Acheni kupotosha alichokuwa amesema Tundu Lissu kuhusu Acacia na MIGA

Na ninataka kufuatilia nikipata hiyo nafasi manake I doubt kama hata huo wakati wa Mkapa tulikuwa tunaweza ku-finance budget yetu kwa hiyo 80%! Nakumbuka moja ya mambo ambayo Mzee wa Msoga alikuwa akijitapa ni kupunguza pengo la utegemezi wa bajeti! Na kwa kumbukumbu zangu, hadi Mkapa anatoka madarakani, at least 40% ya bajeti yetu ilikuwa donor funded, but don't quote me... I'll confirm it next time!
Huo ulikuwa wimbo, enzi za Ukapa, kwamba tunalipa madeni, tunafunga mikanda, ikaundwa TRA tukawa tunakusanya kodi, wakaja na NIHF pilot. Na tukaambiwa tulisamehewa sehemu kubwa ya deni la taifa kupitia Oxfam na budget yetu ikawa imepunguza utegemezi kutoka kwa donor contries na ikawa inajitegemea up to 80%, sasa hapo ndio sielewi lini tumerudi nyuma mpaka 30 to 45%, and how do we fund our own mega projects at that level of dependence in our budget?! Na hili tunadanganywa?
 
Suala la msingi siyo kutoa muda, suala la msingi ni kila mtanzania mwenye uelewa kuleta hoja mezani ili kwanza watanzania wengi zaidi waelewe na kushiriki kwa upana zaidi kutoa michango yao. Pili wale wanaoshiriki katika maamuzi waweze kujielimisha zaidi na zaidi ili waweze kutoa maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. tumejifunza nini kwa kukamata yale makinikia? mapaka hivi sasa serikali ni kama inachezeshwa unyago na Barrick.
Hahaha unataka white paper kwenye eneo lao la kula?!
Hawatakaa wakusanye maoni kwenye hili, waka hata usiote.
Peleka tu maoni kama unayo lakini, hawawezi kukusanya maoni ya wananchi wote.
Wao wanasema kuyazuia makinikia kumefanikisha kuondoa mbaya wao ACACIA, wewe unauliza wamefanikiwaje?!
Huo ndio mtaji wao kisiasa, na ndio msingi wa uzi huu, wali miss construe statements za lisu kuhusu MIGA politically wao na wengi tusiofahamu, wakasema alipotosha ila wao ndio wako right.
 
hata mara ya kwanza shida ilikuwa sio kusafirisha. shida ilikuwa kutojuwa kinachozalishwa huko Japan.

Tuliambiwa hakuna kinachozalishwa ila mchanga wanasafirisha tu kama uchafu. JPM akasema basi wauache uchafu wetu. Mbunge Msukuma akasema kama uchafu mbona unalindwa sana toka machimboni hadi Dar?
Nasikia katika makubaliano yao-makinikia yataruhusiwa kusafirishwa na hiyo smelter siyo issue tena. Hii ina maanisha tumerudi pale pale.
 
Huo ulikuwa wimbo, enzi za Ukapa, kwamba tunalipa madeni, tunafunga mikanda, ikaundwa TRA tukawa tunakusanya kodi, wakaja na NIHF pilot. Na tukaambiwa tulisamehewa sehemu kubwa ya deni la taifa kupitia Oxfam na budget yetu ikawa imepunguza utegemezi kutoka kwa donor contries na ikawa inajitegemea up to 80%, sasa hapo ndio sielewi lini tumerudi nyuma mpaka 30 to 45%, and how do we fund our own mega projects at that level of dependence in our budget?! Na hili tunadanganywa?
Nilisema nitafuatilia, na nikasema kwa kumbukumbu zangu, hadi BM anaondoka madarakani, bajeti yake ilikuwa tegemezi kwa at least 40%... nilikuwa sahihi! Nimetafuta hotuba ya bajeti ya mwaka 2005 ambayo ilisomwa na Basil Mramba! Sehemu ya hotuba hiyo inasema:-
Bajeti.png

Halafu baada ya kuipitia kwa haraka haraka hii hotuba, kuna jambo limenishangaza sana... Mzee wa Msoga sijui alikuwa na nini!! Inaonesha watu wakifanya kazi bila shuruti hata productivity inakuwa kubwa! Kilichonishangaza ni jinsi alivyokuwa ameongeza mapato ya serikali maradufu kwa kulinganisha na yale aliyokuwa ameachiwa na Mkapa!!

Sehemu ya hotuba ya mwisho ya Mkapa inasema:-
Mapato.png

Yaani Mkapa kaacha mapato chini ya TZS 200 Billion kwa mwezi, Mzee wa Msoga kaacha takribani Sh. 900 Bilioni kwa mwezi!!

Hotuba kamili nimeambatanisha hapo chini!

Anyway, niongee kidogo kuhusu hilo la kusamehewa madeni!

Naweza kusema Mkapa aliingia na mguu mzuri... 1996 IMF walikuja na initiative iliyofahamika kama Highly Indebted Poorest Countries wakilenga kusamehe madeni kwa nchi 38 maskini zaidi duniani! Sharti lao la kwanza, walizitaka selected countries waoneshe nia ya kulipa... na Mkapa akaonesha hiyo nia, ndio maana alikuwa analipa kweli kweli ili Tz i-qualify initiative ya kusamehewa madeni!!

Baada ya ku-qualify, tukafutiwa madeni kwa sharti kwamba, zile tulizokuwa tunadaiwa badala ya kuzilipa tuzitumie kuboresha ustawi wa jamii in terms of Elimu, Afya na kuondoa umaskini wa kipato. Kufikia hilo, ndipo ikaanzishwa MKUKUTA... Mkakati wa Kupunguza na Kuondoa Umaskini Tanzania!

Kwahiyo mambo yoooote kuanzia Shule za Kata, MEM (Mpango wa Elimu ya Msingi), MES, MEMKWA, Kufuta Ada Shule za Msingi na Kupunguza Ada kwa Shule za Sekondari, na hatimae Elimu Bure pamoja na Zahanati kila kijiji bila kusahau TASAF... yote hayo chimbuko lake ndo hilo.
 
Attachments

hata mara ya kwanza shida ilikuwa sio kusafirisha. shida ilikuwa kutojuwa kinachozalishwa huko Japan.

Tuliambiwa hakuna kinachozalishwa ila mchanga wanasafirisha tu kama uchafu. JPM akasema basi wauache uchafu wetu. Mbunge Msukuma akasema kama uchafu mbona unalindwa sana toka machimboni hadi Dar?
Ndo maana kila wakati huwa nawaambiwa nyie kazi yenu ni kupiga makofi tu hata mkidanganywa!!! Yaani wanachosema wanasiasa na nyie mnakidakia kama kilivyo bila kutafuta ukweli!

Mwaka 2011, Tanzania Mineral Auditing Agency (TMAA) wakati wanatafiti commercial viability ya kujenga smelters Tanzania, walitoa viwango viwango vya madini mbalimbali vilivyomo kwenye makiniki kama ifuatavyo:-
Acacia.png

Sasa wewe ni nani ambae alikuambia kwamba wanachosafirisha ni uchafu tu?!

Na hata ukiingia kwenye tovuti ya Acacia, walikuwa wameeleza wazi copper concentrate ina-account asilimia ngapi ya mapato yao... na kama sikosei, ni zaidi ya 30% ya mapato yao!! Sasa tangu lini uchafu ukawa unatoa mapato makubwa kiasi hicho?!!

Ndo maana kila wakati hapa nimekuwa nikisema, ningekuwa JPM, kuwa na mashabiki aina yenu ningejisikia aibu sana kwa sababu ingeonesha wazi kwmaba hawa watu wananishabikia kwa sababu ama hawapo well informed au wapo tayari kushabikia hata wasichokijua!!!
 
walikuwa wanakwepa kodi..
kwa kisingizio cha mchanga hauna kitu.

Unawatetea Acacia ama?

wingi wa data sio always ni uwezo wa kuelewa.

kwa kukusaidia zaidi walikuwa wanapata zaidi ya ulivyotaja ikiwamo madini mengine mengi

Kodi waliyokuwa wanalipa kwa kinachotokana na mchanga hakikufanana na uhalisia wa walichokuwa wanapata Japan.

Hakukuwa na ukweli na uwazi... walikuwa wanatuibia... wakionesha they are not getting much from mchanga...

Google tena data uoneshe kuwa Acacia walikuwa wanalipa vizuri kodi. Na walikuwa wanatoa report sahihi ya wanachovuna toka kwenye mchanga.

Duh! Yaani nyie jamaa ni janga sana kwa taifa!!! Kwa kisingizio cha mchanga hauna kitu wakati unaona hapo wameorodhesha viwango vya madini ya aina mbalimbali?!

Kwa akili yako unadhani hizo takwimu zinatoka wapi kama sio kwa hao hao Acacia?! Sasa watasemaje mchanga hauna kitu na wakati huo huo wanatoa viwango vya madini vilivyopo?! Au watasemaje kwamba mchanga hauna kitu na wakati huo huo wanasema mapato yanayotokana na makinikia yana-account 30% ya mapato yao yote?!

Kwa mtindo huo, it's matter of time Magufuli aseme yeye ndie kafanikisha ujenzi wa hospitali ya Muhimbili, na hapo mtaanza tena kushangilia!!
 
Walikuwa wanapata zaidi kwa kiwango kipi?! Kile alichotaja Profesa Mruma sio?! Kama ndivyo, mbona hamjadai basi matrilioni yanayotokana na viwango vikubwa zaidi kama ambavyo mliambiwa na akina Profesa Mruma?1

Kwamba walikuwa wakionesha they're not getting much kwenye mchanga, nimeshakuambia hata ripoti zao zinaonesha mapato yanayotokana na copper concentrates ni 30% of total revenue!!! Sasa how come useme 30% "...not much?"
 
Acacia hawakuwa wanakwepa kodi?
Lissu nawewe mmeshinda [emoji16][emoji16]

Toa data ya kodi waliyokuwa wakilipa kwenye huyo mchanga..

kulikuwa na mazingira ya rushwa... walihonga wachache kukwepa kodi ya wanachopata kwenye mchanga.

Lissu alikuwa mteja wao.. Alifaidika sana.
Nawewe ulifaidika na dhulma ya mchanga?

compared to walichokuwa wanapata Japan sir....

Nn ngumu kuelewa?
Ama unataka Acacia wakuone waanze kukutumia kama Lissu?
Walikuwa wanapata zaidi kwa kiwango kipi?! Kile alichotaja Profesa Mruma sio?! Kama ndivyo, mbona hamjadai basi matrilioni yanayotokana na viwango vikubwa zaidi kama ambavyo mliambiwa na akina Profesa Mruma?1

Kwamba walikuwa wakionesha they're not getting much kwenye mchanga, nimeshakuambia hata ripoti zao zinaonesha mapato yanayotokana na copper concentrates ni 30% of total revenue!!! Sasa how come useme 30% "...not much?"
 
Acacia hawakuwa wanakwepa kodi?
Lissu nawewe mmeshinda [emoji16][emoji16]

Toa data ya kodi waliyokuwa wakilipa kwenye huyo mchanga..

kulikuwa na mazingira ya rushwa... walihonga wachache kukwepa kodi ya wanachopata kwenye mchanga.

Lissu alikuwa mteja wao.. Alifaidika sana.
Nawewe ulifaidika na dhulma ya mchanga?

..Duh!!

..Lissu alikuwa mteja wa acacia?!

..hebu tueleze alikuwa akinunua nini.

..alikuwa akinunua dhahabu, au makinikia?

..vijana wa uv-ccm hamna hoja mmebaki kuleta vioja.
 
kumbe alikuwa anawatetea bure?[emoji16]

Nilisema nitafuatilia, na nikasema kwa kumbukumbu zangu, hadi BM anaondoka madarakani, bajeti yake ilikuwa tegemezi kwa at least 40%... nilikuwa sahihi! Nimetafuta hotuba ya bajeti ya mwaka 2005 ambayo ilisomwa na Basil Mramba! Sehemu ya hotuba hiyo inasema:-View attachment 1241030

Halafu baada ya kuipitia kwa haraka haraka hii hotuba, kuna jambo limenishangaza sana... Mzee wa Msoga sijui alikuwa na nini!! Inaonesha watu wakifanya kazi bila shuruti hata productivity inakuwa kubwa! Kilichonishangaza ni jinsi alivyokuwa ameongeza mapato ya serikali maradufu kwa kulinganisha na yale aliyokuwa ameachiwa na Mkapa!!

Sehemu ya hotuba ya mwisho ya Mkapa inasema:-
View attachment 1241032
Yaani Mkapa kaacha mapato chini ya TZS 200 Billion kwa mwezi, Mzee wa Msoga kaacha takribani Sh. 900 Bilioni kwa mwezi!!

Hotuba kamili nimeambatanisha hapo chini!

Anyway, niongee kidogo kuhusu hilo la kusamehewa madeni!

Naweza kusema Mkapa aliingia na mguu mzuri... 1996 IMF walikuja na initiative iliyofahamika kama Highly Indebted Poorest Countries wakilenga kusamehe madeni kwa nchi 38 maskini zaidi duniani! Sharti lao la kwanza, walizitaka selected countries waoneshe nia ya kulipa... na Mkapa akaonesha hiyo nia, ndio maana alikuwa analipa kweli kweli ili Tz i-qualify initiative ya kusamehewa madeni!!

Baada ya ku-qualify, tukafutiwa madeni kwa sharti kwamba, zile tulizokuwa tunadaiwa badala ya kuzilipa tuzitumie kuboresha ustawi wa jamii in terms of Elimu, Afya na kuondoa umaskini wa kipato. Kufikia hilo, ndipo ikaanzishwa MKUKUTA... Mkakati wa Kupunguza na Kuondoa Umaskini Tanzania!

Kwahiyo mambo yoooote kuanzia Shule za Kata, MEM (Mpango wa Elimu ya Msingi), MES, MEMKWA, Kufuta Ada Shule za Msingi na Kupunguza Ada kwa Shule za Sekondari, na hatimae Elimu Bure pamoja na Zahanati kila kijiji bila kusahau TASAF... yote hayo chimbuko lake ndo hilo.
Asante, kwa hili nadhani zile taarifa zilikuwa za kwenye majukwaa ya siasa.

Nadhani wakati wa kikwete walipa kodi walikuwa wengi, ukilinganisha na kipindi hiki cha sasa.
 
kumbe alikuwa anawatetea bure?[emoji16]

..mtetezi wa accacia ni yule aliyewasamehe deni la 191 billion na kukubali kishika uchumba cha 300 million.

..na aliyeingia makubaliano mapya yatakayoruhusu makinikia kusafirishwa nje ya nchi badala ya kuchenjuliwa hapa Tz.
 
Binafsi mimi huwa sielewi hii misaada tunapewa lini na nani na pesa inaenda wapi?!
Kila siku nasikia deni la taifa linaongezeka, haya madeni ni sehemu ya hiyo misaada?! Au misaada na mikopo tunayokopa ni tofauti?!
Wewe mwenzetu misaada huwa unaipatia wapi?! Binafsi hadi leo hii na umri huu mkubwa sijawahi ona msaada tunaopewa kama taifa popote, naomba msaada kueleweshwa eneo hili la misaada.
Mzee ukiwa kiongoz ndo unakuwa mtanzania halali wa kuzijua tzs moneys ni hela ya nani
 
Wafuasi wa Lumumba ama kwa ile kukosa uelewa, au kwa makusudi tu, since Day 1 wamekuwa wakipotosha ambacho Tundu Lissu aliongea kuhusu MIGA! Au wakati mwingine inawezekana ni kutokana na tabia yetu Watanzania ya kutotafuta ukweli!

Binafsi nimekuwa nikilijadili suala la makinikia since Day 1, na kwavile nilikuwa nafuatilia sana nakumbuka vyema nini Tundu Lissu aliongea, na ninamnukuu hapa chini:-
Hiyo ndiyo hoja ya Lissu... kwamba, kama kweli Serikali ya Magufuli ilikusudia kupambana na Acacia, basi walitakiwa kwanza wajitoe kwenye mkataba wa MIGA!

Ushauri sawa na huo wa TL ulikuja tena kutolewa na Dr. Rugemeleza Nshala mbele ya Wabunge walipokuwa wanatafuta maoni ya wadai wakati wa utungwaji wa sheria mpya ya madini.

Gazeti la the Citizen linatujuza😛ia the Citizen wanatukumbusha kwamba, Dr. Nshala ni Mtanzania wa pili kutoa ushauri kama huo huku wa kwanza akiwa ni TL:-Kwa maajabu ya wale waliofuatilia suala la umakini, watu wakapotosha na kudai TL amesema tukipambana na Acacia, watatupeleka MIGA, na huu ndo umekuwa wimbo wa wana-CCM na wafuasi wa serikali!

Busara ya TL kushauri kujitoa MIGA unaweza kuiona kupitia tovuti ya MIGA, hivi ndivyo wanasema:-Hapo wanaongea wazi ni namna gani pamoja na mambo mengine, wana jukumu la kulinda uwekezaji dhidi ya maamuzi ya serikali!

Sasa basi, hoja ya TL ilikuwa ni kwamba, tukishavurugana na Acacia ,watakachofanya wao ni kile ambacho kinafanywa na kampuni zingine... yaani kukimbilia Mahakamani, au MIGA!

Lakini kama kweli umeamua kupambana na hawa jamaa, unachotakiwa ni kuchomoa betri kwa kujitoa MIGA ili wasiwe na kwa kukimbilia zaidi ya kwenda kwenye mahakama zetu wenyewe... yaani mahakama zile zile zinazoamua ma-DED wanastahili kusimamia uchaguzi ambao mmoja wa washiriki ni mwajiriwa wake mwenyewe!!!

Kwa maana nyingine, ukishajitoa MIGA maana yake ni kwamba unakuwa huzitambui mahakama zao! Ni kama United States asivyoitambua International Criminal Court, matokeo yake pamoja na uhalifu wote wa kivita wanaoufanya duniani kote, huwezi kumpeleka Mmarekani ICC .

Maajabu makubwa zaidi ya taifa hili, badala ya kuiangalia hoja ya TL Critically, watu wale wale wanaojiona ndio wazalendo zaidi, wakaona mtu kama TL anastahli kuuawa mara moja... na wafuasi wa CCM na serikali yake wamekuwa wakiirudia kauli hii mara kwa mara!!!!

Je, kumpuuza TL kumetugharimu kama taifa?!

Serikali na watetezi wataendelea kujitekenya wenyewe na kucheka wenyewe lakini ukweli ni kwamba imetugharimu kama taifa!

Sote tumeshuhudia danadana za Acacia... watetezi wa serikali wasichofahamu ni kwamba, danadana zote zile ni kwa sababu walifahamu maji yakiwazidi shingo, wangekimbilia mahakamani ambako katu tusingetoka.

Na kwa Mtanzania yeyote anayekejeli kauli hiyo ya TL, kwa hakika anatakiwa kujitafakari mara mbili... anatakiwa kujitafakari kwa sababu sisi ni victim wa hizi mahakama, hususani kupitia IPTL!

Sote sisi tunakumbuka kushikiliwa kwa Bombardier kwa wiki kadhaa kule Canada kutokana na maamuzi yaliyotolewa na mahakama za aina hii!!

Hivyo basi, ili kujilinda tusipelekwe kwenye mahakama kama hizi ambazo kuchomoka ni nadra sana, ndipo TL akasema ukitaka kupambana na hawa watu, basi jitoe MIGA lakini sio kwamba tukipamba na Acacia, wanatupeleka mahakamani!!!

Je, kwanini Acacia Hawajatupeleka MIGA?

Kwa kifupi ni kwamba, Acacia hawakuwa na sababu ya kutupeleka MIGA kwa sababu serikali imepita njia ambayo ni nafuu maradufu kwa Acacia!

Kuweka kumbukumbu sawa, wakati Profesa Orosso akiwakilisha Ripoti ya Pili, alitoa takwimu ya pesa ambayo serikali ilipoteza kama mapato! Prof. Orosso na timu yake waliweka makadirioo ya kiwango cha chini kabisa ambacho serikali ilipoteza, na kiwango cha juu kabisa!

Tuachane na kiwango cha juu kabisa, Profesa Orosso anatujuza, na ripoti kamili inapatikana tovuti ya Ikulu:-Hicho ndicho kiwango cha chini kabisa... na ukichanganya na adhabu (ya kuchelewesha kulipa kodi), jumla ndo ile figure maarufu ya TRilioni 450!!

Sasa hebu tujiulize... Uchunguzi uliofanywa na akina Prof Mruma na mwenzake Prof Orosso (pamoja na timu ya watu wa TRA), ilionesha Acacia wamekwepa kulipa Sh. 68 kwa miaka 17. Leo hii serikali imekubali kulipwa Sh. 700 Billion... sasa hata kama wewe ndo ungekuwa Acacia, ungeenda MIGA kufanya nini?!

Na kama ilivyo kwa mahakama zingine, kesi za MIGA zinachukua miaka na miaka!! Sasa kwanini ukae miaka yote hayo huku biashara ikiendelea kuathirika kwa kushindwa kusafirisha makinikia?!

Sasa wakati Wafuasi wa CCM na serikali yake wakiendelea kumkejeli TL kwamba mbona hao Acacia hawajaenda MIGA, jibu ndo hilo hapo! Hawajaenda kwa sababu sisi ndio tumeliwa! Tumekubali kuchukua Sh. 700 Billion out of 68 Trillion!!!!

NOTE: Moderator punguzeni kasi ya kuunganisha threads bila sababu za msingi eti kisa tu kuna baadhi ya keywords zinafanana!!! Kuandika haya mambo it takes time... so, it sucks mtu unapoteza saa moja na ushee kuandika thread, unakuja next time, huoni kwa sababu imeunganishwa na thread nyingine!
Mkuu chige naomba maoni yako kuhusu hizi initiative zote za serikali ya JPM,
1:Je kuna positive outcome yoyote iliyopatikana au itakayopatikana au serikali ingekaa tu kimya na kuendelea as usual na Accacia?
2:Je ushauri wa TL alioutoa ungefuatwa je kungekuwa na matokeo bora zaidi ya haya yaliyofikiwa?
3:Je report za Ossoro na Mruma ni kweli zilikuwa proffessional rubbish kama alivyosema TL? Kwa maoni yangu mimi zile report hasa ya Ossoro(economical ) ndiyo ili-trigger haya majadiliano na for sure i can say it was the good move by our government.
Nawasilisha mkuu
 
kuna namba 16% hujaiona
kuna 50/50 hujaelewa.
Ntakusaidiaje kuanzia hapo mkuu?
[emoji16][emoji16]

Back
Top Bottom