ACT-Wazalendo kuwaponda CHADEMA kuwa hawana ofisi sio vizuri. Muwe mnawashauri kwa barua wajenge ofisi

ACT-Wazalendo kuwaponda CHADEMA kuwa hawana ofisi sio vizuri. Muwe mnawashauri kwa barua wajenge ofisi

Chuki inahusika hapa na si ukosoaji kwa nia ya kujemga. Isitoshe, CHADEMA teyari wameanza harakati za ujenzi wa ofisi zao karibu nchi nzima mbali na kujenga ofisi za makao makuu.
Bwashee ebu tuambie, kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu kiko wapi? Be honest please!
 
This is not good at all
[emoji116]View attachment 2359858
Ushauri murua kabisa, kwa hadhi ilikuwanayo, CDM ni vyema ikajenga ofisi za makao makuu zinazofanana nao. Wanapiga pamba kali sana, wanamiliki magari mazuri sana, wanafanya mikutano yao katika kumbi za gharama kubwa, hivyo vyote ni kithibitisho cha hadhi yao.

Sera za chama zina mlengo wa kibepari. Kwa hiyo ni wakati muafaka wa kuishi kutokana na sera, itikadi na malengo yao ya kimkakati ya kutwaa na kumiliki dola.

Si kila ushauri ni mbaya, ni vyema kuchuja na kutathimini mantiki iliyopo nyuma ya kile unachoambiwa na mshindani wako mara kwa mara. Sidhani kama CDM inashindwa kujenga na kumiliki jengo la thamani ya TZS 50Bn!

Tukubali tu, ukweli wakati mwingine ni mchungu bila hata ya kujali ni nani kausema.
 
Back
Top Bottom