Mkuu chige naomba maoni yako kuhusu hizi initiative zote za serikali ya JPM,
1:Je kuna positive outcome yoyote iliyopatikana au itakayopatikana au serikali ingekaa tu kimya na kuendelea as usual na Accacia?
Uncle Magu did the right thing but poor approach was applied! Positive outcome, mosi ni ule uwezekano wa kulipwa zile USD 300M kwa sababu kama sio hiyo initiative, hizo 300M zisingepatikana!
Pili, sio Acacia peke yake bali hata kampuni zingine za madini (in short, WOTE NI WEZI TU) nadhani watakuwa more careful wanavyofanya wizi wao! Kwa maana nyingine, ule wizi wa kirahisi rahisi kwa sasa watauweka pending!
Tatu, ingawaje basically suala la 16% halina uhusiano wa moja kwa moja na Acacia, kutikiswa kwao kumewafanya Acacia waridhie suala la 16% bila kupinga pinga! Walilazimika kufanya hivyo kwa sababu Barrick walitaka kujionesha wao ni mtoto mwema ambae yupo tayari ku-comply na sheria za nchi!
So, it's a very good move! Binafsi mambo mengi huwa natofautiana na Magu kutokana na approach zake tu!
Hapo juu nimesema alitumia poor approach kwa sababu kazi ile isingefanyika kwa mihemuko, Acacia wangekuwa cornered na hatimae kuwa na one of the two options... to pay more... more than ile 300M ambayo wanatarajia kutoa, au kufungasha virago!
Na kama wangefungasha virago, tungekuwa na basis ya kuwafikisha hata kwenye mahakama za kimataifa kwa sababu, endapo uchunguzi ule tungeufanya kiweledi zaidi, basi am very sure ungetoa matokeo ambayo yangeweza kuwa na nguvu za kisheria dhidi ya Acacia.
Kosa kubwa ambalo tulifanya ni kufanya utafiti ule peke yetu bila kuhusisha upande wa Acacia! Matokeo yake, wakagoma kukubali matokeo ya utafiti ule, and of course, walikuwa na hoja ya kutokukubali!!
2:Je ushauri wa TL alioutoa ungefuatwa je kungekuwa na matokeo bora zaidi ya haya yaliyofikiwa?
Ungefuatwa with a caution, am certain ungetoa matokeo bora zaidi! Nimesema ungefuatwa with caution kwa sababu TL ni Mwanasiasa. Ingawaje ushauri wake ulikuwa ni mzuri na haukuwa wa kisiasa, lakini pia ni ushauri ambao ulipaswa kuchukuliwa kwa umakini kwa sababu kinyume chake, unge-backfire! Na endapo unge-backfire, TL yule yule ambae alitoa huo ushauri, angeanza tena kuwa-stab back!
3:Je report za Ossoro na Mruma ni kweli zilikuwa proffessional rubbish kama alivyosema TL? Kwa maoni yangu mimi zile report hasa ya Ossoro(economical ) ndiyo ili-trigger haya majadiliano na for sure i can say it was the good move by our government.
Nawasilisha mkuu
Hili wala sitapepesa macho... YES, IT'S PROFESSIONAL RUBBISH!
Naona uvivu kutafuta post zangu za ile siku Professor Mruma anawasilisha ile ripoti! The very same day, nilizungumza hapa kwamba hizi takwimu ni kiroja!! Na wala sikutumia nguvu kugundua "rubbishness" ya zile takwimu!
Nilijumlisha tu figures za dhahabu alizokuwa anasoma Professor Mruma kwa kila kontena, nikazidhisha mara idadi ya makontena ambayo yaliwepo, nikazidisha tena kwa idadi ya makontena yanayopatikana mwaka mzima... nikapata idadi ya dhahabu inayotokana na makinikia PEKE YAKE! '
Idadi hiyo nikajumlisha na dhahabu isiyotokana na makinikia, nikajumlisha na dhahabu inayochombwa na kampuni zingine zote... jibu nililokuja kupata nikakuta Tanzania sio tu tunawazidi Afrika Kusini kwa dhahabu tunayozalisha bali tunazipita hata zile largest gold producers kama Russia, Australia, China and USA!
Available geological data on gold doesn't support Mruma's Findings!!!
Kuhusu ni Ripoti ya Ossoro ndiyo ili-trigger yale majadiliano ni kweli, lakini kama ni sifa anayestahili sio Ossoro bali Mruma kwa sababu Ossoro na timu yake walichofanya ni ku-monetize tu zile takwimu za Mruma! Hata hivyo, Mruma kamfanya Ossoro aonekane kituko kwa sababu ni figures za Mruma ndizo after Ossoro's economic analysis, zikaja takwimu zinaonesha "a sister company" Acacia is much bigger kuliko a parent company iliyokuwa na Market Cap ya less than USD 40B.
Ingawaje hili watu wanalichukulia kirahisi rahisi tu kwamba lazima utengeneze figures za kutisha ili uwabananishe vizuri lakini ukweli ni kwamba, mbele ya watalaamu Tanzania tulionekana inawezekana ni kweli tunaibiwa lakini hatujui tunachoibiwa hasa ni nini!!
It's like unampeleka Young Killer mahakamani kwamba amekuibia gunia la mchele lenye uzito wa kilo 200 halafu unaulizwa kaibaje ibaje, unasema alijitishwa akakimbia nalo!!!