Ulifika ukashindwa kuingia?
Unaweza kuwaleta watu waliofika kwake tuwaulize?
Barua ya kujiudhuru haina nguvu, ukivuliwa uanachama unakosa nguvu ya kuendelea kubaki ofisini kwa kuwa unakosa udhamini wa chama. Ikumbukwe hatuna mgombea binafsi ktk sheria zetu.
Ukivuliwa unaweza kwenda kama Covid19. Huyu sidhani kama anaweza fungua shauri mahakamani kupinga mchakato husika.
Ikiwezekana ndg Kiranga ukafungue kwa niaba yake au watanzania kama alivyofanya Zito kwa Asad
Hujajibu maswali unauliza mengine.
Kwanza hiyo habari nzima ya mtu kwenda nyumbani kwake hailazimishwi kisheria. Hiyo ni distraction tu, kwenye sheria hakuna sharti la mtu kwenda nyumbani kwa mtu aliyetoweka ili ku file a habeas corpus motion.
So that whoke "ukienda nyumbani kwake?" point is moot.
Suala si barua ya kujiuzulu kuwa na nguvu au kukosa nguvu, suala ni kujibu kama barua ilikuwa yake ama la. Kwa sababu kuna hoja kwamba hakuandika yeye, sasa kama watu wanataka kujua aliandika yeye ama la, hilo suala zima la kufukuzwa uanachama hapo halipo, kwa sababu mtu anayetaka kujua kama barua iliandikwa na Nchimbi hata hajafika kwenye mambo ya kufukuzwa uanachama.
Tatizo wewe unaleta hoja ya mtu kwenda mahakamani kupinga mchakato husika wa kufukuzwa uanachama, wakati hoja yangu wala haihusiani na kupinga mchakato wa kufukuzwa uanachama, inahusiana na kujua ukweli tu.
Kuhusu mimi kufungua kesi, kama ACT wanafungua, hakuna haja yabkesi mbiki kwa jambo moja.
Hujaelewa hoja umeirukia tu.