ACT: Kutumia Tsh. Bilioni 27.8 kurekebisha Viwanja vya Amani na Gombani ni matumizi mabaya ya fedha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1 Uwanja.jpg

2 Uwanja.jpg

3 Uwanja.jpg
ACT Wazalendo, kupitia taarifa yetu kwa umma ya tarehe: 08/11/2024, tuliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka, hadharani gharama zote za matengenezo ya Viwanja vya Amani na Gombani ambavyo vimetangaazwa kufungwa ili kufanyiwa matengenezo, kutokana na taarifa yetu hiyo, Wizara ya Habari, Utamadui, Sanaa na Michezo, wakajibu kupitia taarifa, mbili kwa umma zilizotolewa, zilizotolewa tarehe 12/11/2024 na 13/11/2024, Chama cha ACT Wazalendo bado tunaamini kwamba, kuna hoja kadhaa ambazo hazijajibiwa na zinahitaji kujibiwa ili kuupa umma wa Wazanzibari haki ya kujua kinachoedelea katika uendeshaji na uwazi wa Serikali yao. Lakini pia jawabu za Wizara hio zimezaa masuali mengine mapya.

ACT Wazalendo tunaamini kwamba, kiasi cha fedha kitakachotumikaa katika matengenezo ya kiwanja cha Amani (New Amani Complex) cha dola za Kimarekani, 6,300,000 ambazo ni sawa na kiasi cha Shilingi za Tanzana 16,672,541,760 na kwa upande wa Kiwanja cha Gombani fedha zitakazotumika ni Dola za Kimarekani 4,250,000 ambazo ni sawa na kiasi cha Shilingi za Tanzana 11,247,349,600 ni fedha nyingi sana kutumika ikiwa viwanja hivyo vimetoka kufanyiwa matengenezo makubwa ndani ya miezi 11 tu iliyopita, hasa ukizingatia aina ya matengenezo yanayokwenda kufanyika katika viwanja hivyo, kwa kile kilichoelezwa katika taarifa ya Wizara kwamba “Ukarabati huu unaofanyika unatokana na vigezo na masharti yaliotajwa kwenye ripoti a wakaguzi wa viwanja wa CAF.”

ACT Wazalendo hatukubaliani na hoja kuwa matengenezo haya ya nyongeza, kuwa ni sababu ya ujio wa AFCON bali tuaamini inatokana na mipango mibovu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, ikiwa ni pamoja na kutotoa maelezo na matakwa ya kina tokea fikra yenyewe ya katengenezo ya viwanja na uchoraji wa michoro kwa miradi hio miwili.

ACT Wazalendo, tunaamini kwamba Taarifa hizo za Wizara ya Habari, Utamadui, Sanaa na Michezo hazikujibu hoja zetu, ambazo nazo pia zinatokana suala zima la kutokuweka utaratibu wa

watu wenye ulemavu kuingia ndani na kutoka kwenye uwanja na hata kuweka maegesho maalum ya magari na vipando vyao.

ACT Wazalendo, tumesikitishwa na Taarifa hizi za mbili za Wizara ya Habari, Utamadui, Sanaa na Michezo ya kutupa tu lawama ya jumla kuwa “ Wizara inasikitishwa baadhi ya Vyama vya Upinzani kupotosha ukweli na uhalisia wa taarifa hizi na kuchukua taarifa zisizo kamilika kutoka vyanzo visivyo sahihi.” Bila ya kujibu hoja zetu na kueleza ukweli ya yale tuliyoyaibua ili wananchi wapate kuujua ukweli hasa ni upi?

ACT Wazalendo, tunaitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, isipate shida ya kusema vyama vya Upinzani bali waseme bayana kwamba ACT Wazalendo kwani, sisi ndio tuliotoa hoja, na taarifa zisizo kamilika kutoka vyanzo visivyo sahihi kama wanavyosema wao, bali tumetoa masuali na kutandika hoja ambazo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo zinawajibu kujibu ili wenye mali zao ambao ni wananchi wa Zanzibar wajue kinachoendelea na sio kupiga danadana.

ACT Wazalendo, tunaamini bila ya shaka yoyote ile kwamba, tunao wajibu wa kikatiba wa kuhakikisha, tunalinda na kusimamia rasilimali za nchii hivyo tunatimiza wajibu wetu huo wa kikatiba, pamoja na maelezo hayo bado, tunaitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ijibu hoja zifuatazo ikiwa ni zile ambazo waliziacha na kutozijibu wakati wa kujibu zetu, kwenye taarifa mbili wazitoa:

1. Serikali itwambie baada ya matengenezo hayo kila Uwanja - Amaan na Gombani - utakuwa umegharimu kiasi gani cha fedha tokea kuanza kwa miradi hiyo hadi hatua hii iliyotangazwa sasa ili Wazanzibari ambao ndio walipa kodi wa nchi waweze kujua gharama halisi za ujenzi wa Viwanja hivyo.

2. Je, ujenzi huu wa udoho udoho umechangia kiasi gani kuongeza gharama ya pesa za kusimamisha miradi hio kutokana na kupanda kwa thamani ya dola?

3. Kutokana na Ujenzi wa Viwanja hivi ni kwa kiasi gani wanatayarishwa Wazanzibari, kuja kushika nafasi muhimu za utawala na ufundi wa viwanja hivyo hapo baadae?

4. Katika Ujenzi huo unaendelea Serikali imezingatia kwa kiasi gani kurekebisha kasoro ya kutokuwa jumuishi (inclusive) kwa watu wenye ulemavu?

5. Serikali ieleze kwa uwazi iwapo taratibu za fedha kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act) katika matengenezo haya zimefuatwa.

ACT Wazalendo, Katika suala hili la AFCON tuna maoni kadhaa kuhusiana na namna bora ya kuliendea jambo hili na tuko tayari kutoa maoni yetu, Serikali ikitukaribisha kama wadau kwa maslahi ya nchi.

Hata hivyo, hatutosita kutekeleza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali na kupambana na uzembe na ufisadi ambao umeota mizizi, lengo letu likiwa ni kuhakikisha fedha za walipa kodi masikini wa Zanzibar wanaokamuliwa bila ya huruma na watawala waliopo madarakani zinajulikana matumizi yake.

Imetolewa leo, tarehe 22/11/2024 na,
Ally Saleh Alberto
Msemaji wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Pia soma ~ ACT WAZALENDO: Serikali iweke wazi ni matengenezo ya aina gani na gharama gani yatakayofanyika katika viwanja vya Amani na Gombani

========================

TAARIFA KWA UMMA_page-0001.jpg

TAARIFA KWA UMMA_page-0002.jpg
 
Na bado wanasema hawataki ufisadi, Sasa hii ni Nini🤕🤕🤕🤕
 
"Africa is dying because we are electing THIEVES to be the leaders in our countries."

Prof. PLO Lumumba.
 
Back
Top Bottom