Acheni kupotosha alichokuwa amesema Tundu Lissu kuhusu Acacia na MIGA

Mimi binafsi naamini ushauri ule wa Lissu ulikuwa ni kipumbavu na usio na mantiki kabisa,

Endapo serikali ingefaya kama alivyoshauri Lissu,basi leo hii Tanzania asingekuwepo muwekezaji yeyote wa kimataifa.

Unachotakiwa kujua ni kwamba,hivyo vyombo kama MIGA vipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya hao wawekezaji wa kimataifa,


Hivyo basi,kitendo cha serikali kujitoa kwenye hivyo vyombo kisa tu wana mgogoro na mmoja kati ya wawekezaji wakubwa nchini,kingesababisha wawekezaji wa kimataifa kuona kwamba uwekezaji wao haupo salama tena ndani ya nchi,na hiyo ingepelekea wao kusitisha uwekezaji wao wote ndani ya Tanzania.


Jinsi hali ilivyo tu leo hii,kelele kibao zinapigwa juu ya kuvurugwa uchumi wa nchi,hebu niambie sasa,hali ingekuwaje kama wawekezaji wakubwa wote wangefunga virago vyao na kusepa?

Unaweza ukaona ni jinsi gani jamaa alitoa ushauri wa kipumbavu,kwa yeye kutokujua ama kwa makusudi kabisa.
 
You don't understand...!Mataifa wanatumia hoja ya kujitoa just for bluffing!! Mbele ya camera mnakaza kweli kweli huku mkionesha mnamaanisha!

Watu mnaweka vikao vya kitalaamu kujadili kujitoa, at the end unaitisha press kwamba tunapeleka taarifa rasmi ya kujitoa; na kweli unapeleka huku ikiwa na mapungufu kwa sababu mnajua in a week or two, or even a month, mtaambiwa wasilisheni upya; lakini hapo tayari unakuwa umeshaonesha nia kwamba "unaweza kujitoa"!

Na Magu vile alishaonesha ni wa aina gani, Acacia na mkubwa wao Barrick lazima chupi zingewabana tu... hata kama wasingetoa hizo trilions lakini wangetoa zaidi ya USD 300M! Hata kama wangetoa only 5% bado ingekuwa pesa ndefu sana!!

Na kimsingi, hata wale Acacia kwenda LCIA London, it's just a bluff!! Ule ulikuwa mchezo wa wote wawili... Acacia and Barrick! Wewe uliona wapi mwenye 64% ya hisa anasema "tuzungumze" yule wa 36% anajifanya kuvimba na kwenda mahakamani kwamba hatambui "makubaliano yenu!"

Na lengo ilikuwa kuwafanya serikali wafikie sehemu wajisemee "...heri nusu shari kuliko shari kamili... kwahiyo bora tulambe tu hii USD 300M tusije kukosa yote!" Na kweli wakaingia mkenge!!

The one who bluffs smarter is the winner!!!!

Lakini hata kama unajitoa... man, asikudanganye mtu!! Hakuna mwekezaji wa kweli atakayeshindwa kuwekeza nchini mwako eti kisa umejitoa MIGA!!! Hawa watu ni wasaka pesa popote ilipo! Watu wanaenda kuwekeza kwenye nchi ambazo kila siku makombora yanapita hewani ndo waogope nchi ambayo sio mwanachama wa MIGA!!!

Hilo kwao ni risk but risk pia kwao ni part of the business... the higher the risk, the higher the return!
 
Barrick walishatupiga tena tusubiri kuuguza majeraha ya vipigo tu
 
Kamanda kwenye issue ya mgogoro wa Accacia na Serikali Tundu alichemka,hasafishiki.
 
UCHUNGUZI HURU UMEBAINI KWAMBA LISSU THE GREAT NDIYE MWANASHERIA BORA KABISA KUWAHI KUWEPO KWENYE ENEO LA MAZIWA MAKUU TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI .
 
Kuna filimbi huwa inapigwa halafu tunapanga foleni pale viwanja vya Mnazi mmoja na bakuli zetu tunapokea misaada.
 

..alishauri tusitaifishe.

..serikali haikutaifisha.

..alisema madai ya usd 191 na ripoti za kina Prof.Mruma na Prof.Ossoro zina kasoro kubwa.

..serikali imeachana na madai ya 191 billion badala yake ime-negotiate, pia imeachana na ripoti za maprofesa.

..alisema tutashtakiwa miga. Kweli tulishtakiwa na kesi iliondolewa baada ya Tz kukubali "kishika uchumba" na minority shareholders wa accacia kununuliwa kwa bei waliyoridhia.

..alisema kama tunaona miga wanatuonea basi serikali ijitoe miga na migogoro yote kati ya Tz na wawekezaji wa nje iamuliwe na mahakama za ndani.

..serikali imepeleka bungeni sheria kwamba mashauri na migogoro ya uwekezaji itaamuliwa na mahakama za Tz.

..hili la kujitoa miga, Lissu alikuwa akishauri kwa mikataba mipya, siyo mikataba ya zamani.

..mwenye uelewa walikuwa wanajua kuwa anachoshauri Tundu Lissu ni sahihi.
 





Naona unazungumzia mambo kinadharia zaidi,
Alichoshauri Lissu ni kwamba kama serikali inataka kupambana na ACACIA bila kuburuzwa katika mahakama za kimataifa na kushindwa kesi(kunyolewa kwa chupa) basi hawana budi awali ya yote, kujitoa katika hivyo vyombo kama MIGA,hakuna sehemu aliyosema serikali itishie kujitoa.

Halafu unaposema kuwa serikali imeambulia pesa kiduchu sana (kishika uchumba tu) kwa kuzingatia deni ambalo serikari ilisema inawadai jamaa,
Je unafahumu lengo kuu la serikali lilikuwa ni lipi tangu mwanzoni kabisa mwa hilo sakata?


Imeshatokea kichwani mwako ukajiuliza kuwa pengine serikali ilikuwa na lengo lake lingine kabisa nyuma ya pazia tangu kusimamisha usafirishaji wa makinikia mpaka kuundwa kwa hizo tume na mwishowe kutangaza hilo deni lao la matrilion ya tshiling?

Vp kama lengo lao lilitimia kama walivyotaka wao na hicho kishika uchumba ni BONUS tu?
 
Tutashitakiwa MIGA ulikuwa ushauri kutoka kwa mwanasheria uchwara.
pamoja na ufafanuzi uliotolewa bado tu hujaelewa? you're a mere simpleton, imbecile and idiot. situkani hapa bali call a spade a spade. na hilo jina lako ondoa - li- libaki tu etwege. laana kwako zitapungua. ushauri wa bure!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…