Wafuasi wa Lumumba ama kwa ile kukosa uelewa, au kwa makusudi tu, since Day 1 wamekuwa wakipotosha ambacho Tundu Lissu aliongea kuhusu MIGA! Au wakati mwingine inawezekana ni kutokana na tabia yetu Watanzania ya kutotafuta ukweli!
Binafsi nimekuwa nikilijadili suala la makinikia since Day 1, na kwavile nilikuwa nafuatilia sana nakumbuka vyema nini Tundu Lissu aliongea, na ninamnukuu hapa chini:-
Hiyo ndiyo hoja ya Lissu... kwamba, kama kweli Serikali ya Magufuli ilikusudia kupambana na Acacia, basi walitakiwa kwanza wajitoe kwenye mkataba wa MIGA!
Ushauri sawa na huo wa TL ulikuja tena kutolewa na Dr. Rugemeleza Nshala mbele ya Wabunge walipokuwa wanatafuta maoni ya wadai wakati wa utungwaji wa sheria mpya ya madini.
Gazeti la the Citizen linatujuza
😛ia the Citizen wanatukumbusha kwamba, Dr. Nshala ni Mtanzania wa pili kutoa ushauri kama huo huku wa kwanza akiwa ni TL:-Kwa maajabu ya wale waliofuatilia suala la umakini, watu wakapotosha na kudai TL amesema tukipambana na Acacia, watatupeleka MIGA, na huu ndo umekuwa wimbo wa wana-CCM na wafuasi wa serikali!
Busara ya TL kushauri kujitoa MIGA unaweza kuiona kupitia tovuti ya MIGA,
hivi ndivyo wanasema:-Hapo wanaongea wazi ni namna gani pamoja na mambo mengine, wana jukumu la kulinda uwekezaji dhidi ya maamuzi ya serikali!
Sasa basi, hoja ya TL ilikuwa ni kwamba, tukishavurugana na Acacia ,watakachofanya wao ni kile ambacho kinafanywa na kampuni zingine... yaani kukimbilia Mahakamani, au MIGA!
Lakini kama kweli umeamua kupambana na hawa jamaa, unachotakiwa ni kuchomoa betri kwa kujitoa MIGA ili wasiwe na kwa kukimbilia zaidi ya kwenda kwenye mahakama zetu wenyewe... yaani mahakama zile zile zinazoamua ma-DED wanastahili kusimamia uchaguzi ambao mmoja wa washiriki ni mwajiriwa wake mwenyewe!!!
Kwa maana nyingine, ukishajitoa MIGA maana yake ni kwamba unakuwa huzitambui mahakama zao! Ni kama United States asivyoitambua International Criminal Court, matokeo yake pamoja na uhalifu wote wa kivita wanaoufanya duniani kote, huwezi kumpeleka Mmarekani ICC .
Maajabu makubwa zaidi ya taifa hili, badala ya kuiangalia hoja ya TL Critically, watu wale wale wanaojiona ndio wazalendo zaidi, wakaona mtu kama TL anastahli kuuawa mara moja... na wafuasi wa CCM na serikali yake wamekuwa wakiirudia kauli hii mara kwa mara!!!!
Je, kumpuuza TL kumetugharimu kama taifa?!
Serikali na watetezi wataendelea kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe lakini ukweli ni kwamba imetugharimu kama taifa!
Sote tumeshuhudia danadana za Acacia... watetezi wa serikali wasichofahamu ni kwamba, danadana zote zile ni kwa sababu walifahamu maji yakiwazidi shingo, wangekimbilia mahakamani ambako katu tusingetoka.
Na kwa Mtanzania yeyote anayekejeli kauli hiyo ya TL, kwa hakika anatakiwa kujitafakari mara mbili... anatakiwa kujitafakari kwa sababu sisi ni victim wa hizi mahakama, hususani kupitia IPTL!
Sote sisi tunakumbuka kushikiliwa kwa Bombardier kwa wiki kadhaa kule Canada kutokana na maamuzi yaliyotolewa na mahakama za aina hii!!
Hivyo basi, ili kujilinda tusipelekwe kwenye mahakama kama hizi ambazo kuchomoka ni nadra sana, ndipo TL akasema ukitaka kupambana na hawa watu, basi jitoe MIGA lakini sio kwamba tukipamba na Acacia, wanatupeleka mahakamani!!!
Je, kwanini Acacia Hawajatupeleka MIGA?
Kwa kifupi ni kwamba, Acacia hawakuwa na sababu ya kutupeleka MIGA kwa sababu serikali imepita njia ambayo ni nafuu maradufu kwa Acacia!
Kuweka kumbukumbu sawa, wakati Profesa Orosso akiwakilisha Ripoti ya Pili, alitoa takwimu ya pesa ambayo serikali ilipoteza kama mapato! Prof. Orosso na timu yake waliweka makadirioo ya kiwango cha chini kabisa ambacho serikali ilipoteza, na kiwango cha juu kabisa!
Tuachane na kiwango cha juu kabisa, Profesa Orosso anatujuza, na
ripoti kamili inapatikana tovuti ya Ikulu:-Hicho ndicho kiwango cha chini kabisa... na ukichanganya na adhabu (ya kuchelewesha kulipa kodi), jumla ndo ile figure maarufu ya TRilioni 450!!
Sasa hebu tujiulize... Uchunguzi uliofanywa na akina Prof Mruma na mwenzake Prof Orosso (pamoja na timu ya watu wa TRA), ilionesha Acacia wamekwepa kulipa Sh. 68 kwa miaka 17. Leo hii serikali imekubali kulipwa Sh. 700 Billion... sasa hata kama wewe ndo ungekuwa Acacia, ungeenda MIGA kufanya nini?!
Na kama ilivyo kwa mahakama zingine, kesi za MIGA zinachukua miaka na miaka!! Sasa kwanini ukae miaka yote hayo huku biashara ikiendelea kuathirika kwa kushindwa kusafirisha makinikia?!
Sasa wakati Wafuasi wa CCM na serikali yake wakiendelea kumkejeli TL kwamba mbona hao Acacia hawajaenda MIGA, jibu ndo hilo hapo! Hawajaenda kwa sababu sisi ndio tumeliwa! Tumekubali kuchukua Sh. 700 Billion out of 68 Trillion!!!!
NOTE:
Moderator punguzeni kasi ya kuunganisha threads bila sababu za msingi eti kisa tu kuna baadhi ya keywords zinafanana!!! Kuandika haya mambo it takes time... so, it sucks mtu unapoteza saa moja na ushee kuandika thread, unakuja next time, huoni kwa sababu imeunganishwa na thread nyingine!