ACT Wazalendo: Maoni ya Upinzani kuhusu mabadiliko ya rasimu ya Uchaguzi hayazingatiwi

ACT Wazalendo: Maoni ya Upinzani kuhusu mabadiliko ya rasimu ya Uchaguzi hayazingatiwi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
dd1a0f50da7e50556363fbf7d393cf1a

Chama cha ACT- Wazalendo kimelalamikia kutozingatiwa kwa maoni ya vyama vya upinzani katika mchakakato wa mabadiliko wa maadili ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza leo na vyombo vya habari katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Magomeni jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewalazimisha kusaini maadili hayo bila kuzingatia maoni yao jambo ambalo amedai linaweza kuvuruga uchaguzi huo.

“Mojawapo ya kanuni mbovu ni ile inayosema kwamba kura zitapigwa, zitahesabiwa, matokeo yatapatikana yatajazwa kwenye fomu za matokeo, halafu nini kinafuata? kanuni hizi zinasema msimamizi wa uchaguzi anaweza kumpa wakala nakala ya matokeo kama kutakuwa na nakala za kutosha ,“ amesema Shaibu

Baadhi ya Kanuni zinazolalamikiwa katika rasimu hiyo ni pamoja na mawakala kudaiwa kunyimwa hati za viapo kwa mujibu Katibu Mkuu huyo utaratibu uliowekwa kikanuni wa wasimamizi wa uchaguzi kutuma orodha na utambulisho wa mawakala kwa wasimamizi wa vituo umeelezwa kuwa utatumika na wasimamizi wa uchaguzi wasio waadilifu kutowasilisha majina ya mawakala wa vyama vya upinzani.

Lingine ni kutoruhusiwa kwa waangalizi wa uchaguzi kuripoti katika vyombo vya habari wanapobaini mapungufu katika uchaguzi na kuwekewa masharti ya kuripoti mapungufu hayo baada ya uchaguzi kukamilika .

Malalamiko ya aina hiyo pia hivi karibuni yalitolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) John Mnyika ambaye hata hivyo alikiri kusaini maadili hayo kwa maelezo kuwa wataendelea kuzipinga ili kuepuka kukosa kushiriki uchaguzi iwapo chama cha siasa hakitasaini kanuni hizo kama iliyoelezwa katika rasimu ya kanuni hizo.
 
Tumesaini ndiyo lakini si kwamba tunakubaliana na yaliyomo...maana baada ya hapo kuna kuipitia na kuifanyia marekebisho
 
Vyama vya upinzani vya kweli kukubali kusaini kanuni za kihuni ni kujiweka wenyewe katika mazingira ya kufanyiwa uhuni
Zitto kabwe hana tofauti na Lipumba, mbatia na lyatonga.
Yumo maalim seif sharaf hamad.
 
Hao waneanza kuogopa Uchaguzi

Wasubirie October tuwakate ngembe
Ndugu comments zingine jaribu kumwogopa mwenyezi Mungu, haya ma itikadi tutayaacha duniani maana tumetakuta..

Kama mwenzio wanalalamikia jambo basi ujue something is wrong somewhere!!
 
Ndugu comments zingine jaribu kumwogopa mwenyezi Mungu, haya ma itikadi tutayaacha duniani maana tumetakuta..

Kama mwenzio wanalalamikia jambo basi ujue something is wrong somewhere!!

Mkuu ccm haina uwezo wa kushindana kisiasa, na wala uchaguzi huru hawautaki maana wanajua hicho ndio kitakuwa kiama chao.
 
Labda kama mtashinda kwa mtutu wa bunduki
Sheria na taratibu zote zitafuatwa, Ccm inashinda sababu imetekeleza ilani yake vuzuri. Tume ya uchaguzi inafanya kazi kwa kufuata katiba na sheria wala haina upendeleo.
 
Hizi zote ni kudanganya umma baada ya kubaini kuwa Ccm inakubalika na inaenda kushinda. Hakuna tume ambayo itawanyima mawakala nakala za matokeo. Au kumzuia muangalizi wa uchaguzi kuongea na waandishi wa habari. Acheni kupotosha.
 
Ndugu comments zingine jaribu kumwogopa mwenyezi Mungu, haya ma itikadi tutayaacha duniani maana tumetakuta..

Kama mwenzio wanalalamikia jambo basi ujue something is wrong somewhere!!
Waulize kwanza hao wapinzani kama wanajua maana ya kusaini!
 
Back
Top Bottom