Ushauri murua kabisa, kwa hadhi ilikuwanayo, CDM ni vyema ikajenga ofisi za makao makuu zinazofanana nao. Wanapiga pamba kali sana, wanamiliki magari mazuri sana, wanafanya mikutano yao katika kumbi za gharama kubwa, hivyo vyote ni kithibitisho cha hadhi yao.
Sera za chama zina mlengo wa kibepari. Kwa hiyo ni wakati muafaka wa kuishi kutokana na sera, itikadi na malengo yao ya kimkakati ya kutwaa na kumiliki dola.
Si kila ushauri ni mbaya, ni vyema kuchuja na kutathimini mantiki iliyopo nyuma ya kile unachoambiwa na mshindani wako mara kwa mara. Sidhani kama CDM inashindwa kujenga na kumiliki jengo la thamani ya TZS 50Bn!
Tukubali tu, ukweli wakati mwingine ni mchungu bila hata ya kujali ni nani kausema.
..50 bn for a party office building?! Hell NO!
..Cdm hawatakiwi kuwaiga Ccm kuwa na gharama kubwa za kuendesha chama.
..Kwamba Ccm wakiwa na ukumbi wa mikutano, Cdm nao waige na kumiliki wa kwao.