Ukipata tip from chanzo fiche, ukataja umethibitishiwa na chanzo fiche, ujue unaponza watu!, utaitwa kuhojiwa na salama yako ni kukitaja hicho chanzo fiche chako!, hivyo ili to protect your source, unatumia an open source ya voices from within.
Believe me Dr. Nchimbi hajazuiliwa na yeyote, bali ameamua kuwa low profile, muda muafaka ukiwadia ataibukia kanisani.
Huu ushujaa wa kuuliza maswali magumu, niliishaufanyaga, niliponyang'anywa press card yangu, na ofisi yangu kufungwa, It was just me and my family!.
Juzi kati nimesema mahali kuwa jamaa ka mind kutoshangiliwa, JAB na TCRA wakanishukia, ile online channel ikafungiwa 90 days!
Nilipoandika Bunge linajopendekeza kwa serikali, aliyeitwa Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Bunge ni mimi, sio wasomaji wangu na sikuchangiwa hata nauli!.
Wanabodi,
Humu jukwaani tuko watu wa fani mbalimbali na miongoni mwao ni sisi watu wa fani ya habari.
Leo nimewakumbuka waandishi wa habari na kupotea/vifo vya kutatanisha, toka kwa Stan Katabalo, Ben Saanane, Azory Gwanda, Daudi Mwangosi, Josephat Isango, maajaliwa ya hatma za maisha yao, ni ama tuombe Mungu atunusuru na dhahama hizo, ama... (Ndio kama vile kilichomkuta Ben Saanane na Azory Gwanda, ni vanish into thin air hata unywele!)
Ukiwa ni mwandishi wa habari wa kawaida tuu au mtangazaji wa kawaida tuu, uandishi wa habari, ni kazi kama kazi nyingine yoyote, lakini ukiwa ni...
P
Pole, pengine tunawapa majukumu unfairly kwa kulinganisha na hali halisi ya nyumbani.
Let me grant that you are right, for the sake of argument.
Let us explore this decision and analyse what it really means.
Nchimbi kajiuzulu, kaamua kujaa kimya.
Kama ni hivyo Nchimbi kawasaliti wananchi, halafu kamsaliti Samia pia.
Yani kwenye moto hayupo, kwenye baridi hayupo, amekuwa vuguvugu na unajua kitabu kimesemaje kuhusu uvuguvugu.
Alitakiwa ama akomae asijiuzulu, ama akubali kuwa kashakuwa chawa wa mama asingelianzisha kabisa.
Kwa sasa ni kama kauwasha mto asioweza kuu control, amejionesha mdhaifu kisiasa, kafanya kitu bila strategy, hata baada ya kuona wanaofanya kitu bila strategy kama Polepole wanaishiaje.
Yani kawa kama mtu fulani rookie wa siasa za Tanzania kataka kusema maneno apate sifa tu, bila mpango endelevu akiliwa kichwa itakuwaje.
Sasa hivi kwa kujiuzulu na kuufyata mkia kavuruga pande zote mbili.
Samia anamuona msaliti kwa sababu kaleta mambo ya wanaharakati serikalini.
Wanaharakati wenye akili (achana na Maria na kundi lake hawajui hata ku stay on the message and not to be distracted by sideshows) wanamuona msaliti kwa sababu kakubali kujiuzulu kindezi wakati angeweza kama si kupigana, angalau kuelezea upande wake watu wajue kajiuzulu kweli hajauawa.
Kwenye hoja ya kuogopa kuuawa, Nchimbi alitakiwa kuwa na bonge la insurance policy kiasi CCM wangeogopa kumdhuru. Inaonekana hana, au kama anayo, haitoshi kuwaogopesha CCM.
But I also suspect Nchimbi is not as clean and principled as many people make him out to be, ana madudu yake kibao, akajisahau kusema sana. Na ukiwa si msafi hivyo, unakosa hata nguvu za kumwaga ugali, kwa sababu unajua ukimwaga ugali, wenzako watamwaga mboga.