PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Waziri Kivuli wa Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Mtutura Abdallah Mtutura, ameishutumu Serikali kwa kuwadanganya wananchi kuhusu ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.
Mtutura ameeleza kuwa kipimo mahsusi cha ufanisi wa bandari ni muda ambao meli inachukua tangu kuingia hadi kutoka (ship turnaround time), na kwamba uchambuzi wa takwimu rasmi za serikali za hali ya uchumi unaonyesha kuwa muda wa meli kukaa bandarini umeongezeka badala ya kupungua kama inavyodaiwa.
Akinukuu viwango vya huduma vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mtutura amebainisha kuwa meli za makontena zinatakiwa kukaa siku tatu au chini ya hapo, meli za shehena za kichele siku nne, na zile za vimiminika kama mafuta siku sita.
Hata hivyo, takwimu zinaonyesha hali ni tofauti, kwani wastani wa muda wa meli kukaa bandarini umeongezeka kutoka siku 3.8 mwaka 2021 hadi siku 9.6, huku meli za makasha zikifikisha wastani wa siku 12.7 mwaka 2024. Pia, meli za shehena za kichele zinakaa siku 13.7 na za mafuta siku 10.4, viwango ambavyo ni vikubwa mno kuliko vile vilivyowekwa na TBS.