilipo.
kuna wachezaji wa Milan wamenisononesha saaana.
hakika Milan ni timu kipenzi changu na najivunia hilo.
Ila narudia KUNA WACHEZAJI WA MILAN WAMENISONONESHA MNO.

Pole Gang chomba... aka Mzee unayedai watu WANAKURUPUKA.... Heshima mbele Gang Chomba...
 
Sijakimbia sheikh lakini nina wakati mgumu sana hapa nilipo.
kuna wachezaji wa Milan wamenisononesha saaana.
hakika Milan ni timu kipenzi changu na najivunia hilo.
Ila narudia KUNA WACHEZAJI WA MILAN WAMENISONONESHA MNO.
Wachezaji gani wanaokusononesha ? Nilikua naangalia jinsi ya Jogoo alivyochinjiwa bandani mwake. Jamadani wa vita amefia nyumbani, so sad.
 
Nina wasiwasi twaweza kuwa tumempoteza Gang Chomba ndani ya JF maana ukiangalia post za kwanza za thread hii alivoanza kwa mbwembwe na majisifu juu ya ACM mhhhhhhhh....Forza Milan

Barantanda mkongwe mwenzangu nipo hai ndugu.
Ila ndo hivyo tena wanasema siku ya kufa Tembo pua zote zinaziba...
Ila kuna wachezaji milan wameniumiza sana Moyo wangu usiku huu.
 
Barantanda mkongwe mwenzangu nipo hai ndugu.
Ila ndo hivyo tena wanasema siku ya kufa Tembo pua zote zinaziba...
Ila kuna wachezaji milan wameniumiza sana Moyo wangu usiku huu.


Nani na nani mkuu!!
 
Mshaambiwa THERE IS NO COUNTRY FOR OLD MEN hamsikii...ona sasa!

Dida, cafu, maldini, stam, nesta, gatusso, pirlo, ambro, ruicosta, crespo na seedorf...

Je ktk kikosi hicho nani ambae si old men? Na unajua kuwa ktk kikosi hicho Man aliparamiwa mara ngapi?Usikurupuke.

Unachotakiwa kufahamu ni kuwa kuna wachezaji wamefungisha leo.
 
Back
Top Bottom