ACT-Wazalendo kuwaponda CHADEMA kuwa hawana ofisi sio vizuri. Muwe mnawashauri kwa barua wajenge ofisi

Ushauri murua kabisa, kwa hadhi ilikuwanayo, CDM ni vyema ikajenga ofisi za makao makuu zinazofanana nao. Wanapiga pamba kali sana, wanamiliki magari mazuri sana, wanafanya mikutano yao katika kumbi za gharama kubwa, hivyo vyote ni kithibitisho cha hadhi yao.

Sera za chama zina mlengo wa kibepari. Kwa hiyo ni wakati muafaka wa kuishi kutokana na sera, itikadi na malengo yao ya kimkakati ya kutwaa na kumiliki dola.

Si kila ushauri ni mbaya, ni vyema kuchuja na kutathimini mantiki iliyopo nyuma ya kile unachoambiwa na mshindani wako mara kwa mara. Sidhani kama CDM inashindwa kujenga na kumiliki jengo la thamani ya TZS 50Bn!

Tukubali tu, ukweli wakati mwingine ni mchungu bila hata ya kujali ni nani kausema.

..50 bn for a party office building?! Hell NO!

..Cdm hawatakiwi kuwaiga Ccm kuwa na gharama kubwa za kuendesha chama.

..Kwamba Ccm wakiwa na ukumbi wa mikutano, Cdm nao waige na kumiliki wa kwao.
 
Sasa wewe tunazungumzia kitu cha msingi, ujenzi wa ofisi ya makao makuu ya chama, wewe unasema chadema imejenga ofisi mioyoni mwa watu! Ndiyo kitu gani sasa hicho?
Mku Itikadi Inaishi Rohoni kwani ni Imani kamili kama unavyoishi Imani yako. Yaani iwe Uislam au Ukristu.
Kwa hiyo Itikadi haishi mwilini au ktk majengo bali Rohoni Mku
 
Mbona kuna misikiti na makanisa.
 
Ushauri murua kabisa, kwa hadhi ilikuwanayo, CDM ni vyema ikajenga ofisi za makao makuu zinazofanana nao. Wanapiga pamba kali sana, wanamiliki magari mazuri sana, wanafanya mikutano yao katika kumbi za gharama kubwa, hivyo vyote ni kithibitisho cha hadhi yao.

Sera za chama zina mlengo wa kibepari. Kwa hiyo ni wakati muafaka wa kuishi kutokana na sera, itikadi na malengo yao ya kimkakati ya kutwaa na kumiliki dola.

Si kila ushauri ni mbaya, ni vyema kuchuja na kutathimini mantiki iliyopo nyuma ya kile unachoambiwa na mshindani wako mara kwa mara. Sidhani kama CDM inashindwa kujenga na kumiliki jengo la thamani ya TZS 50Bn!

Tukubali tu, ukweli wakati mwingine ni mchungu bila hata ya kujali ni nani kausema.
Huo ndio ukweli ni muda wa CHADEMA kujiimarisha katika kila idara,

Dotto hajasema uongo Ila chama kina jukumu la kutekeleza

Pia chama kiwafundishe wanachama wake umuhimu wa kujibu hoja kwa hoja na si hoja kwa matusi..
 
Ila CHADEMA inakera Sana

Chama tunakipenda Sana lakn kinashindwa kujenga ofisi zake

Kama hapo town wanaona ghali watafute hata kiwanja MBONDOLE au MSONGOLA wajenge

Mzee sabodo alitoa pesa had Leo sjui wamefanyia nn

Mikoani wanajitahid kujenga ofisi nzuri lakn makao makuu n aibu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Huo ukumbi uko katika ofisi za shadow cabinet research offices za ACT Wazalendo. Mimi ningependa kujua ziko mtaa gani Oysterbay. Kwenye jengo gani? Picha nyingine zinaonyesha kama vile wamekaa kwa kubanana kiasi.
Amandla...
 
Kitu kingine ni kuwa hamna mantik yeyote kwenye uwekezaji kwenye ukumbi unaotumiwa mara chache tu kwa mwaka. Ni heri kukodi na kuepuka gharama za kuhudumia wakati hautumiki.

Amandla...
 
..50 bn for a party office building?! Hell NO!

..Cdm hawatakiwi kuwaiga Ccm kuwa na gharama kubwa za kuendesha chama.

..Kwamba Ccm wakiwa na ukumbi wa mikutano, Cdm nao waige na kumiliki wa kwao.
Mkuu jengo lenye hadhi ya kuwa makao makuu linapaswa kuwa la kisasa na lenye vitu vingi muhimu. Mbali ya ofisi za viongozi kunapaswa kuwepo kumbi za kisasa za mikutano ya ndani, sehemu za Teknohama na mawasiliano, na nyingine nyeti kwa ajili ya ya ustawi wa chama.

Hiyo 50Bn mbona ni gharama ya kawaida tu kwa 'any sophisticated building"? Kutokana na "reputation risk" gharama kubwa za kifedha za uendeshaji wa taasisi yoyote ile imara huwa haukwepeki.
 
Mku Itikadi Inaishi Rohoni kwani ni Imani kamili kama unavyoishi Imani yako. Yaani iwe Uislam au Ukristu.
Kwa hiyo Itikadi haishi mwilini au ktk majengo bali Rohoni Mku
Illogical. Kwa hiyo tusijenge ofisi kwa kuwa imani huishi rohoni?
Kwa mawazo ya aina hii chadema itaendelea kudumaa kwa muda mrefu.
 
Mkuu jengo lenye hadhi ya kuwa makao makuu linapaswa kuwa la kisasa na lenye vitu vingi muhimu. Mbali ya ofisi za viongozi kunapaswa kuwepo kumbi za kisasa za mikutano ya ndani, sehemu za Teknohama na mawasiliano, na nyingine nyeti kwa ajili ya ya ustawi wa chama.

Hiyo 50Bn mbona ni gharama ya kawaida tu kwa 'any sophisticated building"? Kutokana na "reputation risk" gharama kubwa za kifedha za uendeshaji wa taasisi yoyote ile imara huwa haukwepeki.

..mambo ya ujenzi, umiliki, na utunzaji wa majengo yanahitaji utaalamu.

..siku hizi hata makampuni makubwa hayamiliki majengo ya ofisi bali hukodisha.

..binafsi sishauri Cdm washindane na Ccm kumiliki majengo makubwa-kubwa, kumbi za mikutano za kifahari, viwanja vya michezo, na ma-V8.
 
Mbona kuna misikiti na makanisa.
Kinachowapeleka ktk hiyo misikiti na makanisa ni kile wanachokiamini ambaya ni Imani hakuna anayelala nje so kumbuka hata ndani kwako ni Hekalu la Imani unayoishi.
Mku usicheze na Imani au Itikadi hivi vitu vinavunja mwamba kwani baki kuwaheshimu wanaoamini Imani zao na Itikadi zao.
Kama mm ninavyoiamini Itikadi ya Ccm ila tu baadhi ya matendo yananitatiza kiutendaji na ile mipaka ya kikatiba isivyoheshimika na ambao wanatakiwa kuwa wa mfano wa Taifa
 
Illogical. Kwa hiyo tusijenge ofisi kwa kuwa imani huishi rohoni?
Kwa mawazo ya aina hii chadema itaendelea kudumaa kwa muda mrefu.
Ukishajenga majengo ambayo huna wanachama yatakusaidia nini kumbuka hata chama changu ccm kinajengwa mpaka sasa na ushawishi wa wanachama baada kiishi Itikadi.
Chadema hawawezi kudumaa kwani wamekijenga chama kwa wananchi na wanachama wao.
Ukitaka kujua hili kaa mahali penye mijadala ya Kisiasa uone ni Itikadi gani zimeshika kasi ktk taifa letu yaani Ccm na Chadema ambayo imeenea nchi nzima sio chama cha msimu ndugu yaani si chama kinachoonekana kipindi cha uchaguzi tu.
Tafuta hotuba ya Mzee Msuya ktk kile kipindi cha dakika 45 cha ITV.
 
CUF kumbukeni kila mnachoongea kipo hadharani kwani pandikizi kuu lipo kipande hicho
 
Back
Top Bottom