ACT Wazalendo wakamata Kura Feki uchaguzi Mdogo Kata ya Kasingirima Kigoma zikiwa zimepigwa kwa Mgombea wa CCM

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
11,622
Reaction score
26,005
Kwenye Official Account yao ya X (Zamani twitter) ACT Wazalendo wamethibitisha kukamata kura hizo, na Kusema bado wanaendelea kuchukua Hatua stahiki ikiwa wao ni Moja ya vyama Shiriki kwenye Uchaguzi huo..

"Kura fake zimekamatwa zikiwa zinaingizwa kwenye vituo vya kupigia kura Katika Kata ya Kasingirima Kigoma. Kura hizo zimetiwa alama ya vema kwenye kiboksi cha mgombea wa CCM. ACT Wazalendo tumeshiriki uchaguzi huo".




Your browser is not able to display this video.
 
Dah yaani ni bora Watu tupige kura Online
Hapo ndio watachakachua vizuri mno. Sisi wengine tunaposema njia ya uhakika ni kupindua nchi mnadhani hizo njia nyingine hatuzioni? Nimeshapigwa mabomu na polisi kwenye uchaguzi, nimekoswakoswa na risasi za polisi kwenye uchaguzi. Tena polisi walikuwa wanawalinda wachakachua kura 🤣🤣🤣.



Yaani njia ya uhakika ni kupindua tu. Hata ikija hiyo katiba mpya na tume huru bado madudu yanaendelea 🤣
 
Hakika ni AIBU KUBWA kwa Chama kikubwa na kikongwe Afrika CCM kukamatwa na KURA FAKE zikiwa zimewekwa Alama ya TICK kwa MGOMBEA wake.

Kama Mtakumbuka MAKAMU MWENYEKITI wa CCM mh.KINANA alijinasibu kuwa Mh.RAIS SAMIA Ameahidi UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa wa 2024 na UCHAGUZI MKUU wa 2025 utakuwa HURU na HAKI hivyo WADAU wa UCHAGUZI waondoe HOFU waliyokuwa nayo ktk UCHAGUZI wa 2019 na UCHAGUZI MKUU wa 2020.

Binafsi naamini CCM inatest MITAMBO yake ya WIZI wa KURA utakavyokuwa 2024 na 2025 hivyo WATANZANIA Tutarajie yale yale Yaliyotokea Wakati wa UCHAGUZI wa SERIKALI za Mitaa 2019 na UCHAGUZI MKUU wa 2020 uliosababisha HOFU KUBWA WAPINZANI Kukamatwa na Kufunguliwa KESI za MAUAJI UTAKATISHAJI PESA UGAIDI na UHUJUMU UCHUMI na SERIKALI ya Rais MAGUFULI.
 
Kwani si ninyi kwa ninyi wenyewe!! Kuna shida gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…